Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Jumatatu, 2 Septemba 2013

UZINDUZI ULIOFANYIKA JANA UBUNGO PLAZA WA ALBAMU YA SHUJAA YA NEEMA GASPA NI WA KIHISTORIA

Siku ya jana kulikuwa na uzinduzi wa albamu ya Neema Gaspa inayoitwa SHUJAA katika ukumbi wa Ubungo Plaza hapa jijini Dar es Salaam. 

Waimbaji wengi waliweza kuimba na kumtukuza Mungu wetu aliye juu. Rose Muhando alionekana kukonga mioyo ya watu wengi. Ukumbi mzima ulisimama ukimshangilia Rose Muhando huku watu wakimfuata mahali alipokuwa akienda ndani ya ukumbi.

Watu wengi waliweza kununua albamu hii ya SHUJAA kutokana na uimbaji maridadi wa dada yetu Neema Gaspa. Ujumbe wenye kuelimisha, kufundisha na kuadibisha uliomo ndani ya albamu hii ndio uliofanya watu wengi kununua DVD hii.
Mkurugenzi wa Rumafrivca, Rulea Sanga naye alikuwepo kutafuta matukio
Mgeni Rasmi Mh.Anna Kajumulo Tibaijuka
Neema Gaspa
MC Boniface Magupa
Rose Muhando akifanya yake stejini....
Watu wakimfuata Rose Muhando popote alipokuwa akienda ndani ya ukumbi
Martha Mwaipaja
Aliyesimama ni mtangazaji wa Praise Power Radio, Christtina Mtua

KIPINDI CHA KUONYESHA MAVAZI YA MTU ALIYEOKOKA

KIPINDI CHA KUWASHUKURU WALIOFIKA KATIKA UZINDUZI
Neema Gaspa akiwashukuru waliofika ku-support kazi ya Mungu na kumuunga mkono kwa kazi yake ya SHUJAA


KIPINDI CHA KUUZA DVD
Mtangazaji wa PPR, Christina Mtua akiwa kikazi zaidi....



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...