Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Alhamisi, 6 Machi 2014

CHAKULA CHA BWANA ALICHOWALISHA NABII FLORA WAUMINI WA KANISA LAKE SIKU YA JUMAPILI 02.03.2014

Designer: Rumafrica +255 715 851523 www.rumaafrica.blogspot.com

  Biblia inasema: Wale waandishi wa mfalme wakaitwa pale pale, ilikuwa siku ya tarehe 23 ya mwezi wa tatu, kama vile Modekai alivyoamuru, Wayahudi wakaandikiwa pamoja na Maakida, na Maliwali, na wakuu wa majimbo toka bara hili mpaka Kushi, majimbo mia na ishirini na saba, kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; maana ya jimbo ni kipawa alituma kwa kila jimbo na akaandika kwa mwandiko wake, ukisikia kalamu, kalamu ni kipawa, sasa Mungu anakwenda kuachilia kwa majimbo mbalimbali.



Nabii Flora Peter akihubiri siku ya Jumapili

Biblia inasema: Katika barua hizo mfalme aliwaruhusu Wayahudi wakusanyike katika kila mji na kusimamia maisha zao; yaani simamia maisha yako katika mwezi Wasiwani, usikubali shetani aende kuharibu maisha yako, mimi sikubali hata mmoja kumpoteza, hata kufiwa nilishaapa sinta fiwa kwa UKIMWI, wala Kansa, Wala wachawi.


Biblia inasema: Bwana akawaruhusu Wayahudi kuuwa na kuangamiza; nasi tunakwenda kuuwa UKIMWI na kuangamiza, lazima vitu viangamie kama ni magonjwa yataangamia, UKIMWI utaangamia, umaskini na ufukara unakwenda kuangamia.



Isaya 61:1-4
Biblia inasema: Roho ya Bwana Mungu hii juu yangu, kwa sababu amenituma kuwahubiri wanyenyekevu habari njema, amenichukuwa ili kuwaganga waliovunjika moyo; anasema tazama Roho ya Bwana Mungu hii juu yangu, Bwana amenituma kuwaganga waliovunjika mioyo, haijalishi umejeruika kiasi gani, nimetumwa kukuganga wewe uliyevunjwa moyo wako.



Biblia inasema: Na kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao; yamkini umefungwa, unatembea lakini watu wameshakupiga pini, umepigwa biashara haziendi, ndani ya ndoa huna furaha, leo nimetumwa kuwafungua wale waliofungwa, nimetumwa kutangaza habari ya kufunguliwa kwao.



Biblia inasema: Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika, na siku ya kisasi cha Bwana, na kuwafariji wote waliao; nimekuja kukufariji wewe unayelia upate furaha badala ya maombolezo, badala ya sikitiko tukuvike furaha. Yamkini umefungwa biashara haziendi, haijalishi wamefunga nyota yako chini ya mvungu, chini ya dari tunakwenda kuitoa. Hatuwezi kushindwa nguvu za giza haziwezi kumshinda Yesu.

Kutoka 19:1
Biblia inasema: Mwezi wa tatu baada ya kutoka wana wa Israeli katika nchi ya Misri; na leo unakwenda kutoka katika mikono ya wachawi, walioiba nyota yako, Wa Israeli walitoka katika nchi wa Misri ilikuwa ni mwezi wa tatu, na leo nataka nikutoe unayenitazama kwenye youtube na kunisoma kwenye blogu na facebook nataka nikutoe katika mikono ya Wamisri. Leo ni siku ya kutoka kwako kwa jina la Yesu, wamefunga ndoa yako, kizazi chako, unakuwa ukifanya biashara zinafeli hao ni Wamisri, na leo unakwenda kutoka.

Biblia inasema: Wakapiga kambi huko huko wakiukabili ule mlima; leo tunapiga kambi tukiukabili mlima wa magonjwa, watu waliokufa lazima warejee, nyota yako lazima irejee, sitatulia wala sitanyamaza mpaka haki yako ipate kurejea.


Tembelea
www.nabiiflora.blogspot.com
JINSI YA KUFIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASLA KWA NABII FLORA PETER
Kama unatokea Mwenge, panda magari ya Tegeta, shuka Mbezi Mbuyuni, uliza kanisani kwa Nabii Flora peter

SEHEMU YA TANO: TAMASHA LA UZINDUZI WA ALBAMU YA MESS JACOB CHENGULA YA "MUNGU HABADILIKI" SIKU YA JUMAPILI 02.03.2013 -UBUNGO PLAZA DAR ES SALAAM

Kwa kweli tumeshuhudia matamasha mengi sana lakini hili la Jumapili lilikuwa la tofauti sana. Katika matamsha yaliyoongoza kuwa na waimbaji maarufu nchini Tanzania wanaomwimbia Mungu hili la Jumapili ni la kwanza, hatujui huko baadae. Waimbaji kukusanyika kwa pamoja zaidi ya 20 na kumwimbia Mungu si jambo rahisi. Hii ni kwa Neema tu ya Mungu. Mess jacob alikonga mioyo ya watu kwa ubunifu wake na juhudi zake za kuhakikisha waimbaji wote aliotarajia kufika wamefika, hata kama kuna baadhi hakuonekana lakini hakuna kasoro iliyotokea kwa mashabiki wa mambo ya Mungu.

Haya sasa,,,mzee mwenyewe, Mess Jacob Chengula akimtukuza Mungu na kumsifu kwa jinsi alivyomfanikisha kutimiza ndoto yake ya kuzindua albamu yake ya Mungu Habadiliki
Tamasha hili lilifanyika katoika ukumbi wa Ubungo Plaza na mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Mawasiliano Mh. Januari Makamba akiongozana na familia yake na baadhi ya watumishi wa Mungu kutoka katika kanisa la Mito ya Baraka kwa Askofu Mwakiborwa.
Katika tamasha hili kila mwimbaji aliimba kwa kiwango cha juu sana mpaka mgeni rasmi Mh Januari Makamba kuwaita baadhi ya waimbaji ili ashikane nao mkono kama ishara ya ku-appreciate kazi yao, mmojawapo alikuwa Edson Mwasabwite.
Dancers wa Mess Jacob Chengula wakifanya yao kwa utukufu wa Mungu
Baada ya uimbaji kufanyika, mgeni rasmi akiongozana na wachungaji na wazee wa kanisa kutoka katika kanisa la Mito ya Baraka kwa Askofu Mwakiborwa anakoabudu Mess Jacob Chengula walipanda jukwaani kwa lengo zima la kuiombea albamu ile na kuifungua rasmi.
Mgeni rasmi Januari Makamba alipomaliza kuizindua aliweza kuongea machache kuhusiana na waimbaji. Aliwapongeza waimbaji kwa ushirikiano wao waliuonyesha katika kumuunga mkono rafiki yao Mess Jacob Chengula. Alikipongeza Chama Cha Muziki Tanzania na viongozi wao kwa kazi nzuri wanayofanya kwa waimbaji wa nyimbo za Injili. Mh Januari Makamba aliwaalika viongozi wa Chama cha Muziki Tanzania na baadhi ya waimbaji kufika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano ili waweze kutoa matatizo yao na changamoto wanazopata katika huduma yao ya uimbaji.
Mh. Januari Makamba aliweza kuwaonya waimbaji wa nyimbo za injili juu ya style za uchezaji ambazo hazina baraka kwa mwenyezi Mungu kuziacha na kucheza kama vile Mungu anavyotaka watu wake wamchezee. Pia aliwaonya wale waimbaji ambao wamebarikiwa na kuwa maarufu sana, waachane na tabia ya kujivuna na kujiona wao ni wao. Mbali na kuwaalika katika Bunge, pia aliwaomba waimbaji na viongozi kutosita kufika ofisini kwake muda wowote na hakuna mtu atakayeweza kuwazuia kumuona hata kama atakuwa na majukumu mengi, lakini katika masuala ya Mungu kwa kupitia waimbaji na viongozi wa nyimbo za injili yuko tayari kusimamisha kwa muda na kuwasikiliza.


ZAMU YA MALIKIA WA NYIMBO ZA INJILI TANZANI ROSE MUHANDO KUFANYA YAKE STEJINI KWA UTUKUFU WA MUNGU BABA
Malikia wa Muziki wa Injili Tanzania Rose Muhando akifanya yake kwa utukufu wa Mungu
Rose Muhando akihakikisha kazi ya Bwana inasonga kwa uimbaji
Rose Muhando
Dancers wa Rose Muhando

MAMA JANUARI MAKAMBA KUMTUNZA ROSE MUHANDO WAKATI AKIIMBA STEJINI
Mke wa Mh Januari Makamba aliyeshika mkono mwanae akielekea stejini kumtunza Rose Muhando
Mama Januari Makamba na mwanae (kushoto) wakielekea katika kiti chao baada ya kumtunza Rose Muhando stejini

ZAMU YA MZEE WA NI KWA NEEMA TU, EDSON MWASABWITE KUMTUKUZA MUNGU KWA NJIA YA UIMBAJI
Edson Mwasabwite akiimba wimbo wake wa Ni kwa Neema tu

WAIMBAJI WAKIONYESHA UMOJA NA UPENDO WAKIWA STEJINI WAKATI EDSON MWASABWITE AKIIMBA
Kutoka kulia ni Atosha Kissava, Beatrice Mwaipaja, Neema Gasper na Tumaini Njole

ULIFIKA WAKATI WA MH. JANUARI MAKAMBA KUONDOKA BAADA YA ZOEZI ZIMA LA UZINDUZI KUFANYIKA
Mh. Januari Makamba akiwaaga waimbaji wa nyimbo za injili mara baada ya kumaliza zoezi la uzinduzi wa albamu ya Mess Jacob Chengula. Hapa anasalimina na Mwinjilisti Sarah Mvungi ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili na ni daktari

MADAMU RUTI WA JANA IMEPITA AKIMTUKUZA MUNGIU SIKU HIYO
Madam Ruti akiimba wimbo wake wa jana imepita
Madam Ruti akiimba wimbo wake wa jana imepita huku watu wakipokea baraka zao na mioyo yao kufarikika na kufurahi

UPENDO NKONE MAMA WA KULALAMIKA KWA NYIMBO ZAKE ZA HISIA AKIMTUKUZA MUNGU SIKU HIYO
Hata sasa vidole juu..Upendo Nkone kiboko, Mungu anamtumia ipasavyo kwa uimbaji

FARAJA NTABOBA KUTOKA CONGO HAKUKOSA SIKU HIYO KUMTUKUZA MUNGU
Faraja Ntaboba kutoka nchi ya Congo siku hii aliimba wimbo wa Yuko Mungu

TUMAINI NJOLE MWENYE MIONDOKO KAMA YA ROSE MUHANDO NA SAUTI KAMA YA ROSE MUHANDO SIKU HIYO ALIPAGAWISHA WATU KWA KUCHEZA NA KUIMBA
Tumaini Njole


MESS JACOB AKIFUNGA TAMASHA LAKE KWA UIMBAJI NA KUWASHUKURU WALE WOTE WALIOFIKA KUMUUNGA MKONO

Picha zimepigwa na RumAfrica
Tembelea
+255 715 851523
POSTER NA TIKETI NI KAZI YA RUMAFRICA. TUNAKUKARIBISHA
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...