Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Jumanne, 27 Agosti 2013

JIPATIE DVD YENYE UPAKO YA YESU NI SHUJAA YA NEEMA GASPA SIKU YA UZINDUZI WA ALBAMU HII 01.09.2013 UBUNGO PLAZA

Itakuwa siku ya Jumapili 01.09.2013 kwa kiingilio cha Shilingi 2000 kwa watoto, 5,00/= kwa v-oti vya kawaida na 10,000/= VIP Ubungo Plaza

DVD Cover limetengenezwa na RUMAFRICA +255 715 851523 www.rumaafricajobs.blogspot.com


Neema Gaspa DVD Cover

Neema Gaspa DVD Cover

Alhamisi, 15 Agosti 2013

FILAMU MPYA YA WITCH DOCTOR ITAKAYOKUELIMISHA WEWE MKRISTO


Umeangalia filamu nyingi lakini hii ni funga kazi. Kuna mambo mengi utajifunza kwa kupitia filamu hii ya WITCH DOCTOR, mbali ya hapo itakuelimisha, itakuadibisha na kukuburudisha. Usikose kununua copy yako.
Pata copy yako leo kabla copy hazijaisha...!!!!!



Mkurugenzi wa J-Film 4 Life  na mwigizaji wa filamu za Bongo Movie Tanzania, Jennifer Kyaka (ODAMA) katika studio za TBC1

Mkurugenzi wa Rumafrica Rulea Sanga na Mkurugenzi wa J-Film 4 Life Jennifer Kyaka katika studio za TBC1


Jennifer Kyaka akihojiwa katika kipindi cha Jambo TBC1

ASKOFU MWANAMKE WA KANISA LA LA KILUTHERI MAREKANI APATIKANA...!!!


Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Marekani (ELCA) tarehe 14/08/2013 limemchagua Bi. Elizabeth Eaton kushika nafasi ya uaskofu mkuu, alipata kura 600 dhidi ya anayemaliza muda wake Askofu Mark Hanson, ambaye alipata 287.

Askofu Eaton, ambaye ni Askofu wa ELCA Cleveland, ni mama na mke wa Mchungaji Conrad Selnick. Mtumishi Eaton anaungana na Askofu Jefferts Schori Katharine, ambaye mwaka 2006 alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuliongoza kanisa la Anglikana duniani.
Eaton ataongoza kanisa kwa miaka sita (6) kuanzia mwezi Novemba mwaka huu.

UPENDO NKONE CHRISTINA SHUSHO NA DANILE KIZA KUITIKISA UK KWA NJIA YA UIMBAJI.


BARBER SHOP MPYA MAFINGA OPENING SOON


Wakazi wa Mafinga - Iringa kaaeni mkao wa kunyolewa na vinyozi wa kimataifa watakaokuwa wakiwahudumia katika Barber Shop mpya ya kisasa na ya kimataifa ya kijana wenu na mkazi wa Mafinga Unique Sanga. Unaweza kuwasiliana naye kwa simu +255 652 958639

Tangazo limetengezwa na RUMAFRICA. Ukituhitaji wasiliana nasi kwa simu +255 715 851523

WATU WAKO "VERY BUSY" KUMTAFUITA MUNGU KWA KUSOMA NENO LAKE KATIKA KANISA LA YESU KRISTO LA HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASALA KWA NABII FLORA PETER. HII ILIKUWA TAREHE 28.07.2013



UJUMBE WA LEO UNATOKA KATIKA KITABU CHA KUTOKA 9:8..
Nakukaribisha sana katika mwezi huu, kabla hatuja ingia mwezi Buni tulikuwepo katika mwezi Ethanimu. Niliweza kuzungumza nikasema ndipo Bwana akasikia arufu njema, baada ya kutua ile Safina katika Mlima Hararati.

Ilipokuwa imetua ile Safina Nuhu alichukua mke wake na watoto wake, na kila mnyama aliyekuwa na uhai akamtolea Mungu, ndipo Bwana akasikia arufu njema na ya kuridhisha.
Aliposikia arufu nzuri na ya kuridhisha akasema sinta ipiga hii nchi tena, lakini ndipo tukakumbuka kipindi cha Nabii Musa,walipo kuwa wamejiinua waganga na wapiga ramli katika lile taifa. Kama wanavyojiinua hapa Tanzania, wamekuwa wakipoteza watoto kila siku, zimekuwa ni kesi za watu kufa kufa, ajali zisizoeleweka.
Sasa Mungu akaniambia jitwalie konzi ya Tanuuni, uende kuitupa juu, majivu yatatembea nchi yote, alafu ufanyavyo hivyo patatokea majipu makubwa, yenye kufura na yenye kutumbuka na kutoa usaha. Ili waiachie nchi yetu tupate maendeleo, tufanye kazi, watu wafanikiwe, watu wamuone mungu, fanya kazi kwa bidii utafanikiwa.
Ninakwenda kumkamata na kumwaribu adui yako, watupishe tupite, lazima watupishe tupenye, lazima ukuta uanguke tuvuke. Yeyote aliyekuzuilia mambo yako nakwambia leo lazima atapisha utapita, haijalishi leo nakwenda kuteketeza mahitaji yetu. Ndipo litatokea vumbi kwa maadui zako, wataota majipu yenye kufura na kutumbuka, mengine yatakuja mpaka usoni.
Sikubali kuona watu wanateseka, ninakataa lazima iwe. Aliyekuchukulia mume litatokea jipu lenye kufura na kutumbuka tena lenye usaa yatatokea. Nakwambia hata akienda kwa waganga watashindwa kupiga ramli, leo ni siku yako ya kukukomboa juu ya adui yako, aliye zuia muujiza wako nakwambia leo ni siku yake ya kupigwa.
Ndio maana wanasema Yesu alimpiga Yeriko kuta zikaanguka, na mimi napiga kuta zianguke, lazima kuta zianguke ndani yako, hata kama ameweka jiwe la gubegube leo nalivunja lazima iwe. Lazima leo niangushe ngome, kunatatizo linalokusumbua leo lazima liangushwe, kama Daudi alivyompiga Goliati jiwe moja akaanguka.
Aliyechukua mume wako leo ataachia, aliyezuia cheo chako namtwanga leo, Nabii ni kichwa cha Mungu ameyasikia Mungu mateso yenu. Ameniambia shuka nami niatapiga maadui zenu, tumechoka kuonewa, lazima Yesu aonekane.
Bwana akawaambia Musa na Haruni, jitwalieni konzi za majivu ya tanuuni kisha Musa na ayarushe juu kuelekea mbinguni, mbele ya Farao. Nayo yatakuwa ni mavumbi membamba juu ya nchi yote ya Misri; Farao ni adui anayekutesa, yaani Nabii Flora ayarushe juu yale majivu ya tanuuni, Misri ni watu wasiomjua Mungu.
Nayo yatakuwa ni majipu yenye kufura na kutumbuka, juu ya wanadamu na juu ya wanyama katika nchi ya Misri. Basi wakatwaa majivu ya tanuuni na kusimama mbele ya Farao; wanaokusema juu yako, wanaokuloga usiku kucha, utakuwa na majipu makubwa yenye kufura nakufungua. Farao ni ugonjwa ulionao, pamoja na mateso uliyonayo, wamezuia usiolewe wamefunga funga uchumba wako lakini leo nimesimama.
Lazima umuone Yesu alzima ufanikiwe, aliyezuia atapata majibu, anayezuia usiolewe majipu yatakuja kwake, anayezuia usizae, nakutamkia atapata majipu yenye kufura. Anayezuia mambo yako kwamba usifanikiwe.
Basi wakayatoa majivu ya tanuuni, kasha Musa akayarusha juu mbinguni; umepima ukakuta bado tarajia uzima, lakini uzima upo mahali hapa. Aliyeokoka hawi na Virusi, ukija hapa lazima Virusi viondoke, Mungu wetu ni mwaminifu, tumesikia kijana aliyekuwa amefungungwa kifungo cha maisha ameweza kutoka. Na pia tumesikia ushuhuda watu wamepona magonjwa yote UKIMWI, Kansa wamekuja na vyeti vyao.
Picha zimepigwa na Rumafrica +255 715 851523
You might also like:

Jumatatu, 12 Agosti 2013

RUMAFRICA YAFUNGULIWA MACHO JUU YA UZINDIZI WA ALBAMU YA SHUJAA SIKU YA TAREHE 01.09.2013 UBUNGO PLAZA JIJINI DAR


Ki ukweli mimi kama Rumafrica sijui zimebaki siku ngapi ila ninachojua ni kwamba tarehe 01.09.2013 ndio siku ya uzinduzi wa albamu ya SHUJAA ya Neema Gaspa.

Kilichonishangaza na kunifanya nijiwekee pesa kwaajili ya kiingilio ni ule  ujumbe alioubeba mwana wa Mungu Neema Gaspa katika albamu yake. waimbaji watakaoimba ni wale ambao kiukweli nyimbo zao zinaupako mkubwa na hili si la kuficha kwani unajua....

Nilikuwa najiuliza ni kiasi gani kinahitajika ili watu wote waingie katika kujimwaga kwa Yesu. Neema aliweza kuniambia ya kwamba, watoto ni Shilingi 2,00/= viti vya kawaida in sh. 5000/= na VIP ni sh. 10,000/= na issue nzima inaanza saa 7 na kuendelea mpaka hapo baadae.

Nikajiuliza tena, hivi Neema anaupako gani mpaka akamshauri Mh. Samweli Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania  kuwa mgeni rasmi, Roho wa Bwana akasema, "Kwa Mungu kila jambo linawezekana"

Mimi kama Rumafrica ninaomba sana Mungu anipe uhai na afya njema siku hiyo nishuhudia kazi ya Mungu inavyofanyika na watu wake wanaompenda Mungu na kufanya kazi yake bila kujali gharama.

Unaweza pia ukajiuliza kuwa tiketi utapata wapi?  Ninaamini unajua sana kituo cha Radio cha Wapo (Kurasini) na Praise Power (Mikocheni) huko ndiko unaweza kupata na kama unaona mbali au umebanwa na huwezi kwenda huko basi njoo siku hiyo ya tamasha na utapata mlangoni. Halijaharibika jambo.

Ninamshukuru sana Mungu kwa kuweza kumuwezesha Neema Gaspa kufanya kazi ya matangazo na RUMAFRICA.
Kazi imefanywa na Rumafrica Tanzania. Wasiliana naye kwa simu +255 715851523 au kwa B/Pepe: rumatz2012@gmail.com

SHUHUDA KATIKA IBADA YA JUMAPILI 28.07.2013 KANISA LA YESU KRISTO LA HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASALA KWA NABII FLORA PETER


Mpiga Picha: Rumafrica +255 715851523

BABA ALIYEKUWA NA KANSA YA KIFUA SASA AMEPONA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Thadeus Mchomvu;  nilikuwa naishi Mikocheni B, toka mwezi wa tano mwaka jana nilikuwa na matatizo ya kifua. Nilienda hospitali wakanipima wakaniambia sina TB wala tatizo lolote, mwezi wa nane mwaka jana nilianza matibabu ya TB lakini baadae nikiwa Hospitali wakasema sio TB tena wakagundua ni Kansa.  
 
 Lakini nilikuwa nimeshachelewa, nikaambiwa niende Ocean Road, basi wakaniifadhi Hospitali moja ambayo ipo Tabata City Council.  Basi pale nilitibiwa lakini Doctor aliniambia nimechelewa sana, ikabidi nianze kuja kwenye maombi nakumbuka nilifika hapa mwezi wa 8, kuna mtoto wangu aliniambia kuna mama mmoja anaitwa Nabii Flora anaombea watu na wanapona. Basi nikaja hapa nikaombewa, nakumbuka Nabii Flora aliniambia Mzee utapona, nashukuru Mungu kweli nimepona, kwa maana mwezi wa kwanza mwaka huu nilipimwa nikaambiwa sina dalili yoyote  ya Kansa.  Namshukuru Mungu na Bwana sifiwe, (kwa kweli tulifika hapa Nabii akasema hutakufa baba utapona, alikuwa amezidiwa akawa hawezi hata kuongea lakini Mungu wa Nabii Flora ni wa ajabu, nashukuru sana Nabii nakumbuka ulinimbia mama hautakuwa mjane).


 Wakicheza baada ya kusikia ushuhuda wa baba aliyepona kansa

MAMA ALIYEIBIWA VITU NYUMBANI KWAKE SASA VIMERUDI
Bwana Yesu asifiwe; nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa mema aliyonitendea na maajabu aliyonionyesha ndani ya madhabahu hii.  Ndani ya wiki tatu zilizopita niliibiwa na kijana wangu wa kazi, kijana ambaye nilikaa naye kwa muda wa miaka mi tatu, kijana alikuwa mwema mzuri kabisa akuwa na tatizo lolote. Lakini kwa bahati mbaya siku moja tuliondoka nimeenda kazini narudi jioni, nikakuta kijana hayupo kuingia ndani nikakuta laptop yangu haipo pesa pamoja na nguo chache. Basi tukashauriana tukasema tukaripoti polisi, basi polisi wakajitahidi sana haikuwezekana, tukamtafuta ndugu yake akatuelekeza mpaka  kwao Mtwara. Tukafunga safari kwenda Mtwara, tulikwenda mpaka Mtwara tukisaidiwa na watu wa kijijini hapo, tukafika mpaka nyumbani kwao lakini kwa bahati mbaya hatukumpata kijana yule. Basi tukarudi mimi nikasema kwa nini tusimwachie Mungu sasa kwa sababu kwa mikono yetu na nguvu zetu tumeshindwa . 
Nikaja nikamfuata Nabii nikamweleza tatizo langu, Nabii akaniambia haitawezekana atarudi mwenyewe na atarudisha kila kitu. Nabii akaniambia na kule alipo hata lala, atakula na wala hatapata usingizi, basi wapendwa ndani ya wiki tatu kijana Yule amerudi nyumbani. Amehangaika kutoka Mtwara hana nauli hana chochote lakini alikuwa anaomba magari ya mizigo ili aweze kufika Dar es salaam, Mungu alivyo mwema akamrudisha Dar es salaam akaja mpaka nyumbani.  Kijana alikuja akiwa anatambaa  akaniambia mama ni mimi nimekuja naomba unipokee, basi ile laptop ilikuwa imeuzwa mara nne, yaani kila aliyekuwa anauziwa alikuwa anauza tena.
Basi mtu wa mwisho alisema naombeni mnipe muda naisafirisha alafu nitaleta tena, kijana yule chini ya ulinzi wa serikali, asubuhi alituma mtu askari akapiga simu akasema mama njoo uangalie kama  unaweza kuitambua laptop yako.  Basi nikaenda pale nikakuta ile laptop nikaitambua nikamwambia mheshimiwa  ndiyo laptop yangu hii, akaniambia kama ni kweli naomba uchukue hii laptop, kwa kweli namshukuru Mungu nilishangilia nilifurahi moyoni. Lakini niimwambia Nabii kijana yule alinifanyia makosa lakini mimi nimemsamehe, basi nilirudi hapa kwetu kwenye madhabahi yetu hii ya Nabii Flora, muheshimiwa Nabii Flora akaniambia kijana yule aje aonane nae. Natoa ushuhda huu nikiwaambia wakristo wenzangu msichezee madhabahu hii, Mungu wa Nabii Flora anatenda kweli na anatenda sasa, ana kesho anafanya sasa namshukuru Mungu.

BABA ALIYEKUWA HATAKI KUTUMIKA KIMWILI, ATUMIKE KIROHO SASA AMEFANIKIWA
Bwana Yesu asifiwe; mnanifahamu mimi ni mtumishi hapa mchungaji, wiki iliyopita nilikuwa na workshop sikuweza kuja hapa kuhudumu kwa wiki yote hii. Nabii alikuwa ananiombea kwa sababu miaka yangu mitatu pale Akiba Commecial  Bank  (ACB)nikiwa Mkurugenzi. Kulikuwa na changamoto kubwa kwa sababu nipo kwenye huduma ya kiroho na nipo kwenye huduma ya kimwili, mashirika yanaendeshwa kimwili na tena Jumatatu nilipata Email kutoka Uingereza ambayo inasema niende miezi 6 orientation course kwa hiyo nikawa na changamoto kubwa.

Kutokana ushuhuda wangu Bwana Yesu alinitokea katika huduma yangu, kwa sababu nilikuwa nasema nitatumikaje kimwili na kiroho, basi nikasema nitapata jibu siku ya jumamosi kama nitachaguliwa kuwa Mkurugezi ambayo inaendeshwa kimwili. Niliomba sana na nilimuomba Nabii anisaidie kuoma, roho wa Bwana namshukuru kwa sababu kwanza  hakuniaibisha, tulikuwa watu wanne ambao tunagombea kuchukua nafasi moja. Sasa Roho Mtakatifu ameongea na mimi kwamba hizi kazi za kimwili sasa ni mwisho wangu, kw hiyo akampa mtu ambaye ana PHD mimi nikawa nafasi ya pili, kwa hiyo hakuniaibisha kuwa nafasi ya mwisho, hilo namshukuru Bwana Yesu kwa sababu hakuniaibisha.

DADA ALIYEKUWA H APATI UJAUZITO SASA ANAUJAUZITO
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Junith Salvatori; mimi nimeolewa na mume wangu nina miaka saba, tangu miaka hiyo nilikuwa sijafanikiwa kupata mtoto. Nikaja hapa mwezi wa nne mwaka huu, Jumapili ya Pasaka nikawa nahudhuria ibada hapa, namshukuru Mungu wa Nabii Flora sasa hivi ni mjamzito.

DADA ALIYEKUWA AMEATHIRIKA PAMOJA NA MTOTO SASA WAMEPONA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Priska Andrew natokea manyoni;  kuna rafiki yangu alinipigia simu akaniambia huku Dar es salaam kuna Nabii anaponyesha virusi vya UKIMWI ndo nikafunga safari mpaka hapa kwa nabii Flora. Nimekuja hapa ilikuwa tarehe 8, tarehe 9 nikaonana na Nabii nikamwambia mimi nimeathirika tupo na mtoto, akaniambia nenda kwanza kapime ili uniletee cheti cha positive ndio nikuombee.

Tarehe 10 nikaenda kupima na mtoto wangu ambaye naye alikuwa na UKIMWI, nikaleta vyeti vya positive, akaniombea akasema nakupa siku 7, kabla ya siku 7 akaniambia nenda kapime umepona, nikaenda kupima pamoja na mtoto nikakuta negative, namshukuru sana Mungu.

MAMA MISS KANDA MASHARIKI TANZANIA 2004/2005 APONYWA KANSA (KULIA)
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Asha Selemani;  nilikuja hapa nikiwa na tatizo la Kansa, na mwanangu alikuwa na HIV. Lakini namshukuru Mungu wa Nabii Flora, mwanagu kabla ya siku 21 alizopangiwa akawa amepona, na mimi Kansa nimepona, namshukuru Mungu sana wa mahali hapa
 Kulia ni mama wa miss kanda mashariki Tanzania 2004/2005 ambaye mwanae alipona UKIMWI
DADA ALIYEKUWA NA UVIMBE PAMOJA NA MIRIJA KUZIBA SASA AMEPONA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Felista; nilikuja hapa mwezi wan ne na uvimbe na mirija imeziba, nilikuwa nasumbuliwa na tumbo sana nikamuuliza rafiki yangu anaishi huku Salasala anaitwa Frida. Nilivyoenda kupima niliambiwa natakiwa nizibuliwe mirija na niafanyiwe operation, nikawa naumia sana sijazaa sina mtoto nikatobolewe mirija saizi itakuaje, nikakataa kabisa. Baada ya kuongea na rafiki yangu akaniambia twende kuna Nabii yupo Salasala, nikamwambia mimi nafanya kazi kwa wahindi sina hata muda wa kutoka, lakini nikawa nakaa naumia nasema ipo siku Mungu atanisaidia nitatoka nitaenda. Kweli kuna siku nikafanikiwa nikaomba ruksa nikaja, nikaonana na mama nikamueleza, akaniambia nihudhurie Jumapili 4 nami nitafunguliwa, nikaja kwa imani. Baada ya hapo nikawa nimebanwa kazini sikuwa naonekana hapa, nikawa nimepelekwa Morogoro, nikatoka nikaenda Kigoma, huko nilipokuwa nikaenda kupima maana nilipewa wiki 4 nitakuwa nimepona.  Kwenda  kucheki Doctor akaniambia huna tatizo lolote, nikamwambia hapana mbona niliambiwa nina uvimbe alafu mirija yangu imeziba kwa sababu mimi ni nesi na nilienda kupima kwa mtu ninayemfahamu, kwa sababu alinihakikishia kabisa.
Baada ya kurudi nikasema haiwezekanani mpaka jumapili niende Kanisani, nikawaambia wale wahindi mimi sintakuja nina matatizo kwa sababu usipo aga unamatatizo hupewi hata ruksa. Leo nikaamka asubuh saa 10 nikawachukuwa wadogo zangu nikaja nao. Nilienda kupima Kijibwan ena doctor ambaye ninamfahamu, akanicheki tena hakakuta sina uvime, nikaenda tena Mnazi mmoja nikaambiwa sina uvimbe. Nikaenda tena kule vijibweni akanipima Yule Doctor akanionyesha kila kitu kinavyoonesha sina uvimbe, nikamwambia mbona mimi nilishapimwa na vyeti hivi apa ninavyo, akaniambia basi tucheki tena , akakuta sina uvimbe lakini sikumwambia kuwa nimekuja kwenye maombi. Nikamshukuru M<ungu kwa kweli  nimepona uvimbe maana nilikuwa na wasi wasi, na sasa hivi nimepata mchumba nilikuja hapa nikamwambia mama akanitabiria, na nimetolewa mahari na pete nimevalishwa tutafunga ndoa mwezi wa 10. Namshukuru Mungu wa Nabii Flora.

DADA ALIYEKUWA HIV SASA AMEPONA (MISS TANZANIA)
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Martha Julius; nilikuja hapa mwezi wa sita, nilikuwa na tatizo la HIV nikaonana na Nabii, akanipa maombi ya siku 21. Nashukuru Mungu ndani ya siku 21 nikawa nimepokea uponyaji, na baada ya kupona nikawa nimewataarifu wenzangu ambao walikuwa na tatizo kama langu, yule dada wa Nairobi, Bibi mzungu wa Upanga pamoja na Nurati ambae amepokea uponyaji  Jumapili iliyopita baada ya ibada.
Wa pili kutoka kushoto ni Miss Kanda Mashariki 2004/2005 Martha Julius
DADA ALIYEKUWA NA HIV SASA AMEPONA NA NI MJAMZITO SASA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Anna James; namshukuru sana mama yangu Nabii Flora, nilifika hapa nikiwa na HIV mwezi wa 11 mwaka jana. Ilipofika mwezi wa 3 tarehe 2 mwaka huu nikapona HIV, nilipokuja hapa nilikuwa na CD4 96, baada ya kuhudhuria maombi ya miezi mi tatu nikawa na CD4 341.

Tumeishi na Virusi vya UKIMWI toka mwaka  2001, na nilivyo kuja hapa nikamwambia Mchungaji Komba maadamu mwenzangu wameacha magongo na mimi nitaacha dawa zangu hapa. Na baada ya kupona HIV sasa ni mjamzito, namshukuru Mungu.
KAKA ALIYEKUWA ANAHITAJI KWENDA NJE SASA ANAENDA (MSANII)
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Mkuwa; mimi ni mwana muziki kwa jina la kisanii naitwa Kachumbari, nimekuja hapa kama wiki mbili zimeshapita. Nilikuwa na matatizo yangu ya kikazi, mimi ninabendi ya kwangu mwenyewe, nilikuwa nasafiri kwenda Ulaya lakini baadae nikawa sisafiri.

Lakini nimekuja kwa dada hapa nashukuru mwenyezi Mungu nikabeka CD zangu na Pasport ya kusafiria, kuja kumuomba dada aniombee niweze kusafiri au CD yangu ihiet niweze kuonekana, ili niweze kusafiri na wenzangu kwenda nje. Lakini bahati nzuru dada kaniletea mzungu tiketi hii hapa anakuja kunichukua mwezi wa 12, ninawaambia wenzangu kwamba wageuke waje kwa Mungu katika madhabahu hii ya Nabii Flora, na huyo mzungu ni mwanamke amesema ananipenda anataka niwe mume wake.

...akionyesha picha ya mke wake mtarajiwa (Mzungu) katika simu yake...

DADA ALIYEKUWA MTUKUTU AMEBADILIKA NA SASA AMEPATA KAZI NZURI
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Sayuni; mimi napenda kumshukuru Mungu kwa mambo makuu aliyonitendea katika madhabahu hii ya Nabii Flora, kwa sababu mimi binafsi familia ilikuwa hainiamini kabisa na nilikuwa sieleweki na kila nilichokuwa naongea walikuwa wananiona mimi ni muongo. Kwa sababu nimeshawahi kufanya vituko mara nyingi, walishawahi kunipeleka nikasome uwalimu nikaacha, wakanitafutia kazi kwenye mikopo nikafanya kazi mwezi mmoja nikaacha, nikapelekwa tena sehemu nyingine mbili  nikafanya muda mchache nikaacha.

Ikafikia hatua nikakopa pesa  alafu nikaandikisha vitu vya mama yangu bila yeye kujua, na kunasiku nilimpa mama yangu mirungi nikamdanganya ni dawa ya jino, lakini namshukuru Mungu wa madhabahu hii kwa kuniokoa. Nimekuja hapa kama wiki moja iliyopita nikamueleza Nabii kwamba nataka mume, kazi, pamoja na vitu vingine vingi, Nabii akaniambia niombe siku 21 nitavipata hivyo vitu. Nashukuru Mungu juzi Alhamisi nimepigiwa simu kuna barua yangu imetoka Airport inasema niende nikaanze kazi tarehe 1, kwa hiyo namshukuru Mungu sana. Na kitu kingine jana nilienda Morogoro kutoa taarifa nashukuru Mungu walini[pokea vizuri na huwa nikisafiri sina tabiaya ya kupigiwa simu, lakini sasa hivi napigiwa napendwa na wananijali, jina la Bwana lihimidiwe jamani.

MTOTO ALIYEPOTEA SASA AMEPATIKANA
Bwana Yesu asifiwe; mwanangu alikuwa amepotea lakini baada ya kuja hapa na kuombewa nilivyorudi nyumbani nikaambiwa amerudi. Nilipomuuliza alikuwa wapi akaniambia alikuwa na marafiki zake alafu wakaondoka wakaenda kwa bibi, bibi akawapa tikiti maji

.((Nabii)  huyu mama alikuwa anamkanda mume wake saa tisa usiku kuangalia mtoto hayupo wameshampora, alipokuja nilimwambia huwa sitabiri usiku lakini nitakusaidia, nikamwambia nenda Bunju ingia nyumba ya tatu, akanimbia saizi usiku sana basi nikamwambia nakutumia malaika wangu watamleta.)

BABA ALIYEPOOZA SASA AMEWEZA KUSIMAMA
Shuhuda mwingine mume wangu amepooza kwa muda wa miezi mi tatu, lakini baada ya kumleta hapa na kuombewa sasa anatembea na anaongea.
Nawaambia waumini wenzangu, Watanzania tuzidi kumuomba Mungu kuwa na imani na kila unachoomba unapata, napenda niwaambie watanzania mkija hapa kwa Nabii Flora muwe na imani na kila kitu kinatendeka.

MAMA ALIYEKUWA AMEPOOZA USO SASA AMEPONA
Bwana Yesu asifiiwe, naitwa Linda natokea Mwenge; mimi nilikuwa nimepooza uso tarehe 20 mwezi wa 3, nikawa siwezi kuongea wala kutembea.

Baada ya kuambiwa siku ya jumatano usiku saa tatu, asubuhi saa moja mimi nilikuwa hapa kwa Nabii Flora, na aliponiona tu nilipata uponyaji kama mnavyoniona sasa hivi naweza kuongea, Mungu asifiwe. Nawasihi Watanzania wenzangu na sisi tuliopo hapa mkatangaze Mungu wa Nabii Flora ni mponyaji, kwa kweli nashukuru Mungu sura yangu sasa hivi inaanza kuonekana, nilivyo jiangalia kwenye kioo sikuamini mcho yangu maana sura ilikuwa kama kinyago.
MAMA ALIYEKUWA ANATAKIWA AFANYIWE OPERATION SASA AMEPONA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Hendrew Mbena;  mimi ni mtumishi wa serikali natokea Makambako, ninamiezi mitatu nlikuwa nikimuuguza mke wangu hapa Dar es salaam. Tumehangaika sana Muhimbili lakini tulivyosikia kwamba kuna Nabii Flora kupitia yeye Mungu anafanya kazi.

Mke wangu alikuja akawa anahudhuria hapa kwa Nabii Flora kwa kweli Mungu ni wa ajabu. Tulipewa siku za matazamio ili akafanyiwe operesheni, kwenda mara ya pili Muhimbili tukakuta mafaili hayaonekani, baadae faili lilipokuja kuonekana vipimo vyote viilivyofanywa navyo vikawa havionekani. Akatakiwa kupima tena vipimo vipya, tulivyopima tena wakakuta yupo safi hakuna tatizo lolote.

MTOTO ALIYEKUWA AMEVIMBA BEGA SASA AMEPONA
Shuhuda wa pili, wakati tumeenda kupima vipimo vya pili nikasikia mwanangu nyumbani anaumwa bega, ilikuwa ni siku ya Jumatatu nikawaomba wenzangu wanipelekee hospitali, kupimwa wakasema mishipa imekaa vibaya. Kwa hiyo alitakiwa afanye mazoezi mpaka Jumamosi ya jana, basi mimi nikaona kuliko aendelee kukaa kule Hospitali, tukashauriana aje huku tuendelee kumtibu huku lakini aje kwenye maombi.

Nilivyoenda kumpokea nilitamani niupokee mzigo mimi kwa mateso aliyokuwa nayo, maana bega moja lilikuwa limepanda juu ya kichwa alikuwa kama kanjiwa.  Basi tulivyofika hapa mimi nikabaki hapo nje nikawaambia nyie ingieni, sasa kuingia hapa nashangaa hiyo saa sita na nusu mtoto anatoka mabegi aliyokuwa nayo pamoja na la mama yake yote ameyabeba, akaniambia baba nimepona. ((Nabii) tunafanya kazi kana nyati aliyejeruika, tupo kwaajili ya watu kufunguliwa).

 Wazazi wa mtoto

BINTI ALIYEKUWA NA MAPEPO SASA AMEPONA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Ennausi Asangalus natokea Mkoani Mbeya;  hapa nimeletwa na mtu aliyekuwa ananiambia twende kwa Nabii Flora, akanambia umehangaika sana umetanga tanga lakini pale utafika na utapokea muujiza wako. Huyu binti yetu ameanza kuangaika ndani ya miaka 2, tumezunguka makanisa mengi sana mpaka tukaja kufikia hapa, tumekuja siku ya Alhamisi hapa tumetokea Mtoni kwa Azizi Ali.

Tulienda kwenye maombi  kanisa la Ufufuo, Katunzi, Salu tumezunguka sana baada ya kukutana na binti mmoja akatuambia kwa Nabii Flora kuna upoinyaji  twendeni. Tukasema sawa tutaenda kwa sababu tunatafuta uponyaji, tumekuja hapa Alhamisi tukaingia ibada ya saa nne. Kwa kweli tuliingia na hali mbaya sana, toka tumeingia hapa huyu binti amezimia karibia masaa 2 au 3, tumesikiliza ibada Nabii Flora akasema mwacheni hapo hapo, anagaragara kama nyoka vile.

Baada ya hapo Nabii Flora  akamuombea na mpaka sasa hivi ni mzima, Alhamisi tukalala hapa kanisani, Ijumaa tukashinda hapa kanisani, nsa sasa ni mzima na mpaka leo hii anaendelea vizuri ni mzima atutegemeia kama pepo litamkumba tena. Tunamshukuru Mungu sana  na huyu ni mtoto wake wa kwanza.

DADA ALIYEKUWA NA VIUPELE MIGUUNI SASA AMEPONA (ANSILA)
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Ansila Hasani; Mungu amenifanyia miujiza, nimetoka Tabora miaka sita nilikuwa na alegi ya miguu, nilikuwa na vipele miguuni.

Namshukuru Mungu nimepona, nawaambia Watanazania muwe na imani mkifika hapa, pia namshukuru sana dada Tekla ndiye aliyenipeleka kwenye Kanisala la walokole  kule juu Salasala lakini mimi nikamwambia imani yangu ipo kwa Nabii Flora twende unipeleke jumapili. Jumapili iliyopita vnilikuja hapa nah ii ni jumapili ya pili, nimekuja hapa  nimepokea uponyaji wangu, nashukuru sana.

MTOTO ALIYEPATA AJALI KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA  AKAFA SASA ANAONEKANA
Bwana Yesu asifiwe; kuna mtoto wa ndugu yangu aligongwa na gari mwezi wa 11 mwaka jana akafariki, basi mdogo wangu akanipigia simu akaniambia mtoto wake amepata ajali amekufa. Siku hiyo ilikuwa siku ya jumamosi, sasa inabidi watu tunaosali hapa ukipatwa na tatizo inabidi umfahamishe Nabii. Wakati huyo mtoto anasoma alimwambia baba yake akipata division 1, 2, 3 ni ya baba lakini 4 na  0 ni ya kwake, kwa hiyo ikawa inaonyesha kwamba amekata tamaa akawa anapenda sana kuendesha magari makubwa.

Basi mimi nilipopata taarifa hiyo nikampigia Nabii simu, baada ya kumpigia Nabii simu akaniambia kwamba atanitafuta ili aweze kumuuliza Mungu wake kwamba hichi kifo ni cha ukweli au ni namna gani. Basi mimi nikatoka nyumbani nikaenda kulala kwa Nabii, nilipofika nikamwambia mimi ndo niliye kupigia simu kuwa mtoto wa mdogo wangu amekufa, akaniambia unapicha  hapo nikamwambia hapana, basi akaniambia niende nikazike alafu nirudi na picha yake nitakuja kuifanyia maombi mtoto huyo ni mzima. 
Basi nilivyorudi nikaja na picha, sasa kila nilipokuwa nahudhuria hapa Nabii alikuwa anaishika ile picha anaiyombea, siku moja jirani akanipigia simu akasema anamuona yule mtoto, sasa huyo mama akawa anamuuliza mume wake inakuwaje huyu mtoto wa watu yupo huku ndeani kwetu, yule mwanaume akawa ajali. Alivykua anaona kila siku mtoto yupo sebuleni akakimbilia huku, lakini yule mtoto akaendelea kubaki na yule baba,  sasa huyo baba akawa anajificha watu wakawa wanamtafuta haonekani, lakini sasa hivi huyo mtoto wanamuona anatokea nyumbani kwa huyu baba alafu anarudi. Na pia tuliteta mchanga wa lile kaburi alilozikwa, Nabii akaugusa sasa juzi wamepiga simu wanasema wale walioshirikiana kufanya hayo mambo wameshaanza kuchanganyikiwa sasa hivi.

DADA ALIYEKUWA NA HIV SASA AMEPONA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Mwajabu;  nilikuja kwa Nabii nikamwambia tatizo langu, nikamwambia naumwa tu ninapofika chuoni lakini sielewi tatizo ni nini.

Nabii akaniambia niende nikacheki HIV, nilicheki HIV nikakuta kweli ninayo, nikamwambia nimeipataje akaniambia kwa ndugu zako. Nyumbani walinificha lakini dakika za mwisho niligundua, waganga wa kienyeji waliniambia lakini nilikuwa siamini, walinipeleka Loliondo lakini sikufanikiwa, baada ya kuja hapa kwa Nabii alinipa siku 21. Ndani ya siku 21 nimepona.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...