Mchungaji na mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania Debora Said amekuwa
dunia tangia mwaka 1972 na mwaka huu wa 2014 Juni Mungu amemchukua kwa
mapenzi mema. Mch.Debora Said amefanya kazi yake akiwa duniani,
amewaleta watu wengi kwa Yesu kwa njia ya uimbaji na uchungaji wake,
ameisaidia familia yake mbali na huduma yake ya uimbaji na uchungaji.
Katika sherehe hii ya kumuaga Mch. Debora Said kulikuwa na waimbaji
weng0i sana, baadhi yao ni Upendo Nkone, Victor Aron, Joshua Makondeko,
Chidumule, Neema Gasper, Madam Ruti, Lungu la Yesu, Addo November,
Christina Matai, Miriam Lukindo, Chriss, Martha Mwaipaja, Kyambiki,
Petro, Apostle Gideon Mutalemwa, Upendo Kilahiro, na wengine wengi sana.
Askofu John Said mume wa marehemu Mch. Debora Said
Siku hii ilikuwa ni siku ya furaha na shangwe kwa kumuaga mtumishi wa
Mungu Debora Said, waimbaji waliweza kuimba kwa furaha na bila kuonyesha
huzuni. Lakini haikuishia hapobali watu wengine walionekana wakitoa
machozi na kulia kwa sauti, na hii inaonysha ni jinsi gani Mchungaji
Debora Said alikuwa mchango mkubwa Tanzania na Afrika nzima.
Katika sherehe hii kulihudhuriwa na wachungaji wengi sana kwaajili ya
kumuaga mpendwa wetu Mch. Debora Said. Wachungaji waliweza kutoa maneno
machache kukuhisiana na msiba huu na wengine walionekana wakishindwa
kujikaza na badala yake machozi yakiwatoka.
Rulea Sanga aliyekaa na shart nyeusi akitafakari
Tunamshukuru sana Mungu kwa kumpa ujasiri mume wake na marehemu Askofu
John Said, alionekana ni mtu mwenye ujasiri kwa sura na akiwa na
matumaini ya kwamba mke wake ametwaliwa na Mungu wetu wa mbinguni.
Kibinadamu inaumiza sana kuona yule uliyekuwa unamtegemea kimawazo
ametoweka duniani. Hakika huu ni wakati mugumu sana kwa Askofu John Said
na kanisa lake zima kwa maana wameondokewa na mtu ambaye alikuwa kama
nguzo ya kanisa.
Kwa wasiojua, ni kwamba marehemu Mchungaji Debora Saidi alikuwa ni
mwimbaji, Mchungaji na pia mwanamichezo (netball). Kutoakana na taarifa
tulizopata msibani ni kwamba alijituma sana katika ujuenzi wa kanisa lao
na pia alikuwa muhimizaji mkubwa katika swala zima la michezo.
Rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Addo November aliwaomba
waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania waache tabia ya kujiona mastaa na
kujitenga na wengine wakati wa raha na shida. Alisema anayeweza kukuweka
wewe kuonekana staa ni Yesu Kristo tu na sio mwanadamu, Mungu anaweza
kukushusha na kumuinua mtu mwingine kwa kazi yake. Pia aliwataka
wasijifananishe na watu wa Bongo Fleva kwani wao ustaa mara nyingi
wanategemea votes za mashabiki na asilimia kubwa hawategemea kutoka kwa
Yesu Kristo. Rais aliwashukuru waimbakji wote kwa usirikiano wao katika
zoezi zima la kumuaga mtumishi wa Mungu Mch. Debora Saidi.
Mch mama Fednandes wa kanisa la AGAPE alitoa ofa ya kurusha matukio ya
msiba huu wote katika kipindi cha FIRE katika television cha ATN na pia
ameandaa tamasha kubwa la waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania hapo
kanisani kwake.
KIPINDI CHA KUPELEKA MWILI WA MAREHEMU MCH. DEBORA SAID KANISANI
Wa pili kutoka kushoto ni Askofu John Said mume wa Marehemu Mch. Debora Said akijianda kuingia Kanisani
WAIMBAJI WAKISHREKEA SIKU YA PEKEE YA KUMUAGA MWIMBAJI MWEZAO MCH. DEBORA SAID
Tumaini Njole akimsindikiza rafiki yake Mch. Debora Saidi
Edson Mwasabwite akisema bye bye Debora Said huku akiimba wimbo wa Ni kwa Neema tu
MC Joshua Makondeko
Kwaya ya kanisa la Maisha ya Ushindi kwa Askofu John Said
Waimbaji kutoka Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) wakiimba
wimbo maalum wa kumuaga mpendwa wao marehemu Debora Saidi
Edson Mwasabwite
Neema Gasper (aliyeshika mic)
Apostle Gideon Mutalemwa
Christina Matai hakuweza kujizuia, alijishtukia analia wakati waimbaji
wenzake wakiimba. Hii inaonyesha ni jinsi gani alipigwa na kifo cha
marehemu Mch. Debora Said
Sifa John
Kutoka kulia ni Victor Aron
Upendo Nkone
Lungu la Yesu
Mchunga Anton Lusekelo (Mzee wa Upako)
Mchungaji Anton Lusekelo "Mzee wa Upako" (aliyekaa)
Mwimbaji wa nyimbo za injili Petro aliyevalia koti la draft
wa kwanza kutoka kwenye nguzo ya kanisa ni mume wa Upendo Kilahiro
wa pili kutoka kushoto mstari wa kwanza ni mwimbaji Orida Njole
Mume wa Martha Mwaipaja (kulia) akiwa na mke wa Mtume Fidnandes wa ATN
Mchungaji Harisi Kapiga
MATUKIO MBALIMBALI YAKIENDELEA NJE YA KANISA WAKATI SHEREHE IKIENDELEA KANISANI
Victor Aron (mwenye tshirt nyeusi akiwa na baadhi ya marafiki wakibadilishana mawazo
Baadhi ya waimbaji walioamua kupiga picha ya kumbukumbu
MC Joshua Makondeko mwenye kitamba cha bendera ya taifa akiwaelekeza wenzake ratiba ya waimbaji
Miriam Lukindo (kushoto.gauni nyeusi) na kulia ni Tumaini Njole
Mwimbaji wa Gospel Tanzania Furaha Isaya (kulia)
Gideon Mutalemwa akichukua namba za simu kutoka kwa mtumishi wa Mungu Datson
Sarah Mvungi akifanya mawasilia
KIPINDI CHA KUOMBEA CHAKULA
Upendo Kilahiro (wa pili kutoka kulia) akiongea na rafiki yake
KIPINDI CHA KUTAMBULISHA WACHUNGAJI NA WAGENI MBALIMBALI
Wachungaji, mitume na viongozi mbalimbali (waliosimama)
Waliosimama ni wake wa wachungaji
"Nyamayao" wa tatu kutoka kushoto
Bloga na mtangazaji wa WAPO REDIO Silas Mbise akifanya kazi ya Mungu
Mchungaji Mama Finandesi wa ATN akisema jambo
Askofu John Said akiwa na mwanae
Rais wa Chama Cha Muziki Tanzania (CHAMUITA) Addo November akiwashukuru
waimbaji kwa kujitolea kufika katika msiba huu. Pia aliweza kusema
waimbaji waache kujiita mastaa kwa anayekupa ustaa ni Yesu Kristo na sio
mtu mwingine. Leo unaweza kuonekana unang'aa lakini kesho Mungu
akamuinua mtu mwingine.
ASKOFU JOHN SAID AKIWA AMEMKARIBISHA MAMA HUYU KUSEMA JAMBO KUHUSIANA NA KIFO CHA MKE WAKE
Mama huyu alionekana kulia wakati wote hata ulipofika wakati wa kula
chakula bado alionekana kulia huku akila chakula. Mama huyu alishikwa na
uchungu mkubwa kwa kutwaliwa kwa marehemu Debora Said
Kulia ni Askofu John Said
Askofu John Said
KIPINDI CHA KUOMBEA WATU WALIOWEZA KUOKOKA SIKU YA MAZISHI YA MCH. DEBORA SAID