Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Ijumaa, 27 Juni 2014

MSANII WA BONGO FLEVA NA BONGO MOVIE BABY MADAHA AMGEUKIA MWENYEZI MUNGU

Kufuatia vifo vya wasanii vilivyotokea mfululizo, mwigizaji Baby Joseph Madaha amelazimika kubadili mtindo wake wa maisha na kuishi kitakatifu.
Baby Joseph Madaha

Akipiga stori na wana habari, Baby Madaha alisema anawasihi hata wasanii wenzake wabadili mfumo wa maisha kwa kumgeukia Mungu na kufanya ibada kila mara kwa kuwa vifo hivyo vinawapa somo la kuwakumbusha kumkaribia Mungu.

“Nimebadili mfumo wa maisha kwa kufanya ibada na ninawashauri wasanii wenzangu tumgeukie Mungu kwani vifo na mambo yanayotokea yanatukumbusha ibada na kujiweka safi,” alisema Baby Madaha.

MUNGU awasaidie hawa wanaojiona kuwa ni watu maarufu maana umaarufu wao ni hapa hapa duniani, mbinguni hakuna anaowajua. Wanazidiwa umaarufu na watoto wadogo ila tu wanaisha maisha ya kumpendeza MUNGU huku wamempa BWANA YESU maisha yao.

Sio mpaka matatizo yaje ndio tumkumbuke MUNGU lakini wakati wa amani tunamsahau MUNGU kama yupo.

WOKOVU NI SASA NA KAMA SIO SASA BASI NI SASA HIVI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...