Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Jumatatu, 4 Agosti 2014

JIUNGE NA CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI TANZANIA KWA KUTIMIZA VIGEZO VIFUATAVYO


MASHOGA NA WASAGAJI KUTOKA KENYA NA UGANDA KUFANYA MKUTANO SERENA HOTEL JIJINI DAR

Kama Mtanzania una haki ya kusema na kutoa maono yako juu ya tabia hii ya usagaji na ushoga. Katika vitabu vitakatifu tabi hii imekatazwa na imeonekana ni dhambi kama mwanadamu mwenye akili sawa na asiye na akili sawa anafanya vitendo hivi.

Inasahangaza sana kuona mataifa makubwa na yaliyoelimika na kuwa na maprofesa inaunga mkono vitendo hivi vichafu. Binafsi kutokana na iamani yangu na maadili ya dini yangu ya KIKRISTO ninapiga tabia hii na kama kuna watu wanaunga mkono basi hao ni wao wanahitaji kuombewa ili siku ya mwisho tukamuone Mungu wetu.

Kama Taifa tunawajibika sana katika kuliombea Taifa letu kupingana na hii tabia ya ushoga na usagaji. Hata kama kuna mataifa yanatetea lakini tunatakiwa kusimama na kuwasaidia hawa ndugu zetu wanaoteseka na hili pepo la uzinsi. Inaumiza sana unapoona mwanaume mwenzako anamfanyia mwanaume mwenzake, hii ni aibu sana watu wa Mungu. Umefika wakati wa kufumbua macho yetu na kuwajibika katika kupiana vita na hii tabia isionekane ikitokea nchini kwetu na dunia nzima.

Wenu katika Bwana
Rulea Sanga
RUMAFRICA FOR ALL NATIONS

SOMA HABARI KUTOKA KATIKA MITANDAO MINGINE JUU YA HUU MKASA

MASHOGA kutoka nchi tatu za Afrika Mashariki wamekutana kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.

Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam, zinasema mashoga hao walikutana juzi katika Ukumbi wa Kivukoni 3 ulioko katika Hoteli ya Serena na kuwashirikisha wasichana wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mashoga hao wapatao 50 walitoka katika nchi za Kenya na Uganda na waliungana na wenzao wa Tanzania.


Katika kuhakikisha malengo ya mkutano huo hayatambuliki, katika ubao wa matangazo wa hoteli hiyo waliutambulisha kama ulikuwa ni mkutano wa kujadili masuala ya kimataifa ya afya ulioitwa International Health (SA).

Mwandishi wetu aliyepata taarifa za uwepo wa mkutano huo, alishuhudia jinsi mkutano huo ulivyokuwa ukiendeshwa kwa usiri wa hali ya juu kwa kuwa kila aliyekuwa akitaka kuingia ukumbini alikuwa akizuiwa.

Pamoja na watu wasiohusika kutotakiwa kuingia ukumbini, hata wahudumu wa hoteli hiyo walikuwa wakiruhusiwa kuingia ukumbini kwa tahadhari ili wasijue kinachoendelea.

Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa, mashoga hao walikuwa wakisitisha mjadala kila wahudumu walipokuwa wakiingia ukumbini kwa ajili ya kutoa huduma na mazungumzo yalikuwa yakiendelea baada ya wahudumu kutoka ukumbini.

Pamoja na ulinzi uliokuwa mahali hapo, taarifa zilisema mada kuu iliyowakutanisha mashoga hao ilikuwa ni kujadili changamoto zinazowakabili katika utendaji wao wa kazi. Pia taarifa zinasema walikuwa wakijadili namna ya kufanya utafiti wa kukabiliana na changamoto hizo.

Pamoja na mashoga hao kuonyesha walikuwa wakijadili masuala ya afya ya kimataifa, Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja, alisema wizara hiyo haikuwa na taarifa za mkutano huo.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania ushoga hauruhusiwi lakini wiki iliyopita Mahakama ya Kikatiba nchini Uganda ilifutilia mbali sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, ambayo ilisababisha mataifa kadhaa ya magharibi kuinyima misaada.

Sheria hiyo ilizua mjadala si tu nchini Uganda bali kote duniani kiasi cha kuyafanya mataifa ya magharibi yalazimike kuingilia kati.

Mahakama ilisema muswada uliopitishwa kabla ya kuidhinishwa na rais kuwa sheria, ulipitishwa na wabunge ambao idadi yao haikutosha kuupitisha na kwa hivyo ulikuwa kinyume na sheria.

Sheria hiyo iliharamisha hatua zozote za kueneza au kushawishi mapenzi ya jinsia moja na wakati huo huo ikiwajumuisha wanawake wasagaji katika kundi hilo.

Wabunge nchini Uganda huenda wakalirudisha upya bungeni suala hilo, mchakato unaotarajia kuwa mrefu ukizingatia sheria ya sasa ilichukua miaka minne hadi kupitishwa.

Source: Vituko vya Mtaa
You might also like:

GLORIOUS WORSHIP TEAM WAJA NA NEW LOOK YA COVER LAO LA ALBAMU YA WAWEZA - BADO LIKO JIKONI LINAKARABATIWA

Safari moja huanzisha safari nyingine. Hawa vijana wa Yesu wametoka mbali sana kihuduma. Kazi yao imewagusa walio wengi sana Tanzania na nje ya Tanzania, kinachoshangaza sana ni vijana bado lakini wanafanya mambo makubwa wakishirikiana kama siafu. Inapendeza sana kuona vijana wanafanya kazi ya Mungu. Sio kazi rahisi kwa maisha ya sasa kuona watu wanakaa pamoja na kuacha kazi zao na kuamua kufanya kazi ya pamoja kama hii tunayoona kwa vijana hawa wa GWT



Ukiwakuta hawa vijana wanavyoishi ni kama mtu na dada yake , ni vijana wanaopenda sana kutaniana na pia kufanya kazi kwa pamoja. Mungu wetu na azidi kuwatumia hawa vijana ili wasonge mbele kwa kazi ya Mungu.

Huu ndio muonekano wa kava jipya la albamu ya WAWEZA. Rumafrica katika pitapita mindaoni ilikuta kuna stori kuwa kava hili bado halijakamilika, bado liko jioni linafanyiwa utundu ili lionekane bora zaidi, kwahiyo hata aliyeweza kurirusha mitandaoni amefanya makosa. Tuzidi kusubiri muonekano mzuri wakava hili hapo baadae

KANISA LA UFUFUO LATOA SHUKRANI YA KUPATA HELKOPTA

WAUMINI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima leo wamefanya ibada ya shukrani kwa kupata helikopta.

Kanisa hilo lililopo maeneo ya Kawe jijini Dar limetoa shukrani zake za dhati kwa Mwenyezi Mungu kuwawezesha kumiliki helikopta hiyo ambayo itatumika zaidi kutoa huduma sehemu mbalimbali za Tanzania na duniani kote.

Helkopta hiyo inakadiriwa kugharimu shilingi bilioni 7.5.

Misa hiyo iliyoanza majira ya asubuhi mpaka jioni ilifanyika kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers ambapo ilihudhuriwa na waimba injili maarufu nchini wakiwemo; Rose Mhando, Upendo Nkone, Christina Shusho, Flora Mbasha, John Lissu, Boniface Mwaitege, Munishi na wengineo.


Christina Shusho na Flora Mbasha wakiimba sambamba na waumini wengine waliohudhuria misa hiyo.



Flora Mbasha akiimba katika kanisa la Gwajima.



Halima Mdee akisisitiza jambo alipokuwa akiwahutubia waumini wa kanisa hilo.


Mchungaji Gwajima akicheza kwa shangwe.


Rose Mhando akicheza kwa hisia na shangwe kubwa.


Umati wa watu waliohudhuria misa hiyo wakifuatilia kwa makini.


Upendo Nkone akiimba kwa hisia kali.


Gwajima (kushoto) akicheza pamoja na Christina (Kulia)
.
You might also like:

WAUMINI MORAVIAN KIZIMBANI TENA

KESI inayowakabili waumini 29 wa Kanisa la Moravian lililopo Mwananyamala-Msisiri ” A”, Dar leo imesikilizwa tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni chini ya hakimu mwandamizi wa mahakama hiyo, Boniphace Lihamwike.
Waumini hao wanatuhumiwa kufanya fujo hadharani katika Kanisa la Moravian lililopo Mwananyamala-Msisiri ” A” Wilaya ya Kionondoni, Julai 20 mwaka huu na kuzua mzozo uliosababisha waumini kupigana na kusababisha askari polisi kutumia nguvu kutuliza fujo hizo ikiwa ni pamoja na kutumia mabomu ya machozi.
Kesi hiyo imeahirishwa kutokana na baadhi ya watuhumiwa kutokuwepo hadi Septemba 4 mwaka huu itakaposikilkizwa katika mahakama hiyo.

Watuhumiwa wakienda kusomewa mashitaka.

Akina mama ambao ni waumini wa Kanisa la Moravian wakificha sura zao wakati wakitoka mahakamani.

TAMASHA LA UZINDUZI WA ALBAMU YA ROSE MUHANDO YA "PINDO LA YESU " YAFANA DIAMOND JUBILEE DAR


MWANAMUZIKI, Rose Mhando jana amefanya kweli kwa kuwapa mashabiki wa nyimbo za Injili utamu wa Yesu alipozindua albamu ya Pindo la Yesu katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Mstaafu,


Frederick Sumaye na wasanii mbalimbali akiwemo Sarah K kutoka Kenya, Ephraim kutoka Malawi, na wale wa hapa nchini wakiwemo Upendo Nkone, Emmanuel Mbasha, Upendo Kilaeni na wengine.

Katika hafla hiyo Sumaye alitoa ujumbe wa kuitaka Tume ya Uchaguzi ya Taifa na Watanzania kuwa makini ili kuwepo uchaguzi wa haki katika uchaguzi mkuu mwaka kesho.


Rose Mhando akicheka wakati wa uzinduzi wa albamu yake. Nyuma ni waimbaji wake.

Mchungaji Maboya akitoa neno katika uzinduzi huo.

Watu waliofurika katika tukio hilo.

Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye (kushoto) akizindua albamu hiyo, pembeni ni Promota wa Muziki wa Injili, Alex Msama.

Mwimbaji Sarah K (kushoto) wa Kenya akiwa na Upendo Nkone.

Emmanuel Mbasha (wa pili kushoto) Upendo Kilaheni pamoja na wadau wengine wakiwa katika pozi.

Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akiwa ameshika album ya ‘Pindo la Yesu’.

Waumini na mashabiki wa Rose Mhando wakipiga makofi.

Sumaye akiwa na Alex Msama (katikati) na Rose Muhando.

Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye na mkewe wakifuatilia uzinduzi huo.

Mwandishi wa mtandao huu, Gabriel Ng'osha, na Sarah K.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...