Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Jumatatu, 4 Agosti 2014

WAUMINI MORAVIAN KIZIMBANI TENA

KESI inayowakabili waumini 29 wa Kanisa la Moravian lililopo Mwananyamala-Msisiri ” A”, Dar leo imesikilizwa tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni chini ya hakimu mwandamizi wa mahakama hiyo, Boniphace Lihamwike.
Waumini hao wanatuhumiwa kufanya fujo hadharani katika Kanisa la Moravian lililopo Mwananyamala-Msisiri ” A” Wilaya ya Kionondoni, Julai 20 mwaka huu na kuzua mzozo uliosababisha waumini kupigana na kusababisha askari polisi kutumia nguvu kutuliza fujo hizo ikiwa ni pamoja na kutumia mabomu ya machozi.
Kesi hiyo imeahirishwa kutokana na baadhi ya watuhumiwa kutokuwepo hadi Septemba 4 mwaka huu itakaposikilkizwa katika mahakama hiyo.

Watuhumiwa wakienda kusomewa mashitaka.

Akina mama ambao ni waumini wa Kanisa la Moravian wakificha sura zao wakati wakitoka mahakamani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...