Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Jumatatu, 4 Agosti 2014

MASHOGA NA WASAGAJI KUTOKA KENYA NA UGANDA KUFANYA MKUTANO SERENA HOTEL JIJINI DAR

Kama Mtanzania una haki ya kusema na kutoa maono yako juu ya tabia hii ya usagaji na ushoga. Katika vitabu vitakatifu tabi hii imekatazwa na imeonekana ni dhambi kama mwanadamu mwenye akili sawa na asiye na akili sawa anafanya vitendo hivi.

Inasahangaza sana kuona mataifa makubwa na yaliyoelimika na kuwa na maprofesa inaunga mkono vitendo hivi vichafu. Binafsi kutokana na iamani yangu na maadili ya dini yangu ya KIKRISTO ninapiga tabia hii na kama kuna watu wanaunga mkono basi hao ni wao wanahitaji kuombewa ili siku ya mwisho tukamuone Mungu wetu.

Kama Taifa tunawajibika sana katika kuliombea Taifa letu kupingana na hii tabia ya ushoga na usagaji. Hata kama kuna mataifa yanatetea lakini tunatakiwa kusimama na kuwasaidia hawa ndugu zetu wanaoteseka na hili pepo la uzinsi. Inaumiza sana unapoona mwanaume mwenzako anamfanyia mwanaume mwenzake, hii ni aibu sana watu wa Mungu. Umefika wakati wa kufumbua macho yetu na kuwajibika katika kupiana vita na hii tabia isionekane ikitokea nchini kwetu na dunia nzima.

Wenu katika Bwana
Rulea Sanga
RUMAFRICA FOR ALL NATIONS

SOMA HABARI KUTOKA KATIKA MITANDAO MINGINE JUU YA HUU MKASA

MASHOGA kutoka nchi tatu za Afrika Mashariki wamekutana kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.

Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam, zinasema mashoga hao walikutana juzi katika Ukumbi wa Kivukoni 3 ulioko katika Hoteli ya Serena na kuwashirikisha wasichana wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mashoga hao wapatao 50 walitoka katika nchi za Kenya na Uganda na waliungana na wenzao wa Tanzania.


Katika kuhakikisha malengo ya mkutano huo hayatambuliki, katika ubao wa matangazo wa hoteli hiyo waliutambulisha kama ulikuwa ni mkutano wa kujadili masuala ya kimataifa ya afya ulioitwa International Health (SA).

Mwandishi wetu aliyepata taarifa za uwepo wa mkutano huo, alishuhudia jinsi mkutano huo ulivyokuwa ukiendeshwa kwa usiri wa hali ya juu kwa kuwa kila aliyekuwa akitaka kuingia ukumbini alikuwa akizuiwa.

Pamoja na watu wasiohusika kutotakiwa kuingia ukumbini, hata wahudumu wa hoteli hiyo walikuwa wakiruhusiwa kuingia ukumbini kwa tahadhari ili wasijue kinachoendelea.

Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa, mashoga hao walikuwa wakisitisha mjadala kila wahudumu walipokuwa wakiingia ukumbini kwa ajili ya kutoa huduma na mazungumzo yalikuwa yakiendelea baada ya wahudumu kutoka ukumbini.

Pamoja na ulinzi uliokuwa mahali hapo, taarifa zilisema mada kuu iliyowakutanisha mashoga hao ilikuwa ni kujadili changamoto zinazowakabili katika utendaji wao wa kazi. Pia taarifa zinasema walikuwa wakijadili namna ya kufanya utafiti wa kukabiliana na changamoto hizo.

Pamoja na mashoga hao kuonyesha walikuwa wakijadili masuala ya afya ya kimataifa, Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja, alisema wizara hiyo haikuwa na taarifa za mkutano huo.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania ushoga hauruhusiwi lakini wiki iliyopita Mahakama ya Kikatiba nchini Uganda ilifutilia mbali sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, ambayo ilisababisha mataifa kadhaa ya magharibi kuinyima misaada.

Sheria hiyo ilizua mjadala si tu nchini Uganda bali kote duniani kiasi cha kuyafanya mataifa ya magharibi yalazimike kuingilia kati.

Mahakama ilisema muswada uliopitishwa kabla ya kuidhinishwa na rais kuwa sheria, ulipitishwa na wabunge ambao idadi yao haikutosha kuupitisha na kwa hivyo ulikuwa kinyume na sheria.

Sheria hiyo iliharamisha hatua zozote za kueneza au kushawishi mapenzi ya jinsia moja na wakati huo huo ikiwajumuisha wanawake wasagaji katika kundi hilo.

Wabunge nchini Uganda huenda wakalirudisha upya bungeni suala hilo, mchakato unaotarajia kuwa mrefu ukizingatia sheria ya sasa ilichukua miaka minne hadi kupitishwa.

Source: Vituko vya Mtaa
You might also like:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...