Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Jumamosi, 12 Julai 2014

MKURUGENZI WA RUMAFRICA RULEA SANGA AMEFIWA NA SHEMEJI YAKE MBEYA USIKU

Rulea Sanga ambaye ni mkurugenzi wa blogu hii siku ya jana akiwa na masikitiko makubwa sana baada ya kupata taarifa kutoka kwa mtoto wa kaka yake, Furaha Sanga usiku wa kuamkia  jumamosi 12/07/2014 ya kwamba shemeji yake aliyekuwa akimuuguza Muhimbili amefariki dunia.

Rulea Sanga baada ya kupata habari za kifo cha shemeji yake nyumbani kwake Sinza

Mgonjwa huyo ameugua kwa muda mrefu kidogo kwa ugonjwa wa kansa ya mifupa na koo. Ugonjwa huu ulimtesa sana na mpaka ikalazimika kumleta Muhimbili Dar es Salaam. Hali ake ilizidu kuwa mbaya kila kuitwapo leo, na mwisho wa siku madaktari wakaamua kumruhusu aende nyumbani kwani ilionekana ni ngumu sana kumtibu.

Wanafamilia walilzimika kumsafirisha mgonjwa mpaka mkoani Mbeya ambako ni nyumbani wa marehemu. Na leo hii amefariki dunia.

KNOW MORE ABOUT BISHOP JANE K. MUHEGI: FACTORS THAT LED PASTOR JANE MUHEGI INTRODUCE THE DORCUS CHRISTIAN MINISTRIES AND UKUVYU ORGANIZATIONS

Bishop Jane Muhegi. Formerly used to be a teacher. She had a tender heart for the children and youth who no absolute other wise other than to steel and do other immoral conducts which caused the community alert to safe guard themselves from the wrath of such I was blessed to find favor from God and be friend to them.

One day she was bewildered to witness a young man being burnt to death. In spite of her efforts to rescue the boy, she could not help the situation. This moved her spirit and began to find the best ways to help the youth from the destruction.

To manifest God's Love to the disabled, aged, HIV AIDS Victims and widow
Manifest God's love to the misfortune, the needy, the disabled was her objectives number two. We are preaching the word of God and rehabilitating the aged, the homeless and the poor, where we provide them food, clothes and shelter also providing counseling center for AIDS Victims as part of dorcus forums to fight HIV AIDS and its transmission – Bishop Jane!

More about Dorcus Christian Ministries:
P.O. Box 13504 | Tel: +255-22-2650378
Kunduchi Beach - Bahari Beach Road | Dar es Salaam - Tanzania

Healing hour with Bishop Jane Muhegi at Dorcus Christian Ministries

John Shabani giving thanksgiving offering in church at Dorcus Christian Ministries

Dorcus Christian Ministries center



MATUKIO KATIKA PICHA:WINGU JEUSI LATANDA MSIBA WA SISTA ANNA, DAYOSISI YA KUSINI

Msiba wa sista Anna Peterson umeibua simanzi si kwa familia yake tu bali kwa wananchi wa wilaya ya Makete mkoani Njombe alipokuwa akifanya kazi za kijamii tangu ujana wake.

Hayo yamebainika wakati wa ibaada maalum ya kumkumbuka iliyofanyika hii leo katika kanisa la KKKT usharika wa Amani Bulongwa, ibaada iliyoongozwa na baba askofu wa dayosisi ya kusini kati Levis Sanga, Askofu Mstaafu Dkt. Solomon Swallo na Askofu Mstaafu Shadrack Manyiewa pamoja na msaidizi wa askofu Philemon kahuka.


Sista Anna Enzi za uhai wake.

Akihubiri katika ibaada hiyo maalum Askofu Mstaafu Shadrack Manyiewa amesema marehemu alikuwa akifanya kazi zake kwa mkono wa dayosisi ya kusini kati tangu enzi za ujana wake bila ubaguzi ingawa yeye alikuwa mzaliwa wa nchi ya Sweeden.

Amesema amemfahamu toka 1969 na hadi anafikwa na umauti alikuwa akisaidia watoto yatima, wajane, wagane na walemavu wote na hata wasiojiweza na kusisitiza kuwa kanisa haliwezi kumsahau kamwe.

Akielezea historia ya marehemu Askofu mstaafu Dkt Solomon Swallo amesema Sista Anna alikuwa akifanya kazi zake kwa kujituma bila kujali ugumu wa kazi uliokuwepo kwa kipindi hicho hasa ubovu wa barabara na ugumu wa kuwafikia wananchi kutokana na tabu ya usafiri.

Askofu mstaafu Manyiewa akihubiri ibadani hapo.

Dkt Swallo amesema alikuwa akisisitiza kuwa Mungu ndiye aliyemtuma kufanya kazi Bulongwa Makete na si Binadamu hivyo haoni shida kutumikia jamii ya Makete toka ujana hadi uzee wake.

Askofu mstaafu Dkt Solomon Swallo.


Dkt Nicodemas Kikoti.

Kwa upande wake Kaimu Mganga mkuu hospitali ya Bulongwa Dkt Nicodemas Kikoti amesema marehemu pia alikuwa akifanya kazi na hospitali hiyo pamoja na jamii ikiwemo kusomesha watoto yatima kutoka shule ya awali mpaka vyuo, kuwajengea nyumba wasiojiweza, kuhudumia wajane, kusaidia vifaa vya umeme pamoja na kujenga makao ya kituo cha watoto yatima Bulongwa.


Mch. Dkt Phares Ilomo.

Naye Mch. Dkt Phares Ilomo kutoka chuo Kikuu cha Iringa amesema yupo tayari kuandika kitabu cha kuelezea historia ya marehemu Sista Anna kwa kushirikiana na viongozi wengine wa kanisa na washarika kuchangia gharama ili kitabu hicho kichapishwe na kuzalishwa kwa faida ya vizazi vijavyo ikiwemo kukiweka katika maktaba ya chuo chake.

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira Dkt Binilith Mahenge ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Makete akitoa salamu za rambirambi amesema marehemu alikuwa akifanya shughuli ambazo kimsingi zilitakiwa kufanywa na serikali hivyo wema wake kwa jamii ya Makete hauna mfano.


Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira Dkt Binilith Mahenge ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Makete akitoa salamu za rambirambi.

Amesema njia pekee ya kumuenzi ni kufanya yale aliyoyapenda huku akisisitiza kuwa serikali itashirikiana na kanisa kuendeleza kazi zote alizoziacha Sista Anna.


Askofu wa dayosisi ya kusiki kati Levis Sanga.

Askofu wa dayosisi ya kusiki kati Levis Sanga ametangaza tarehe 26 Juni kila mwaka kuwa ni siku maalum kikanisa ya kumkumbuka marehemu sista Anna hivyo jamii inashauriwa kufika kwenye kituo cha watoto yatima Bulongwa kwa ajili ya kuwatembelea na siku hiyo itakuwa ikifanyika ibaada maalum kwa ajili ya marehemu.

Sista Anna Peterson amefariki Juni 26 mwaka huu nchini Sweeden alipokwenda kwa ajili ya matibabu na amezikwa leo hii nchini humo, na hapa Makete alikokuwa akiishi toka ujana wake imefanyika ibaada maalumu ya kumkumbuka.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Sista Anna Peterson, Amen.

Habari/Picha Na Edwin Moshi, Makete

JAMANI TUMUOMBEE NDUGU YETU ORIDA NJOLE

Kwa wale wasiomjua Oride Njole, ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania. Leo hii yuko kitandani anaumwa, anatamani kuwa kama wewe ambaye kwa sasa unacheka na kufurahi lakini anashindwa kutokana na ugonjwa alionao. Jamani ndugu yetu anaumwa sana tunapaswa kumuombea na ikiwezekana tufike pale hospitalini Temeke hospitali ya serikali.


Orida Njole

RUMAFRICA YAPATA TAARIFA ZA UGONJWA

Rumafrica imepokea habari hizi siku ya leo kwa njia ya simu kutoka kwa mtangazaji wa Radio Tumaini Obedi Kikao, anasema hali yake sio nzuri sana, ndugu yetu anateseka sana. Kama binadamu mwenye huruma basi fika pale hospitalini kumpa pole ndugu yetu huyu. Kumbuka ulikuwa naye kipindi mnacheka leo hii mwenzetu amenuna kutoka na maumivu anayopata. Anahitaji faraja kutoka kwako Mtanzania.



NDUGU NA MARAIKI
Kumbuka wewe rafiki uliyekuwa unacheza naye mpira wa mikono, Oride ni mwanamichezo mkubwa sana na amekuwa nawe katika michezo mbalimbali, lakini leo hii anashindwa hata kushika mpira kutoka na ugonjwa alionao. Umefika wakati wa kwenda kumuona ndugu yetu na kubwa zaidi ni maombezi.


WACHUNGAJI NA WATUMISHI WA MUNGU

Mchungaji ambaye ulikuwa ukimtumia Oride Njole katika huduma yako, ameimba sana kanisani kwako lakini leo hawezi kuimba tena kutoka na kile kinachomsumbua. Nenda basi ukamuombee pale kitandani alipolala ili aweze kuamka na kufanya kazi ya Mungu kama zamani. Kuwa na moyo wa huruma basi.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiOwQlqihwXMe7mtHGAYjwMIxXNXaKa3ylVTXlyMU_b064YZ6CWsOBNnL_JVRk_qhCTxE4YZseoSeqx9QRhaoiM3P0Q0O9fXbtnJ3PF0kgGrqhmsEv0AoUndF4TymZQ0A6YRVDlhgMNjII/s640/orida6.jpg
Orida Njole akimtumika Mungu kanisani

Hata wewe mchungaji ambaye unayemfajhamu na wewe uliyemfahamu kwa kupitia blogu hii ya Rumafrica basi acha hicho unachofanya sasa anza kumuombea. Ondoa hiyo roho inayokusukuma usimmuombee na ikemee sasa.

WANAMICHEZO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgtSKeClRxnGGLHMRIm0KLRhFAsa3O1rWw2qG4fc7DNTbseXoRJJudINkaER5Gp-vxrYKiFrIUgG_VXWstq6aOSgmdCxUys2XP7ajybraUCcvGSq2_5DSx9XPmkm-iUj6TD8i4YsyABHbo/s640/DSCN7837.JPG
Orida Njole (kushoto)

Marafiki zake ambao mmekuwa naye studi kurekodi nyimbo za kumtukuza Mungu, sasa tunawaomba mfanye maombi na kufika pale hospitalini kumtia moyo na kumpa pole. Mmekuwa mkicheka na kupeana mawazo studio lakini leo hii mwenzenu anashindwa hata kuwapa mawazo kutokana na maumivu anayopata. Kuwa na moyo wa upendo na huruma kama vile mnavyotuimbia sisi tuyafanye yale manyoimba.
http://photos-a.ak.fbcdn.net/hphotos-ak-ash3/t1.0-0/c0.2.960.639/s720x720/379618_192151074260838_1925803444_n.jpg
Orida Njole kushoto wa kwanza
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjW-n0ja52JJmz4DHQzOMdonN3qU6qULdyiNcyhieky96DWpV2mAPzeokGULBpJSFNYTJN_ypZ7rwcvNWNqlqm8fLA2pvo-mIf57eTRjb9ahug9RpmGTATPQL06l3v-5lRtLP89n8XPFox3/s640/Orida-Njole-Poster.jpg
DVD Cover la albamu ya Orida Njole

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEihY5UGc2CuKXDwnICXieiqP7SFgrIPC0qKrsQn9yPzSl7Ohu8v4PKy-xS3-C18TLftqdmJoxhlin-hdlMiX624nluK3nZbNxOPsgdZSNNHMjuOC3B2wtNTdBQe2g8ry_PsRJl7WXLMfBpc/s640/Orida.jpg
Orida Njole

MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA JUBILEI YA MIAKA 75 YA TAG TANZANIA YALETA NEEMA MKOA WA MBEYA.

KANISA la Tanzania Assemblies of God (TAG) nchini linaadhimisha sherehe za miaka 75 tangu kuzaliwa kwake zinazofanyika kitaifa Mkoani Mbeya.

Kutokana na maadhimisho hayo Jiji na Mkoa wa Mbeya utanufaika na sherehe hizo kutokana na shughuli ambazo Kanisa hilo litafanya katika siku zote za maadhimisho hayo.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Askofu Mkuu wa TAG nchini, Dk. Barnabas Mtokambali, katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa MMRP jijini hapa, alisema Sherehe hizo zitaambatana na shughuli mbali mbali.

Askofu Mkuu wa TAG nchini, Dk. Barnabas Mtokambali, akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa MMRP jijini hapa.

Alisema maadhimisho hayo yatafikia kilele Julai 13, Mwaka huu katika sherehe zitakazofanyika katika viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Dk. Jakaya Kikwete Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Askofu alisema kabla ya sherehe hizo kutakuwa na zoezi la kugawa vyandarua 8550 vyenye thamani ya shilingi 270 kwa ajili ya Hospital,Vituo vya Afya pamoja na zahanati zinazo laza wagonjwa katika Mikoa ya Mbeya, Rukwa na Njombe.

Askofu Mtokambali alisema mbali na kanisa kutoa msaada wa Kiroho kwa waumini wake lakini limeona katika kushurehekea miaka 75 ya tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo hapa nchini ni bora wakafanya na huduma za kijamii.

Askofu Mtokambali alisema vyandarua vitagawiwa katika Hospitali 34 na vituo vya afya 83 katika mikoa ya Mbeya, Njombe na Rukwa zoezi litakalofanyika kuanzia Julai 1 hadi julai 4, Mwaka huu.

Alisema katika mgawanyo huo vyandarua 1300 vitaenda Mkoani Rukwa katika Hospitali 3 na vituo vya afya 22, Mkoa wa Njombe vyandarua 3100 kwa ajili ya Hospitali 11 na vituo vya afya 25.

Askofu alisema Vyandarua 4150 vitabaki Mkoa wa Mbeya katika Hospitali 20 na vituo vya afya 36 ambapo kati yake Vyandarua 500 vitabaki katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na Vyandarua 150 vitakua kwa ajili ya Hospitali ya Wazazi ya Meta.

Mbali na msaada wa vyandarua Askofu Mtokambali alisema pia kanisa hilo litaendesha zoezi la uchangaji damu litakalowagusa Wachungaji zaidi ya 800 hivyo kupunguza upungufu wa damu unaokikabili kituo cha damu salama Kanda ya Mbeya.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Husein Kandoro, alipokea vyandarua 650 kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mbeya ambapo kati yake vyandarua 150 vitagawiwa katika Hospitali ya Wazazi ya Meta.


Mkuu wa mkoa Mbeya Abasi Husein Kandoro, alipokea vyandarua 650 toka kwa Askofu mkuu wa TAG nchini, Dk. Barnabas Mtokambali,

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abasi Husein Kandoro akishukuru msaada huo kwaniaba ya Hospitali ya rufaa




Dr. Leonard Maboko Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ya TAG ambae pia ni Mkurugenzi wa NIMR, akitoa neno kwa wageni

Kaimu mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Dr. Kaimu Mku Humphrey Kihwelu akimkaribisha mkuu wa mkoa Mbeya









Ijumaa, 4 Julai 2014

MINYORORO MIGUUNI WAKATI WA KUJIFUNGUA YASABABISHA ULEMAVU KWA MWANANGU - MWANAMKE SUDAN


Meriam akiwa na watoto wake.

Mwanamke aliyekuwa amehukumiwa kifo kabla ya kuachiwa huru hivi majuzi Meriam Ibrahim wa nchini Sudan ameeleza kwamba kitendo cha kujifungua mtoto wake akiwa gerezani ilihali miguu yake ikiwa imefungwa minyororo imemsababishia mtoto wake apate ulemavu.

Meriam ameyaeleza hayo wakati akihojiwa na gazeti la The Guardian la nchini Uingereza kwamba ilikuwa vigumu kwake katika kujifungua binti yake aliyempa jina la Maya kwakuwa miguu yake ilikuwa imefungwa minyororo ndani ya gereza la wanawake la Omdurman lililopo kaskazini mwa jiji la Khartoum nchini humo. Meriam amesema kwamba alilazimishwa kujifungua akiwa katika hali hiyo jambo ambalo lilisababisha kujifungua binti yake kwa shida na kumsababishia ulemavu wa mwili na kwamba amesema hajui endapo Maya atakuwa na uwezo wa kutembea ukubwani ama atahitaji mtu wa kumsaidia.

Meriam ambaye ameachiwa huru mapema wiki iliyopita na mahakama ya rufaa nchini humo, alihukumiwa kifo kwa madai ya kuikana dini yake ya kiislamu na kuwa Mkristo, lakini pia kosa lingine ni kufunga ndoa na mkristo jambo ambalo halitambuliwi na dini yake ya zamani kama ni ndoa halali bali ni uasherati hivyo anapaswa kuhukumiwa kifo.

Mwanamke huyo alikamatwa toka mwezi february mwaka huu na kuishi gerezani pamoja na mtoto wake mdogo wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu. Baada ya shinikizo kutoka mataifa mbalimbali serikali ya nchi hiyo ilimwachia huru lakini akiwa na mumewe uwanja wa ndege wa Khartoum kuelekea nchini Marekani, alikamatwa tena na mumewe kwa madai ya kutumia hati za kusafiri za kufoji jambo ambalo kwa mujibu wa Meriam amelipinga kwamba si la kweli.
Meriam na mumewe Daniel Wani pembeni ni mtoto wao wa kiume.

Meriam na mumewe Daniel Wani wanauraia wa nchi mbili Marekani na Sudan ambapo Daniel anatumia hati ya kusafiria ya taifa la Sudan kusini jambo ambalo serikali ya Sudan imelipinga na kuwataka wote kutosafiri mpaka wamepata nyaraka halali za kusafiri, kitendo ambacho Meriam amekipinga akidai kwamba yeye na mumewe wana haki ya kutumia hati ya Sudan kusini kwakuwa mumewe ametokea huko. Kwasasa Meriam na familia yake wanakaa ndani ya jiji la Khartoum sehemu salama kwa mujibu wa Meriam ingawa hapana uhuru wa kutosha wakisubiri hati mpya za kusafiri.

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI MESS JACOB CHENGULA ATOA HISTORIA FUPI YA MAISHA YAKE NA KUWATAKA WANAOHITAJI USHAURI WA MAFANIKIO WAMUONE

Ukiamua unaweza nikikupa historia yangu kwa ufupi nimezaliwa katika kijiji cha Makangalawe mkoani Iringa wilaya ya Makete. Elimu yangu darasa 7 nilihitimu shule ya msingi nilimwomba baba yangu mtaji baba bila hiana akanipa 30000 nikaenda mji mdogo Makambako nikiwa machinga na uza vitu stand na mwaka nilio pewa mtaji ili 1999 kwakuwa moyo wangu ulikuwa nikufanya biashala nilifanya kazi usiku na mchana na kila fulusa iliyo tokea mbele yangu nilitumia nakumbuka mwaka 2001 nikiwa na miaka 16 nilifanikiwa kukopa mkopo benki ya NMB wakati inabidi uwe na miaka 18 nilipata nikafanya biashara vizuri nikwambie tu mwaka 2003 tayali nilikuwa na hela nyingi nilikuwa na maduka mawili gari ndogo ya kutembelea japo badala ya kadi nilipewa kalatasi tu nikawa na vyombo vya disko kimsingi ndani ya miaka 4 ya mtaji wa 30,000 niliweza kufikia 5,000,000 kwakifupi najuwa hum fb kunawatu wengi ila nataka mtu anaye Taka kufanya biashara na hajiamini anitafute nimpe mbinu jinsi ya kufikia malengo yake nimeishia mwaka 2003 bado kuna shida nyingi hapa kati nimepitia ukiwa kuishiwa kwa uzembe nanini nahitaji kumsaidia mtu mmoja ambaye anaona yuko tayari kufanya biashara.
Mess Jacob Chengula akiwa China

Naomba mnielewe sihitaji Mtu anayesema anaweza au anapenda biashara ninachotaka mimi ukitaka nikupe ushauri kwanza kabisa unaanza kutaja uko mkoa gani na unafanya biashala gani na changa Moto unayo ipata ndipo naweza kupa ushauli kwakile ulicho uliza au kwa mfano mess naomba ushauli sija wahi fanya biashara nina hela yangu mil 1000000 nataka kufanya biashala au mess nina biashara lakini naona kama duka langu halikuwi nifanyaje ndo nataka ushauri huo

OMBENI TAIFA LA ISRAEL




Shalom,

Ombea Israel,
1. Omba ulinzi na amani juu ya Israel hasa wakati huu kuna tension kubwa sana baada ya kupatikana miili ya watoto watatu waliotekwa na kikundi cha kigaidi cha kiislamu, Waziri mkuu wa Israel amesema hao magaidi watalipa kwa kitendo hicho, na sasa Israel imeshaanza kurusha rocket kuelekea Gaza.

2. Omba kwa ajili ya familia ambazo zimepoteza hao watoto Mungu awafariji na pia awape roho ya msamaha na pia kwa taifa la Israel maana imekuwa ni majonzi makubwa huku, Mungu aipe hekima serikali ya Israel hasa wakati huu.

3. Ombea ulinzi juu ya Jerusalem hasa kwa wayahudi kila wakati wanapoenda temple mountain inatokea vurugu kutoka kwa waislam.

4. Pia kuna kikundi cha kigaidi kingine kimeibuka Iraq kilikuwa pamoja na al Qaeda na sasa wamejitenga na inasemekana kuwa ni radical kuliko al Qaeda kinaitwa ISIS itakuwa umeshakisikia kimeteka baadhi ya miji Iraq na sasa inasemekana kuwa lengo lao ni kuteka Jerusalem. Omba ulinzi juu ya Israel na kila lengo la adui lisifanikiwe juu ya Israel.
Unaweza kunukuu maandiko haya Zaburi 121, 122:6-7, Isaya 31:5, Isaya 62:1.

5. Ombea Mungu ainue waombaji wengi watakao simama na kuomba kwa ajili ya Israeli hasa kutoka Tanzania. Isaya 62:6-7.
Mungu awabariki,
“I will bless those who bless you, and whoever curses you I will curse; and all peoples on earth will be blessed through you.” Genesis 12:3
Blessings,
–Grace

Source: Strictly Gospel

WAIMBAJI ZAIDI YA 25 KUVAMIA STAGE MOJA WAKITUMIA MIC MOJA KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU YA NITASEMA NDIYO KWA BWANA YA MDADA WA YESU FURAHA ISAYA

JUDITH KISIMBA KUZINDUA ALBAMU YAKE YA MUNGU NI MKUBWA JUMAPILI 13.07.2014


AUNT EZEKIEL AMWAGA CHOZI UTABIRI WA KIFO CHAKE


SIKU chache baada ya Nabii wa Huduma ya Ufufuo, Buza jijini Dar, Yaspi Paul Bendera kutabiri kuwa vifo vya mastaa vitaendelea, staa wa sinema Bongo, Aunt Ezekiel amemwaga machozi baada ya kuhusishwa kuwa yeye ndiye anayefuata kufa.

Staa wa sinema Bongo, Aunt Ezekiel Kupitia gazeti la Ijumaa, Juni 13, mwaka huu, Nabii Bendera alisema ameoneshwa kwamba wasanii 20 wangekufa hivyo kama wanataka kujinusuru, wafike kanisani kwake na kupakwa mafuta.

Wakati gazeti hilo lilipoingia mtaani, ukurasa wa mbele uliambatanisha picha mbalimbali za baadhi ya wasanii waliofariki pamoja na wengine ambao wapo hai akiwemo Aunt Ezekiel (pichani) ndipo utata ulipoanzia.

Chanzo kilicho karibu na staa huyo, kilipenyeza habari kuwa, ndugu zake walimpigia simu Aunt ambapo walionesha kuwa na hofu ya kifo ambayo ilimfanya mwigizaji huyo naye aangue kilio mara kwa mara.
“Ndugu zake walilia sana kwani baada ya kuona picha ya Aunt katika gazeti, waliamini maneno ya nabii huyo kwa kujua pengine anayefuata kufa kati ya hao kumi ni ndugu yao.

“Aunt alilia sana siku hiyo na Wema (Sepetu) ndiye alisimama kumsihi asiendelee lakini kama haitoshi, bado amekuwa akiteseka mara kwa mara kila anapokumbuka tu, anakosa amani na kujikuta analia,” kilisema chanzo.

Hata hivyo, chanzo kimeeleza kuwa baada nguvu kubwa kutoka kwa marafiki wa karibu wa Aunt akiwemo Wema wamekuwa wakimsihi amuombe Mungu kwani si kwamba picha yake kutumika gazetini ndiyo atakufa wala maneno ya nabii huyo si sababu ya kuamini kwamba kweli vifo hivyo vitatokea.

“Wamemtaka amuombe Mungu na kutosikiliza maneno ya watu maana kuna watu ambao wamekuwa wakishadadia ishu hiyo katika mitandao na kumfanya Aunt aingiwe na hofu ya kifo, kidogo ameanza kuwaelewa,” kilisema chanzo.

Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Aunt, alipopatikana aliweka wazi kuwa suala hilo limemkosesha amani sana pamoja na ndugu zake.
“Walijua ndiyo nakufa, na mimi pia niliposikia harakaharaka niliamini nimetajwa mimi hususan waliponiambia picha yangu imetumika gazetini, nililia sana siku hiyo na siku zilizofuata pia watu walizidi kuniliza mitandaoni, mwisho wa siku nimemwomba Mungu anisimamie, atakaponichukua ni kwa mapenzi yake kama maandiko yanavyosema,” alisema Aunt.

Kwenye utabiri huo, nabii huyo alinukuliwa kuwa ndani ya mwezi Juni, idadi ya wasanii 20 wangefariki lakini hadi sasa hakuna kifo chochote kilichotokea hali ambayo inawafanya baadhi ya watu kuamini kwamba masuala ya kifo ni Mungu pekee anayejua nani atakufa lini.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...