Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Ijumaa, 4 Julai 2014

OMBENI TAIFA LA ISRAEL




Shalom,

Ombea Israel,
1. Omba ulinzi na amani juu ya Israel hasa wakati huu kuna tension kubwa sana baada ya kupatikana miili ya watoto watatu waliotekwa na kikundi cha kigaidi cha kiislamu, Waziri mkuu wa Israel amesema hao magaidi watalipa kwa kitendo hicho, na sasa Israel imeshaanza kurusha rocket kuelekea Gaza.

2. Omba kwa ajili ya familia ambazo zimepoteza hao watoto Mungu awafariji na pia awape roho ya msamaha na pia kwa taifa la Israel maana imekuwa ni majonzi makubwa huku, Mungu aipe hekima serikali ya Israel hasa wakati huu.

3. Ombea ulinzi juu ya Jerusalem hasa kwa wayahudi kila wakati wanapoenda temple mountain inatokea vurugu kutoka kwa waislam.

4. Pia kuna kikundi cha kigaidi kingine kimeibuka Iraq kilikuwa pamoja na al Qaeda na sasa wamejitenga na inasemekana kuwa ni radical kuliko al Qaeda kinaitwa ISIS itakuwa umeshakisikia kimeteka baadhi ya miji Iraq na sasa inasemekana kuwa lengo lao ni kuteka Jerusalem. Omba ulinzi juu ya Israel na kila lengo la adui lisifanikiwe juu ya Israel.
Unaweza kunukuu maandiko haya Zaburi 121, 122:6-7, Isaya 31:5, Isaya 62:1.

5. Ombea Mungu ainue waombaji wengi watakao simama na kuomba kwa ajili ya Israeli hasa kutoka Tanzania. Isaya 62:6-7.
Mungu awabariki,
“I will bless those who bless you, and whoever curses you I will curse; and all peoples on earth will be blessed through you.” Genesis 12:3
Blessings,
–Grace

Source: Strictly Gospel

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...