Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Alhamisi, 30 Januari 2014

ALBAMU YANGU YA NI SHUJAA IKO SOKONI

Kwako wewe ambaye ulikuwa hujui kuhusiana na albamu yangu ya Ni Shujaa, sasa inapatikana madukani. Jipatie nakala yako sasa. Mungu wangu akubariki

DHU..!!!! SIKU ZINAYOYOMA KUFIKIA TAMASHA LA UZINDUZI WA ALBAMU YA MESS JACOB CHENGULA..MUNGU HABADILIKI

Huwezi amini jinsi siku zinavyoyeyuka na tarehe zinavyokimbia kufikia ile siku inayosubiriwa na walio wengi katika kuzindua albamu ya mtumishi wa Mungu Mess Jacob Chengula katika ukumbi tulivu wa wastarabu UBUNGO PLAZA hapa Bongo.

Mess Jacob Chengula
Siku hiyo hapatakalika kabisa kwa maana kutawashwa moto na waimbaji zaidi ya 20 watakaovamia jukwaa moja. Unachotakiwa sasa ni kuweka pembeni kiingilio chako cha Tsh. 10,000 kwa VIP na Tsh 5,000 kwa viti maalumu ili siku hiyo ya tarhe 02 Machi 2014 utumbukie katika eneo la maajabu ya Mungu. Sikia hiyo utasahau shida zako na kufunikwa na wingu la Mungu kwa kupitia uimbaji.
http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2013/05/makamba.jpeg
Naibu Waziri wa Mawasiliano Januari Makamba atakuwa mgeni rasmi siku hiyo.

GLORIOUS WORSHIP TEAM WAKIHUDUMIA AFYA ZAO KWA MISOSI

GWT ni kundi la waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania, ni vijana walioamua kumtumikia Mungu kwa akili zao na mali zao wakiwa bado vijana. Huduma yao ya uimbaji imefanyika baraka kubwa sana kwa walio wengi waliobahatika kusikia au kuwaona wakimtumikia Mungu. Hakika ukiwaona hawa vijana utatamani kuwaona tena na tena kwa wema wao na ukarimu wao. Watanzania tuna bahati kubwa sana kutoka kwa Mungu kwa kile Mungu ameweka ndani ya waimbaji hawa. Kundi lao limesikika Afrika Mashariki kwa matunda yao, wamekuwa wakipata miaaliko mengi sana kwaajili ya kuhudumia mioyo ya watu. Tunawaombea maisha mema na Mungu azidi kulidumisha kundi lao.

Baadhi ya waimbaji wa GWT wakiwa Sinza Mori wakipata msosi wa mchana

RATIBA YA IBADA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYANI KWA NABII FLORA PETER



Kazi imefanywa na Rumafrica +255 715 851523

ALIYEKUWA DANCER WA BONY MWAITEGE BWANA CLAUDY P. MWAKALASYA AACHIA ALBAMU YAKE

 Claudy P. Mwakalasya
Baada oya muda mrefu wa kumtumikia Mungu kwa njia ya kucheza, sasa Mungu ameweza kumuinua tena Claudy P. Mwakalasya kwa kumpa karama nyingine ya uimbaji. Kabla ya uimbaji Claudy akiongea na Rumafrica alisema alikuwa na hamu sana ya kuonana na Bony Mwaitege ili aweze kufanya naye kazi ya kumtumikia Mungu.

Siku ya kwanza ya kuonana na Bony Mwaitege anasema ilikuwa ni muujiza kwake kwani hakutegemea kabisa kuonana naye kutokana na Bony kuwa busy sana na huduma. Alipopaya mpenyo tu, cha kwanza alimuomba ampe nguo yake avae ili apate upako kama wa Bony Mwaitege.

Bony alimkaribisha nyumbani kwake na kuanzia hapo Claudy aliweza kufanya kazi ya Bwana na mtumishi wa Mungu Bony Mwaitege. Kuna mengi ametueleza Claudy P Mwakalasya, wewe endelea kutembelea blogu hii...

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEitGbztBnT_nExP5a14ukyGAvTHwQNVk-XO_qOlPdhoP8wj0eFAj97Gf6-HV8DBiMA9Dfvg4sPWellkbBVTvA-vw97LaNxVMRStIcjREg_zA9AJl5kpbBUJY2artoNOsye9Jbthpc7GChR4/s640/P1.bmp
Bony Mwaitege

ZIKODOLEE PICHA 4 ZA HALI YA MAISHA YA BABU WA LOLIONDO ANAVYOISHI KWA SASA






Hii ni nyumba aliyokuwa anaishi Babu Ambi kabla Dozi ya Kikombe haijachanganya

WATU WA SINZA MAKABURINI ZAMU YENU IMEFIKA YA KUGUSWA NA MUNGU KATIKA MKUTANO HUU MKUU WA INJILI..MTUME NYAGA ATAHUBIRI


Mkutano huu umeandaliwa na Mch. Dk. Alphonce Mwanjala wa kanisa la EAGT Sinza Makaburine na mgeni atakayehubiri ni Mtume Peter Nyaga wa kanisa la RGC Tabata Chang'ombe

Tangazo limetengenezwa na RumAfrica +255 715 851523

TUNAKUALIKA KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU YA MESS CHENGULA YA MUNGU HABADILIKI UBUNGO PLAZA

MIRATHI YA KULOLA, FAMILIA YAMEGUKA

SHETANI ana majaribu yake! Anaendelea kuifuatilia familia ya mtumishi wa Mungu aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT), Marehemu Dkt. Moses Kulola.

Habari za karibuni, mpasuko mkubwa umeibuka baada ya kuwepo kwa sintofahamu dhidi ya mirathi ya marehemu huyo aliyefariki dunia Agosti 29, mwaka jana huku makundi mawili yakiibuka.
Awali, Mchungaji Katunzi aliibuka na kudai kuwa yeye ndiye msimamizi wa mirathi ya ambapo tamko hilo lilipingwa na baadhi ya wanafamilia.
Kwa mujibu wa chanzo makini, hivi karibuni Katunzi alitimuliwa nyumbani kwa marehemu Kulola akiwa amepeleka mchele na pesa taslimu shilingi laki tatu (300,000) alizodai ni sadaka kwa mjane wa marehemu.

Mchungaji wa Kanisa la EAGT City Center, Florian Katunzi.

“Hivi karibuni Mchungaji Katunzi alikwenda kwa mjane wa marehemu akatimuliwa, walidai ni msaliti mkubwa wa familia.
“Wakati akitimuliwa nyumbani hapo maeneo ya Capripoint, Abel (mtoto wa marehemu) naye alimshambulia mchungaji huyo na kumwambia asirudi tena nyumbani kwa marehemu kwani amekiuka miiko ya uchungaji ya kiapo cha uaminifu,” kilisema chanzo chetu na kuomba hifadhi ya jina.
Pia kiliongeza: “Familia kwa sasa ina mpasuko mkubwa, kuna makundi mawili, wapo wanaomuunga mkono Mchungaji Katunzi na wasiomuunga.
“Kundi linalomuunga mkono linaongozwa na watoto wawili wa marehemu (majina tunayo).
Kundi jingine ni la mjane wa Kulola, Elizabeth Kulola linaundwa na watoto wa marehemu wakiongozwa na Abel aliyekuwa dereva wa marehemu, Mchungaji Dany, Goodluck, Mary, Anna, Janga Faith na Susan.
Mke wa marehemu Moses Kulola.

Mchungaji Dany Kulola kwa sasa yuko Marekani na inasemekana kuwa amechukizwa sana na kitendo cha ndugu wanaomuunga mkono Katunzi.
Marehemu Kulola alikuwa na watoto 13, waliofariki dunia ni Flora, Benjamin na Rachel.
Wosia wa marehemu uliopatikana hivi karibuni unaonesha kuwa, mjane wa marehemu ndiye mrithi halali wa mali zote.
Habari zaidi zinasema Katunzi ameshaitwa na wachungaji wa Kanisa la EAGT ngazi za juu na kumtaka ajitoe katika sakata hilo la mirathi lakini anaendelea kufuatilia.
Habari nyingine kuhusu sakata hilo zinasema kuwa, Jumapili iliyopita akina mama 150 wa Kanisa la EAGT Jimbo la Mwanza walikwenda nyumbani kwa marehemu baada ya kusoma habari kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi Toleo Namba 1074 la Januari 25-28, 2014 likiwa na kichwa cha habari; Mgogoro Mzito Mirathi ya Kulola.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, akina mama hao walimuombea mjane wa marehemu huku wakimshutumu vikali Katunzi kwa kufanya jaribio la kumpeleka mahakamani mama Kulola kabla ya kufanyika kwa kikao cha ukoo na kuona nani anaweza kuwa msimamizi wa mirathi hiyo.
Mjane wa marehemu alipozungumza na gazeti hili alikuwa na haya ya kusema:
“Familia yangu ina mpasuko mkubwa, watoto wangu hawaelewani na Katunzi, nimepata mfadhaiko kuhusu mambo ya familia kuanza kuhusishwa na mahakama, watoto wangu siku hiyo walipomfukuza Katunzi nyumbani niliwagombeza sana kwani halikuwa jambo la kawaida.
“Kwa sasa mambo yote namwachia Mwenyezi Mungu, wote ni watoto wangu siwezi kuwabagua hata siku moja. Kinachosumbua hapa ni kila mmoja kuwa na tamaa ya mali za kidunia. Haya yote ni majaribu ya mwovu shetani.”
Jumatatu iliyopita, saa 2:56- 58 asubuhi, Mchungaji Katunzi hakupokea simu ya mwandishiili kujibu madai ya kuwa aliwahi kutimuliwa na baadhi ya watoto wa mzee Kulola kama chanzo chetu cha habari kilivyodadavua.

Jumanne, 28 Januari 2014

NAKUSHUKURU KWA KU-SUPORT KAZI YANGU

Ninakupenda kwa jina la Yesu Kristo, najisikia fahari sana ninpokuwa na mdau wangu ambaye ana-suport kazi zangu. Hakika nimekuona ukiniunga mkono kwa kununua albamu yangu ya "Ni Shujaa" Ninaomba uwambie na rafiki zakoa ambao bado hawajajipatia nakala yao waweze kujipatia. DVD zangu ziko madukani kwaajili yako. Mungu akubariki sana.

Neema Gasper wa Ni Shujaa

BONY MWAITEGE AACHIA UPAKO WA UIMBAJI KWA DANCER WAKE NA KUMTOA KATIKA KILEVI CHA ULANZI

Claudy P. Mwakalyasa ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania. Kabla ya uimbaji alikuwa dancer wa mwimbaji maarufu sana Tanzania, Bony Mwaitege. Amekuwa naye kwa muda mrefu sana kwa kazi ya Mungu. Claudy Mwakalyasa siku ya jana aliweza kuongea na Rumafrika ambapo aliweza kuzungumzia maisha yake kabla ya kuokoka na baada ya kuokoka. Claud moja ya sifa aliyokuwa nayo kabla ya kumpokea Yesu Kristo kuwa mwokozi wa maisha yake, alikuwa ni mtu wa pombe sana hasa kilevi cha ulanzi. Baada ya kusikia huduma ya Bony Mwaitege aliamua kumfuatilia ili aweze kufanya naye kazi. Juhudi za Claud P. Mwakalyasa ziliweza kuleta matunda na baadae akaweza kumpata Bony Mwaitege na kuwa dancer wake.

Claudy P. Mwakalasya


Kuna mengi Claudy Mwakalyasa aliweza kufunguka juu ya maisha yake kabla ya wokovu na baada ya wokovu, njia alizotumia kumpata Bony Mwaitege ikiwa ni pamoja na kuomba vazi la Bony alivae ili apata kuwa kama Bony Mwaitege kwa kuimba, matatizo mbalimbali aliyopambana nayo katika huduma yake ya kucheza, sababu zilizomfanya aachane na ku-dance na Bony Mwaitege na kusimama kama mwimbaji, nini anazungumzia juu ya waimbaji wengine wa nyimbo za injili. Endelea kufuatilia habari zake kwa kupitia blogu yetu hii.

Unaweza kuwasiliana naye kwa simu +255 756 573 788 au +255 712 616 112


MUNGU WANGU WA MBINGUNI NA AKUBARIKI.

Source: Rumafrica
www.rumaafrica.blogspot.com

HIVI NDIVYO MWINJILISTI ALIVYOMUUA MKEWE KWA KUMCHINJA KAMA KUKU

YULE Mwinjilisti wa Kanisa la Angilikana lililopo Kijiji cha Gama Makaani wilayani Bagamoyo, Pwani, Elikia Daniel (35) aliyemuua mkewe Mboni Patrick (28) kwa kumchinja kikatili naye kujinyonga, simulizi yake inashangaza.

Baada ya mauaji hayo, waandishi wa Uwazi walikwenda kwenye kijiji hicho kilichopo kilomita 100 kutoka jijini Dar es Salaam na kukutana na ndugu, jamaa, marafiki wa marehemu wote sanjari na uongozi wa kijiji.

MWANZO WA MKASA

Wakisimulia kwa masikitiko, wakazi wa kijiji hicho walisema siku ya tukio, Mwinjilisti Elikia na mkewe, Mboni walikwenda msituni kukata miti kwa ajili ya kuchoma mkaa wa biashara. Walikuwa wameongozana na mtoto wao wa miaka (12) ambaye jina halikupatikana mara moja.

Baada ya kufika msituni, simulizi inasema, majira ya saa tatu asubuhi, mwinjilisti huyo alimtaka mwanaye huyo kurudi nyumbani kupika.
“Yule mtoto alipika chakula na kukiweka kwenye ‘hotipoti’ kwa ajili ya kuwapelekea wazazi. Alikwenda msituni akiwa ameambatana na mtoto wa jirani ambaye ni rafiki yake.

Waombolezaji wakiwa msibani.

WAZAZI HAWAPO
“Alipofika msituni, mahali alipowaacha wazazi wake hakuwakuta, akawaita kwa muda mrefu, baba, mama lakini ukimya ulitawala eneo lile.

“Katika juhudi za kuwasaka huku na kule, mtoto alishangaa kuona damu nyingi imetapakaa eneo lile na aliposogea akashangaa kuuona mkono wa mama yake ukiwa umetokeza nje huku mwili wake umefunikwa na magogo kwenye tanuri walilokuwa wakitumia kuchomea mkaa,” alisema ndugu mmoja wa marehemu Mboni aliyeomba hifadhi ya jina lake.

WATOTO WAKIMBIA KIJIJINI KUSEMA
Simulizi inazidi kuweka wazi kwamba, baada ya kuona hali hiyo, watoto hao huku wakilia walikimbilia kijijini ambapo waliwaambia watu walichokutana nacho msituni.
Wanakijiji walikukusanyika na kwenda eneo la tukio kushuhudia mwili wa mwanamke huyo.

MSAKO WAANZA
Kwa vile wawili hao waliachwa msituni na mtoto wao, wanakijiji waliamini kwamba, Elikia ndiye aliyefanya mauaji hayo, wakaanza kumsaka.
Walitembea umbali mrefu, wakafika mahali na kukuta nguo za mwinjilisti barabarani, waliposogea sehemu yenye miti iliyoshonana ndipo walipouona mwili wa Elikia ukining’inia mtini. Hakuacha ujumbe wowote.

NINI CHANZO?
Akizungumza kuhusu mauaji hayo, mwenyekiti wa eneo hilo, Ali Thabiti alisema kwa jinsi alivyopata taarifa kutoka kwa majirani, chanzo cha mauaji hayo ni fedha za mkaa. Mwinjilisti alikuwa akidaiwa fedha na mkewe lakini alikuwa akimzungusha kumlipa.

Alisema mgogoro wa marehemu hao ulikuwa wa muda mrefu, walishapelekwa mpaka kanisani kusuluhishwa, mwinjilisti alikubali ana makosa na kuahidi kwamba atangemlipa mkewe fedha za mkaa wake wa magunia mia moja alizokuwa akimdai.

“Usiku wa kuamkia siku ya tukio, mtoto alisema alimsikia baba yake akimwambia mama yake kuwa atamuua na kweli akamuua asubuhi iliyofuata,” alisema jirani mmoja.

UNAWEZA KUAMINI HII?
Vyanzo mbalimbali kijijini hapo vilieleza kuwa, mwinjilisti huyo aliwahi kudaiwa kumuua mtu (jina halikupatikana) huko Kigoma kwa kutumia nondo ambayo alimpiga nayo kichwani.

KUMBE MKE ALIKUWA MJAMZITO?
Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio wakati daktari alipofika kuupima mwili wa marehemu Mboni, taarifa ilitoka kwamba mwanamke huyo alikuwa na ujauzito wa miezi mitatu wakati anauawa.

NI MAUAJI YA KUTISHA
Mwili wa marehemu Mboni ulikutwa ukiwa na majeraha mengi, kubwa zaidi ni la shingoni kwani mumewe alimchinja kama kuku.

MWINJILISTI AZIKWA NA SANDA YA KIROBA
Baada ya polisi kufika eneo la tukio na daktari kufanya uchunguzi, wanakijiji walifikia uamuzi kwamba mwanamke azikwe eneo hilohilo ulipokutwa mwili wake, mwinjilisti alizikwa chini ya mti aliojinyongea, tena mwili wake ukiviringishwa kwenye kiroba. Wote walizikwa bila majeneza na miili yao iliharibika.

ASKOFU MOKIWA AMKANA MWINJILISTI
Uwazi lilizungumza na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, Valentine Mokiwa (zamani alikuwa askofu mkuu Tanzania) ambaye alikana marehemu Elikia kuwa mwinjilisti wa kanisa hilo.

“Si kweli. Anglikana hatuna mwinjilisti huyo. Nimesoma kwenye vyombo vya habari kuhusu madai hayo, waandishi hawakuchunguza vizuri,” alisema Askofu Mokiwa.

Jumatatu, 27 Januari 2014

SIKU YA UZINDUZI WA ALBAMU YA MUNGU HABADILIKI IMEKARIBIA SASA...JIANDAE ILI USIKOSE

Siku zinasonga mbele na ile siku inayosubiriwa na walio wengi ya kumtukuza Mungu imekaribia. Ni muda wako sasa wa kujiwekea kiingilio chako pembeni ili siku ikifika usipate shida ya kujumuika na wenzako katika kumuinua huyu Bwana Yesu Kristo kwa kupitia uzinduzi huu wa kipekee na fungua mwaka.

Mess Jacob Chengula akitoa zawadi ya soda kwa watoto walioachwa na ndugu zao katika mazingira tatanishi. Tour hii iliandaliwa na wanafunzi wa Ustawi wa Jamii (Social Club Tour)
Mess Jacob Chengula amekuwa akishiriki katika madhabahu mbalimbali kumwimbia Mungu wetu. Na amekuwa karibu sana na jamii kwa kutoa misaada mbalimbali katika sehemu mbalimbali. Ngudu yangu na jamaa yangu usikose kabisa siku ya tarehe 02 Machi 2014 saa 6 mchana kwa kiingilio cha 10,000 VIP na viti  vya kawaida ni 5,000 tu ya Kitanzania
Kutakuwa na waimbaji ishirini kuvamia stage moja wakitumia MIC moja na ukumbi moja katika kuzindua albamu moja ya mtumishi wa Mungu mmoja, Mess jacob Chengula

MWALIMU LILIAN NDEGI AKAMIA KUUKOMBOA UZAO WA MWANAMKE

Ritha Chuwalo,

GK Guest Contributor

Mwalimu Lilian Ndegi akizungumza jambo kuhusu kitabu chake.

Wito umetolewa kwa wanawake wajawazito, wakina mama walio katika malezi pamoja na mabinti kusoma kitabu cha Mungu na Uzao Wangu kilichoandikwa na Mwalimu Lilian Ndegi wa Kanisa la Living Water Centre chini ya mtume Onesmo Ndegi lililopo Kawe jijini Dar-es-salaa, Tanzania.

Akitoa wito huo katika uzinduzi wa kitabu hicho hivi karibuni, Mwalimu Lilian Ndegi amesema kuwa, kitabu hicho ni msaada mkubwa kwa wakinamama wajawazito kwani watapata maarifa ya Ki-Mungu yatakayowasaidia kuwaondoa katika uharibifu wa mimba tangu inapotungwa, inapolelewa, pamoja na wakati wa kujifungua mtoto na kwamba hiyo inawahusu pia na mabinti ili kuwasaidia kuwa na uzazi mwema hapo baadae.


Akifafanua zaidi amesema kuwa Serikali ya Tanzania imeweka utaratibu mzuri wa kujenga vituo vya afya kuwasaidia wakina mama wajawazito, na kwamba mila na desturi nazo zina kanuni zake, lakini wakati umefika kwa Kanisa kujihoji Mungu anasema nini juu ya uzao wa Mwenye Haki na kwamba litembee katika kanuni zipi ili kuweza kupata ushindi mkubwa katika Uzazi.

Aidha amesema kitabu hicho kimebeba ujumbe wa Mungu wenye kusudi maalum juu ya maisha ya kiroho na kimwili, utakaofungua ufahamu wa watu na kuliona pendo kuu la Mungu juu ya maisha yao na uzao wao maana Mungu anaanza kushughulika na uzao wa mwenye haki kizazi hata kizazi.
Mwl. Lilian Ndegi ameongeza kuwa kama ambavyo ilikuwa kwa Ibrahim kupitia kitabu hicho cha Mungu na Uzao Wangu, wazazi na walezi kwa ujumla watajifunza mambo muhimu ambayo Mungu anawaagiza kufanya, kama sehemu ya wajibu wao kwa mfano; Mume kumtunza mkewe siku zote, kuwalea na kuwatunza watoto pamoja na kuziona athari za kinywa katika ulimwengu wa roho zinavyoweza kuathiri maisha ya uzao wao kutokana na kuwanenea maneno au kuwapa majina yasiyofaa kama vile kumwita mtoto majina kama Mateso na kadha wa kadha.

Mtume Onesmo Ndegi akinadi kitabu mara baada ya kuzinduliwa.

Kwa upande wake mgeni rasmi ambae ni mkuu wa makanisa ya Living Water Center nchini Tanzania, Mtume Onesmo Ndegi ambaye pia ni mume wa Lilian Ndegi, amewaasa Wanaume kuwa chachu ya mabadiliko katika ndoa zao, badala ya kujifanya wana misimamo isiyobadilika, na kuwataka kubadilika wao kwanza katika mitazamo yao juu ya wake zao na ndipo itakapo kuwa chachu kwa wake zao kubadilika kitabia na mienendo katika ndoa.

Aidha ametoa wito kwa vijana wa kiume kuwa na Mungu zaidi katika ujana wao ili kumpata mke mwema atokae kwa BWANA atakaeweza kuwa msaidizi wa kweli katika maisha kiroho na kimwili, huku akimshukuru Mungu kwa ajili ya Mke wake Lilian alie mtaja kuwa wa maana sana katika maisha yake na kwamba amefanyika baraka na msaada si tu katika huduma, bali pia kwenye familia kwa ujumla.


Mtume Onesmo Ndegi akimpongeza Mkewe, Lilian Ndegi.

Mtume Ndegi amewataka wanaume wote kuiga mfano huo wa kuwasifu wake zao na kuwashukuru pamoja na kuomba msamaha wanapokosea, ili ndoa zao zijengwe katika misingi ya urafiki na penzi la kweli na sio ubabe kama ilivyo miongoni mwa wanajamii wengi.

Kitabu cha Mungu na Uzao Wangu kimezinduliwa tarehe 19 jan 2014 ambapo pamoja na mambo mengine Mwl. Lilian Ndegi ameelezea kwa kina juu ya Uzao wa mwenye haki, Nalikujua kabla ya Mimba Haijatungwa Tumboni mwa Mama Yako, Nafasi ya Mwanamume Wakati wa Ujauzito Mpaka Malezi, Magonjwa na Mateso Mengineyo Katika Kipindi cha Ujauzito, Mtazamo wa Wazazi juu ya Uzao Wao, Mtazamo wa Mungu juu ya Uzao wa Mwenye Haki, Mwanamke anahitaji ujasiri Mwingi wakati wa Kujifungua pamoja na uzazi wa Mpango ndizo sura 8 za kitabu hicho.


Mtume Ndegi na mkewe wakikata keki kuashiria uzinduzi wa kitabu cha Mungu na Uzao Wangu hivi karibuni jijini DSM.


Mwl. Lilian Ndegi akimlisha keki Mch.Naomi Mhamba wa Living water Centre Kawe Dar es Salaam


Mtume Onesmo Ndegi akisalimiana na mhariri wa kitabu cha Mungu na Uzao Wangu, Mzee Ernest Tarimo

Sifa kwa kwenda mbele, Mkurugenzi wa makanisa ya Living Waters Tanzania, Mchungaji Grace Mbwiga (wa kwanza kushoto)

Upendo Nkone akisindikizwa na wenyeji wake kumsifu Mungu.

Sifa zikiendelea kurudishwa kwa BWANA Yesu muweza wa yote,

Mtangazaji wa WAPO Radio FM, MC Ritha Chuwalo (wa kwanza kushoto) akifurahia jambo pamoja na umati.

Salamu za kipekee, Mtume Onesmo Ndegi na Bwana Diesco Rugambage mara baada ya salamu na kuahidi.
Katibu Mkuu makanisa ya Living Waters Tanzania Mch. Peace Matovu madhabahuni akimkaribisha Mgeni rasmi Mtume Ndegi hayupo pichani.

Hiki ni kitabu cha pili kikitanguliwa na kitabu chake cha kwanza JE UNASAMEHE? Ambavyo vyote vinapatikana madukani jipatie nakala yako kwa jumla na rejareja kwa kupiga simu namba 0754465578 au 0655465578 ma kwa kuwasiliana na mwandishi kwa barua pepe lilyonesmo@gmail.com web: www.lwc.or.tz.

MUNGU AZIDI KMBADILISHA LULU NA SASA AACHANA NA KILEVI CHOCHOTE

Lulu akiwa katika muonekana mpya na hii ni baada ya mdada huyo kutangaza kuachana na matumizi ya kilevi jambo ambalo kila mpenda watu wastaarabu watakuwa amemuunga mkono kwa kitendom hicho kwani pombe imekuwa ikiwabadilisha akili watumiaji wake na kujikuta wakifanya mambo yanayowakera watua ama jamii kwa ujumla.

TAMASHA KUBWA LA KWANZA LA KUSIFU NA KUABUDU KWA MWAKA 2014 LAFANA .

TAMASHA kubwa la kwanza la kusifu na kuabudu kwa mwaka 2014 Lafana .Tamasha hilo ambalo hufanyika kila jumapili ya mwisho mwezi lilifanyika jumapili iliyopita (26.01.2014) pale Dar es Salaam Pentecoste Church ( DPC) .

Lilijumuisha wasanii kadhaa wa nyimbo za injili akiwemo John Lisu na kwaya ya rivers of life ya DPC .
Pata habari zaidi kwa njia ya picha .

Mc Boniface & Joyce M wa DPC : 

Sehemu ya kwaya ya Rivers of life wakiwa jukwaani .





Picha kwa hisani ya DPC na Worshipers family Tanzania
Imetayarishwa na Erasmus Augustine.

Jumatano, 22 Januari 2014

HABARI NJEMA MKAZI WA MBEZI MWISHO, MTUME MOSES KINGU NA MTUME PETER NYAGA KUHUBIRI IINJILI MALAMBA MAWILI..USIKOSE


Creativity RumAfrica +255 715851523

MOJA YA KAZI ALIZOFANYA MTUMISHI WA MUNGU MESS JACOB CHENGULA KATIKA MADHABAHU MBALIMBALI. ANGALIA CLIP HII UTANAMBIA....USIKOSE UBUNGO PLAZA KATIKA UZINDUZI WAKE...


Hakika ukiangalia hii clip utaamini kuwa watu wamezipokea nyimbo za Mess Jacob Chengula kwa mikono miwili. Watu wamejiachia katika clip hii, wakicheza bila steps ili mradi sifa na utukufu zimrudie Mwenyezi Mungu. Ukiangalia kwa makini utaona hata Mess Chengula mwenyewe alifika point akawa haamini watu walivyoupokea wimbo wake "MUNGU WETU HABADILIKI|"

Mess Jacob Chengula

Sipati picha hiyo siku ya tarehe 2 Machi 2014 katika ukumbi tulivu wa UBUNGO PLAZA hapa jijini Dar es Salaam, hapatakalika kabisa siku hiyo!!. Ninakusihi  usikubali wala kuwaza kupanga kutofika ukumbini kwa maana utakosa mengi kutoka kwa Mtumishi wa Mungu aliyekubalika machoni pa watu na mbele za Mungu kwa huduma yake hii ya uimbaji. Ukiangalia kwa makini katika clip hii utaona Mess Chengula alivyodata badala ya kupokea pesa wanazomtunza akaanza kurusha pesa kwa wadau. Hii ina maanisha mtumishi wa Mungu anafurahia sana kufanya kazi ya Mungu kuliko kupenda pesa.

Akiwa katika kanisa la Mlima wa Moto

Kitu kingine ambacho kinanichanganya katika albamu hii ni vile Mess Jacob Chengula alivyo-shoot albamu yake katika nchi mbalimbali kama Hong Kong, China, Dubai na Tanzania. Kama mdau wa nyimbo za injili na mzalendo wa nyimbo zetu za kibongo,  unafikiri humo ndani mna utamu wa aina gani?  Ninakusihi mtu wa Mungu usikose kujipatia albamu hii siku ya tamasha la uzinduzi ili ujionee watu wanapokuwa kuwa serious kwa kazi ya Mungu.

Mess Jacob Chengula na dancers wake

Mbali na hayo yote, lingine ni juu ya waalikwa watakaosindikiza tamasha hili la fungua mwaka 2014. Mess Jacob Chengula ameweza kualika waimbaji zaidi ya 20 watakaoimba siku hiyo. Ki ukweli binafsi nimeona matamasha lakini hili kiboko kwa kuwa na waimbaji wengi namna hii na ni waimbaji wale ambao wana majina makubwa Afrika Mashariki na dunia. Kutakuwa na Rose Muhando, Bony Mwaitege, Masanja Mkandamizaji, Neema Gasper, Ibrahimu Sanga, Silas Mbise wa Wapo Radio, AtoshaKissava na wengine wengi.
Mess Jacob Chengula hakuishia hapo pia ameaalika mabloga kama akina sisi, Rumafrica na wengine wengi watakaofika siku hiyo.

Kutakuwa na kiingilio katika tamasha hili. VIP ni Tshs 10,000 na viti vya kawaida ni Tshs. 5,000. Tamasha la uzinduzi litaanza saa sita mchana ambapo mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Mh. Januari Makamba.


DVD ya Mungu Habadiliki ya Mess Jacob Chengula.




Creativity Rumafrica +255 7158523
www.messchengula.blogspot.com

BLOGGER WA GOSPEL KITAA AKIWA ALIYETOA TAARIFA ZA KIFO NYOTA WA MUZIKI WA INJILI MAREKANI ALIYEFIWA NA BABA YAKE MZAZI

 
Blogger wa Gospel Kitaa (kulia) akiwa na James Fortune mwimbaji aliyetoa taarifa za kifo cha baba yake Tasha, hapa ilikuwa Ruach Ministry Kilburn jijini London mwezi January 2013.

Mwimbaji anayetamba na limbo wake maarufu "Breaks every chains" Tasha Cobbs wa nchini Marekani amefiwa na baba yake mzazi askofu Fritz Cobbs katika taarifa ambayo ilitolewa na mwimbaji mwingine wa injili nchini humo James Fortune kupitia mitandao ya kijamii kwakuwataka wapenzi wa muziki wa injili kumkumbuka katika maombi mwimbaji huyo kwakuwa amefiwa na baba yake mzazi.


Aidha kwa upande wake Tasha hakuandika chochote kuhusu msiba huo isipokuwa amewashukuru mashabiki na wapenzi wa muziki wa injili kwa maombi yao na kumalizia kwakuwaambia kwamba anawapenda.
Hey Family! Thank you for your thoughts and prayers! They are felt! Love you guys!


Tasha Cobbs ambaye siku za hivi karibuni alijinyakulia tuzo za Stellar awards katika kipengele cha mwimbaji mpya wa mwaka kupitia album yake iliyotengenezwa na mwimbaji na mwandaaji wa muziki VaShawn Mitchell ikiwa na wimbo maarufu wa "Break Every Chain"

Mwimbaji huyo alikuwa jijini London pamoja na mwimbaji mwingine Micah Stampley na kundi lake wakati wa sikukuu za mwaka mpya chini ya mwaliko wa kanisa la Ruach Ministry lililochini ya askofu John Francis lililopo Kilburn ambaye amekuwa akiwaalika waimbaji tofauti wa injili kila mwaka kutokea nchini Marekani.

Mapema mwaka jana gwiji wa muziki wa injili nchini humo Donnie McClurkin alifiwa na wazazi wake wote wawili lakini pia wakati mwaka mpya ukianza gwiji huyo alijikuta kipindi chake cha radio kikiondolewa na wamiliki wa radio ya WBLS/WLIB na nafasi yake akapewa askofu Hezekiah Walker na kuwataka mashabiki waliokuwa wakisikiliza kipindi chake kumpa sapoti askofu huyo ambaye aliteuliwa na radio kuchukua nafasi yake, ombi ambalo hata hivyo mashabiki ndugu, jamaa na marafiki wa mwimbaji huyo asilimia kubwa wameonyesha kusikitishwa na kitendo hicho na wengine kuahidi kutosikiliza.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...