Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Jumatano, 22 Januari 2014

SHUHUDA ZITAKAZOKUJENGA KIIMANI KUTOKA KATIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASALA - DAR ES SALAAM

JOSEPHATA AKISHUHUDIA MTOTO WAKE ALIYEKUFA AMERUDI BAADA YA KUFIKA KWA NABII FLORA 

       Bwana Yesu asifiwe, naitwa Josephata Fabian;  mtoto wangu alikuwa anasoma Morogoro, amemaliza kidato cha nne anaingia kidato cha tano. Ilipofika mwezi wa tisa nikapigiwa simu kwamba anaumwa, nilipofika pale nikakuta mtoto amechanganyikiwa, nikamchukuwa nikampeleka Hospitali ya mkoa. Tulilazwa kule akapima vipimo vyote wakasema hana ugonjwa ile mtoto huyu ni kichaa, wakampeleka kwenye hodi ya watu waliochanganyikiwa, nikakaa naye kule mpaka mwanangu akafariki.


Basi sasa hivi nilivyoondoka kwenda kule kijijini wakawa wanasema anakujaga usiku anagonga mlangu na kuondoka, niliporudi tena mwezi huu wa kwanza, nina mtoto wangu anaitwa Imma, usiku akilala anaamka anasema mama washa taa kaka huyu hapa. Nikiwasha taa simuoni mtu, nikimuuliza mbona sioni mtu, anasema mama kaka amekuja lakini hakuongea kitu amesimama tu.  Baada ya kuja huku, jana asubuhi mume wangu ananipigia simu, akaniambia mtoto amekuja saa saba ya usiku, nimemshika lakini nimeshindana naye mpaka saa tisa ananguvu sana.

ASHA RAMADHANI ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMPATANISHA NA MUME WAKE

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Asha Ramadhani
; natokea Kigogo, mimi nilianza huduma kuanzia siku ya Jumatatu, mume wangu alikuwa ananinyanyasa sana, alikuwa analala nje siku tatu, nina watoto wawili alikuwa ananiachia shilingi mia. Nikaja kwa Nabii akanipa huduma ya siku 21, siku Jumatatu nililala, niliporudi nyumbani nikakuta ujumbe kwamba umeambiwa na mume wako, utoe vyombo vyako vyote ujue utakapokwenda.

Nikaamini nimetoka kwa Mungu wangu, Mungu wa Nabii Flora, nikawachukuwa wanangu tukafika nyumbani, tukapika chakula tukala tukawa tumepumzika. Amini hivyo, yule mume wangu alirudi akaingia ndani, nikasema sasa hapa naanza kupigwa, alipofika ndani akapiga magoti akaanza kuniomba msamaha. Kwa kweli siku ya leo ninafuraha sana, wale walioniambia nimeambiwa nitoe vyombo asubuhi wanajiuliza mbona yupo na mume wake, kuniuliza wanashindwa, namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora, napenda kuwaambia kwamba msife moyo Mungu wa hapa anatenda.

KALISTA URASA ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMPA AMANI KATIKA NYUMBA YAKE, NA PIA BINTI ALIYEMLETA KWA NABII FLORA AKIWA ANAUMWA SASA ANANAFUU                          
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Kalista Urasa; kwa kweli Nabii Flora amenitendea mambo makubwa sana, nilipokuja hapa nilikuwa na hali mbaya, moyo wangu ulikuwa unatamani kufa. Lakini Nabii Flora amenisaidia sana, familia yangu sasa hivi wananisikia, na kila ninachoongea wapo na mimi yaani nashukuru sana. Na hata yule dada mgonjwa niliyekuja naye hapa, ilikuwa kila baada ya siku mbili dawa ikiisha namkimbiza Muhimbili, lakini sasa hivi toka nimlete hapa ule ugonjwa ulipanda mara moja tu. Na hata sasa hivi amekataa dawa amesema nimepona, na ule ufahamu wake kidogo unarudi, japo haujarudi sawa lakini naimani kwa Nabii Flora utakuwa sawa.
PATRICK PAULO ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMPONYA MUME WA MTOTO WA KAKA YAKE BAADA YA KUMWEKEA STICKER YA NABII FLORA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Patrick Paulo; natokea Kigogo, Mungu wa Nabii Flora amenitendea mambo makubwa sana, siku ya Jumatatu nilikuja hapa nikaonana na mama. baada ya kutoka hapa majira ya usiku nikapokea taarifa kwamba kuna mume wa mtoto wa kaka yangu amelazwa Muhimbili hali yake ni mbaya sana, kwa hiyo anapumua kwa kutumia mipira. Basi nikamuomba Mungu ambaye ninamuabudu mahali hapa kwa hiyo sikuwa na wasiwasi. Asubuhi nilipofika pale Hospitali kweli yule mgonjwa hali yake ilikuwa ni mbaya, nikakumbuka kauli ambazo walinifundisha watumishi wangu, kwanza nikaongea na Mungu wa mtumishi Nabii Flora. Nikasema kwanza nafunga mauti ya mgonjwa wangu, vilevile nikasema nazuia kupelekwa Thieta, pamoja na vipimo vyote viwili wakasema kwamba anatakiwa afanyiwe operation, nikasema nafunga operation kwa jina la Yesu. Nikachukuwa sticker ya Nabii Flora nikamwekea, nikamwambia mwanangu nimeshafunga kila kitu kuwa na imani mume wako atapona, nikamwambia naondoka ikifika mchana nataka nipokee habari njema, kwa sababu mtumishi wangu Nabii Flora kashafunga mauti. Ilipofika saa sita nikapiga simu kwa mwanagu nikamwambia vipi, akaniambia naona anatapika, nikamwambia huyo ni shetani moto unamuwakia, na bado atakimbia mwenyewe. Kufika saa nane, mwanangu akaniambia ile habari ya kupelekwa Thieta wameahirisha, na vipimo vile hakuna kitu. Ilipofika saa kumi wakampeleka tena kupimwa, wakakuta hakuna kitu, kwa hiyo kwa sasa yupo nyumbani na nitamleta aje kushuhudia.
FLORA ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMPONYA VIRUSI VYA UKIMWI
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Flora; nimekuja hapa toka mwaka 2012 mwezi wa 9, nimekaa hapa karibu mwaka mmoja na nusu, kila ninapoenda kupima sipati mafanikio, lakini Nabii alishanitamkia wewe umeshapona.

Nikamwambia Mungu kama nimeshapona katika ulimwengu wa Roho naomba unidhibitishie katika ulimwengu wa mwali. Toka mwaka jana nilivyopima mwezi wa nane Nabii sikumuonyesha tena vyeti, nikasema sasa Bwana Yesu mimi nimeshapona.

Nikabadilisha maombi badala ya kusema Mungu naomba uniponye, nikawa nasema asante Yesu kwa kuniponya, nikawa naamka asubuhi nasoma ile Zaburi ya 51, na 116, na 103. Lakini kilichoniponya ni ile kuvumilia, sikiliza kile anachokwambia mtumishi wa Mungu, alafu kingine cha msingi unatakiwa kuamka mapema uje kwenye ibada.
 


Mimi kwa mara ya mwisho tarehe 29 nilisema sipimi tena, lakini Nabii alisema kwa mara ya mwisho usikate tamaa inaweza ikawa siku ya leo ndio siku yako ya uponyaji, nikasema kama mtumishi wa Mungu amesema usikate tamaa inaweza ikawa ndio siku yangu. Kweli kila mmoja anasiku yake na mimi siku yangu ilitimia, siku ya Jumatatu asubuhi nikaamka nikawa nafanya kazi zangu lakini kama nimechoka sana.
Nikaondoka nikaenda Hospitali, kabla sijaenda nikachukua sticker ya Nabii Flora nikaiweka kwenye damu kubwa, kufika Hospitali nikaichukuwa nikaishika kwenye kidole kwa sababu damu wanachukuwa kwenye kidole, nikamwambia Yesu hii si damu yangu ni ya kwako naomba majibu yawe negative. Kufika kwa Daktari akaniuliza umeshawahi kupima, nikamwambia ndio, basi akanichukuwa damu alafu akanipa namba nikatoka nje, bada ya muda kidogo akaniita akaniambia mama damu yako ni salama.

MICHAEL AKIELEZEA JINSI NABI FLORA ANAVYOTENDA MAKUU YA MUNGU
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Michael; nililetwa hapa na mchumba wangu, nimejionea mambo ambayo siwesi kuelezea, kwa kulinganisha na maisha niliyokuwa naishi kule Canada. Nilikuwa ni fundi wa kujenga nyumba, nilikuwa najenga kuanzia ghorofa 20 hadi 80, nilikuwa ni mtu ambaye nimebarikiwa pesa, lakini nikazitumia vibaya. Baada ya kuingi hapa fedha yangu situmii vibaya tena.
MUSA ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMPONYA VIRUSI VYA UKIMWI
Kabla sijapata matatizo nilikuwa nasikia Nabii Flora lakini nilikuwa siamini kwamba ni mtu ambaye anatenda mambo makubwa kama haya. Nilikuwa nampinga Nabii Flora mtaani, namsema vibaya, lakini nilipopata matatizo niliweza kufika mahali hapa.
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Musa; namshukuru Mungu nimepona Virusi vya UKIMWI katika madhabahu hii ya Nabii Flora. Nilikuja mwaka jana nikiwa na hali mbaya sana, nilipopewa taarifa za Nabii Flora kwamba anaponya ndio nikafika mahali hapa. 
Kabla sijapata matatizo nilikuwa nasikia Nabii Flora lakini nilikuwa siamini kwamba ni mtu ambaye anatenda mambo makubwa kama haya. Nilikuwa nampinga Nabii Flora mtaani, namsema vibaya, lakini nilipopata matatizo niliweza kufika mahali hapa. 
Nilipofika hapa Nabii Flora alinipa mwezi mmoja, lakini nilitendewa baada ya wiki mbili na siku tatu, namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora.
TERESIA HARUNA ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMPONYA VIRUSI VYA UKIMWI; nilikuja hapa nikiwa naumwa sana, nilipima nikakutwa na Virusi vya UKIMWI toka mwaka 2008.
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Teresia Haruna; nilikuja hapa nikiwa naumwa sana, nilipima nikakutwa na Virusi vya UKIMWI toka mwaka 2008. 
Lakini baada ya kufika hapa na kuombewa tarehe 30/12/2013 nilipokea uponyaji, namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora


BABA ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMPONYA MKE WAKE UKIMWI, KUPATA UJAUZITO NA AMEPATA MFADHILI WA KUMSOMESHEA WATOTO WAKE
Bwana Yesu asifiwe; kwa kweli nashindwa hata nimpe Nabii shukrani gani kwa sababu aliyonitendea ni makubwa sana, mke wangu nilivyomleta hapa alikuwa amechoka akiumwa UKIMWI.
Lakini baada ya kuudhuria kwa wiki moja tu akaanza kubadilika na afya yake kuwa nzuri, nikamwambia mke wangu tusiondoke hapa ndo kuna uzima.

Na pia nimepata mfadhili wa kuwasomesha watoto wangu, nilipata mfadhili wa kusomesha mtoto mmoja lakini baada ya kufika kule wakabadilisha akasema atanisomeshea watoto wangu wote wawili. Napenda kuwaambia muamini tu, msipoamini hamtafanikiwa. Pia juzi wakati anaondoka kwenda Ulaya alinipa machine za kunyolea, na amesema akirudi ananipa pesa ya kuanzisha saloon.
BABA ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUFANYA BIASHARA ZAKE KWENDA VIZURI                                                 
Bwana Yesu asifiwe
; ninamiezi 6 toka nimeanza kuabudu mahali hapa, nilikuwa na Hotel nimefungua hapa Salasala, nipo hapa toka mwezi wa 8 mwaka 2010, toka mwaka huo sijawahi kuona faida yoyote, ikafika hatua mpaka nataka kuchanganyikiwa. Mke wangu mpendwa akaja hapa, alipokuja mimi nilikuwa nampiga vita, kwa sababu nilikuwa namwambia unaenda huko Kanisani ndio kunapesa, nikamwambia kama unaona maisha yamekuwa magumu wewe fanya kazi kwa bidii. Baada ya hapo Mungu kanibadilisha na nitafungua Hotel nyingine muda sio mrefu, na sasa hivi nimeshatumia zaidi ya milioni mia moja. Na pia biashara zangu za magari ya nje, zinakwenda vizuri namshukuru sana Mungu wa mahali hapa.
JINSI YA KUFIKA KANISANI
Kama unatokea Mwenge Dar es Salaam, panda magari ya Tegeta shuka kituo cha Mbezi Mbuyuni uliza kanisa la Nabii Flora
Tembelea
Facebook: Nabii Flora Peter

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...