Blogger wa Gospel Kitaa (kulia) akiwa na James Fortune mwimbaji
aliyetoa taarifa za kifo cha baba yake Tasha, hapa ilikuwa Ruach
Ministry Kilburn jijini London mwezi January 2013.
Mwimbaji anayetamba na limbo wake maarufu "Breaks every chains" Tasha
Cobbs wa nchini Marekani amefiwa na baba yake mzazi askofu Fritz Cobbs
katika taarifa ambayo ilitolewa na mwimbaji mwingine wa injili nchini
humo James Fortune kupitia mitandao ya kijamii kwakuwataka wapenzi wa
muziki wa injili kumkumbuka katika maombi mwimbaji huyo kwakuwa amefiwa
na baba yake mzazi.
Aidha kwa upande wake Tasha hakuandika chochote kuhusu msiba huo isipokuwa amewashukuru mashabiki na wapenzi wa muziki wa injili kwa maombi yao na kumalizia kwakuwaambia kwamba anawapenda.
Aidha kwa upande wake Tasha hakuandika chochote kuhusu msiba huo isipokuwa amewashukuru mashabiki na wapenzi wa muziki wa injili kwa maombi yao na kumalizia kwakuwaambia kwamba anawapenda.
Hey Family! Thank you for your thoughts and prayers! They are felt! Love you guys!
Tasha Cobbs ambaye siku za hivi karibuni alijinyakulia tuzo za Stellar awards katika kipengele cha mwimbaji mpya wa mwaka kupitia album yake iliyotengenezwa na mwimbaji na mwandaaji wa muziki VaShawn Mitchell ikiwa na wimbo maarufu wa "Break Every Chain"
Mwimbaji huyo alikuwa jijini London pamoja na mwimbaji mwingine Micah Stampley na kundi lake wakati wa sikukuu za mwaka mpya chini ya mwaliko wa kanisa la Ruach Ministry lililochini ya askofu John Francis lililopo Kilburn ambaye amekuwa akiwaalika waimbaji tofauti wa injili kila mwaka kutokea nchini Marekani.
Mapema mwaka jana gwiji wa muziki wa injili nchini humo Donnie McClurkin alifiwa na wazazi wake wote wawili lakini pia wakati mwaka mpya ukianza gwiji huyo alijikuta kipindi chake cha radio kikiondolewa na wamiliki wa radio ya WBLS/WLIB na nafasi yake akapewa askofu Hezekiah Walker na kuwataka mashabiki waliokuwa wakisikiliza kipindi chake kumpa sapoti askofu huyo ambaye aliteuliwa na radio kuchukua nafasi yake, ombi ambalo hata hivyo mashabiki ndugu, jamaa na marafiki wa mwimbaji huyo asilimia kubwa wameonyesha kusikitishwa na kitendo hicho na wengine kuahidi kutosikiliza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni