Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Jumatatu, 3 Machi 2014

KANISA ANGLIKANA UGANDA LAKATAA USHOGA, LIKO TAYARI KUJITOA NA MAKANISA MENGINE




Askofu mkuu wa kanisa Anglikana Uganda Stanley Ntagali akizungumza na vyombo vya habari nchini humo.©changing attitude
Kanisa la Anglikana nchini Uganda (Church of Uganda) limesema halitasita kujiondoa kwenye umoja wa makanisa ya Kianglikana na nchi za ulaya endapo wataendelea kusukumwa kuishinikiza serikali ya nchi hiyo kubadilisha sheria iliyowekwa na Rais Yoweri Museveni dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Akizungumza na mwandishi wa AFP askofu mkuu wa kanisa hilo ambalo linaheshima na wafuasi wengi nchini Uganda Stanley Ntagali, amesema nchi za magharibi zinapaswa kuheshimu msimamo na sheria za nchi ya Uganda dhidi ya watu wa mapenzi ya jinsia moja kama hawataki kuheshimu hilo wao kama kanisa Anglikana nchini humo wako tayari kujitoa kwenye muungano wa makanisa hayo na kujiendesha lenyewe.

Askofu Ntagali amesema vitendo vya kishoga ni kinyume na neno la Mungu na kwamba hakuna kiongozi wa kweli wa kanisa ambaye ataruhusu vitendo hivyo ikiwa na kuruhusu watu hao kuoana na kupata kibali cha ndoa na kuongeza kwamba wakiwa katika muunganiko wa kanisa la England wasingependa kuona kanisa hilo linaruhusu vitendo hivyo endapo wataruhusu wao kama kanisa nchini Uganda watajiondoa.

Askofu Stanley Ntagali katikati na wasaidizi wake wakiwa katika moja ya huduma nchini humo ©Church of Uganda.

Tangu Rais Yoweri Museveni apitishe sheria hiyo ya watu wanaojihusisha na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kupata kifungo cha maisha gerezani, sheria hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti katika nchi mbalimbali duniani hususani nchi za magharibi ambako vitendo hivyo vinaruhusiwa kwa asilimia kubwa hadi mataifa hayo kufikia hatua ya kumtaka Rais Museveni kutengua sheria hiyo kwakuwa inakwenda kinyume na haki za binadamu. Rais Museveni alikaririrwa katika moja ya mahojiano akisema "hakuna uthibitisho wa kusema mtu anaweza kuzaliwa shoga…. na mwanaume kumpenda mwanaume mwenzake wakati kuna wanawake wengi warembo wamejaa.. ni uchaguzi wa mtu na si vinginevyo, baada ya kuwasikiliza wana sayansi nimegundua nimepata ukweli" alikaririwa Rais Museveni.

Ukiachana na mataifa ya magharibi ambayo yameijia juu Uganda kwa msimamo wake huo, lakini tukio lililowashangaza waumini wa dini ya Kikristo waliowengi Afrika ni kitendo cha askofu mkuu mstaafu wa kanisa hilo nchini Afrika ya kusini Desmond Tutu naye amelaani Uganda kupitisha sheria hiyo huku pia kukiwa na fununu kwamba askofu huyo aliyeonyesha wazi kuunga mkono vitendo vya mapenzi ya jinsia moja yuko njiani kuanzisha chama kitakachounga vitendo hivyo.

Kanisa kuu la Anglikana Mtakatifu Paul Kampala nchini Uganda. ©Church of Uganda

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...