Kwa kweli tumeshuhudia matamasha mengi sana lakini hili la Jumapili lilikuwa la tofauti sana. Katika matamsha yaliyoongoza kuwa na waimbaji maarufu nchini Tanzania wanaomwimbia Mungu hili la Jumapili ni la kwanza, hatujui huko baadae. Waimbaji kukusanyika kwa pamoja zaidi ya 20 na kumwimbia Mungu si jambo rahisi. Hii ni kwa Neema tu ya Mungu. Mess jacob alikonga mioyo ya watu kwa ubunifu wake na juhudi zake za kuhakikisha waimbaji wote aliotarajia kufika wamefika, hata kama kuna baadhi hakuonekana lakini hakuna kasoro iliyotokea kwa mashabiki wa mambo ya Mungu.
Haya
sasa,,,mzee mwenyewe, Mess Jacob Chengula akimtukuza Mungu na kumsifu
kwa jinsi alivyomfanikisha kutimiza ndoto yake ya kuzindua albamu yake
ya Mungu Habadiliki
Tamasha hili lilifanyika katoika ukumbi wa
Ubungo Plaza na mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Mawasiliano Mh.
Januari Makamba akiongozana na familia yake na baadhi ya watumishi wa
Mungu kutoka katika kanisa la Mito ya Baraka kwa Askofu Mwakiborwa.
Katika tamasha hili kila mwimbaji aliimba kwa kiwango cha
juu sana mpaka mgeni rasmi Mh Januari Makamba kuwaita baadhi ya
waimbaji ili ashikane nao mkono kama ishara ya ku-appreciate kazi yao,
mmojawapo alikuwa Edson Mwasabwite.
Dancers wa Mess Jacob Chengula wakifanya yao kwa utukufu wa Mungu
Baada ya uimbaji kufanyika, mgeni
rasmi akiongozana na wachungaji na wazee wa kanisa kutoka katika kanisa
la Mito ya Baraka kwa Askofu Mwakiborwa anakoabudu Mess Jacob Chengula walipanda jukwaani kwa
lengo zima la kuiombea albamu ile na kuifungua rasmi.
Mgeni rasmi Januari Makamba
alipomaliza kuizindua aliweza kuongea machache kuhusiana na waimbaji.
Aliwapongeza waimbaji kwa ushirikiano wao waliuonyesha katika kumuunga
mkono rafiki yao Mess Jacob Chengula. Alikipongeza Chama Cha Muziki
Tanzania na viongozi wao kwa kazi nzuri wanayofanya kwa waimbaji wa
nyimbo za Injili. Mh Januari Makamba aliwaalika viongozi wa Chama cha
Muziki Tanzania na baadhi ya waimbaji kufika katika Bunge la Jamhuri ya
Muungano ili waweze kutoa matatizo yao na changamoto wanazopata katika
huduma yao ya uimbaji.
Mh. Januari Makamba aliweza kuwaonya
waimbaji wa nyimbo za injili juu ya style za uchezaji ambazo hazina
baraka kwa mwenyezi Mungu kuziacha na kucheza kama vile Mungu anavyotaka
watu wake wamchezee. Pia aliwaonya wale waimbaji ambao wamebarikiwa na
kuwa maarufu sana, waachane na tabia ya kujivuna na kujiona wao ni wao.
Mbali na kuwaalika katika Bunge, pia aliwaomba waimbaji na viongozi
kutosita kufika ofisini kwake muda wowote na hakuna mtu atakayeweza
kuwazuia kumuona hata kama atakuwa na majukumu mengi, lakini katika
masuala ya Mungu kwa kupitia waimbaji na viongozi wa nyimbo za injili
yuko tayari kusimamisha kwa muda na kuwasikiliza.
ZAMU YA MALIKIA WA NYIMBO ZA INJILI TANZANI ROSE MUHANDO KUFANYA YAKE STEJINI KWA UTUKUFU WA MUNGU BABA
Malikia wa Muziki wa Injili Tanzania Rose Muhando akifanya yake kwa utukufu wa Mungu
Rose Muhando akihakikisha kazi ya Bwana inasonga kwa uimbaji
Rose Muhando
Dancers wa Rose Muhando
MAMA JANUARI MAKAMBA KUMTUNZA ROSE MUHANDO WAKATI AKIIMBA STEJINI
MAMA JANUARI MAKAMBA KUMTUNZA ROSE MUHANDO WAKATI AKIIMBA STEJINI
Mke wa Mh Januari Makamba aliyeshika mkono mwanae akielekea stejini kumtunza Rose Muhando
Mama Januari Makamba na mwanae (kushoto) wakielekea katika kiti chao baada ya kumtunza Rose Muhando stejini
ZAMU YA MZEE WA NI KWA NEEMA TU, EDSON MWASABWITE KUMTUKUZA MUNGU KWA NJIA YA UIMBAJI
ZAMU YA MZEE WA NI KWA NEEMA TU, EDSON MWASABWITE KUMTUKUZA MUNGU KWA NJIA YA UIMBAJI
Edson Mwasabwite akiimba wimbo wake wa Ni kwa Neema tu
WAIMBAJI WAKIONYESHA UMOJA NA UPENDO WAKIWA STEJINI WAKATI EDSON MWASABWITE AKIIMBA
WAIMBAJI WAKIONYESHA UMOJA NA UPENDO WAKIWA STEJINI WAKATI EDSON MWASABWITE AKIIMBA
Kutoka kulia ni Atosha Kissava, Beatrice Mwaipaja, Neema Gasper na Tumaini Njole
ULIFIKA WAKATI WA MH. JANUARI MAKAMBA KUONDOKA BAADA YA ZOEZI ZIMA LA UZINDUZI KUFANYIKA
Mh.
Januari Makamba akiwaaga waimbaji wa nyimbo za injili mara baada ya
kumaliza zoezi la uzinduzi wa albamu ya Mess Jacob Chengula. Hapa
anasalimina na Mwinjilisti Sarah Mvungi ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo
za injili na ni daktari
MADAMU RUTI WA JANA IMEPITA AKIMTUKUZA MUNGIU SIKU HIYO
MADAMU RUTI WA JANA IMEPITA AKIMTUKUZA MUNGIU SIKU HIYO
Madam Ruti akiimba wimbo wake wa jana imepita
Madam Ruti akiimba wimbo wake wa jana imepita huku watu wakipokea baraka zao na mioyo yao kufarikika na kufurahi
UPENDO NKONE MAMA WA KULALAMIKA KWA NYIMBO ZAKE ZA HISIA AKIMTUKUZA MUNGU SIKU HIYO
UPENDO NKONE MAMA WA KULALAMIKA KWA NYIMBO ZAKE ZA HISIA AKIMTUKUZA MUNGU SIKU HIYO
Hata sasa vidole juu..Upendo Nkone kiboko, Mungu anamtumia ipasavyo kwa uimbaji
FARAJA NTABOBA KUTOKA CONGO HAKUKOSA SIKU HIYO KUMTUKUZA MUNGU
Faraja Ntaboba kutoka nchi ya Congo siku hii aliimba wimbo wa Yuko Mungu
TUMAINI NJOLE MWENYE MIONDOKO KAMA YA ROSE MUHANDO NA SAUTI KAMA YA ROSE MUHANDO SIKU HIYO ALIPAGAWISHA WATU KWA KUCHEZA NA KUIMBA
TUMAINI NJOLE MWENYE MIONDOKO KAMA YA ROSE MUHANDO NA SAUTI KAMA YA ROSE MUHANDO SIKU HIYO ALIPAGAWISHA WATU KWA KUCHEZA NA KUIMBA
Tumaini Njole
MESS JACOB AKIFUNGA TAMASHA LAKE KWA UIMBAJI NA KUWASHUKURU WALE WOTE WALIOFIKA KUMUUNGA MKONO
Picha zimepigwa na RumAfrica
Tembelea
+255 715 851523
POSTER NA TIKETI NI KAZI YA RUMAFRICA. TUNAKUKARIBISHA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni