Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Alhamisi, 6 Machi 2014

CHAKULA CHA BWANA ALICHOWALISHA NABII FLORA WAUMINI WA KANISA LAKE SIKU YA JUMAPILI 02.03.2014

Designer: Rumafrica +255 715 851523 www.rumaafrica.blogspot.com

  Biblia inasema: Wale waandishi wa mfalme wakaitwa pale pale, ilikuwa siku ya tarehe 23 ya mwezi wa tatu, kama vile Modekai alivyoamuru, Wayahudi wakaandikiwa pamoja na Maakida, na Maliwali, na wakuu wa majimbo toka bara hili mpaka Kushi, majimbo mia na ishirini na saba, kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; maana ya jimbo ni kipawa alituma kwa kila jimbo na akaandika kwa mwandiko wake, ukisikia kalamu, kalamu ni kipawa, sasa Mungu anakwenda kuachilia kwa majimbo mbalimbali.



Nabii Flora Peter akihubiri siku ya Jumapili

Biblia inasema: Katika barua hizo mfalme aliwaruhusu Wayahudi wakusanyike katika kila mji na kusimamia maisha zao; yaani simamia maisha yako katika mwezi Wasiwani, usikubali shetani aende kuharibu maisha yako, mimi sikubali hata mmoja kumpoteza, hata kufiwa nilishaapa sinta fiwa kwa UKIMWI, wala Kansa, Wala wachawi.


Biblia inasema: Bwana akawaruhusu Wayahudi kuuwa na kuangamiza; nasi tunakwenda kuuwa UKIMWI na kuangamiza, lazima vitu viangamie kama ni magonjwa yataangamia, UKIMWI utaangamia, umaskini na ufukara unakwenda kuangamia.



Isaya 61:1-4
Biblia inasema: Roho ya Bwana Mungu hii juu yangu, kwa sababu amenituma kuwahubiri wanyenyekevu habari njema, amenichukuwa ili kuwaganga waliovunjika moyo; anasema tazama Roho ya Bwana Mungu hii juu yangu, Bwana amenituma kuwaganga waliovunjika mioyo, haijalishi umejeruika kiasi gani, nimetumwa kukuganga wewe uliyevunjwa moyo wako.



Biblia inasema: Na kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao; yamkini umefungwa, unatembea lakini watu wameshakupiga pini, umepigwa biashara haziendi, ndani ya ndoa huna furaha, leo nimetumwa kuwafungua wale waliofungwa, nimetumwa kutangaza habari ya kufunguliwa kwao.



Biblia inasema: Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika, na siku ya kisasi cha Bwana, na kuwafariji wote waliao; nimekuja kukufariji wewe unayelia upate furaha badala ya maombolezo, badala ya sikitiko tukuvike furaha. Yamkini umefungwa biashara haziendi, haijalishi wamefunga nyota yako chini ya mvungu, chini ya dari tunakwenda kuitoa. Hatuwezi kushindwa nguvu za giza haziwezi kumshinda Yesu.

Kutoka 19:1
Biblia inasema: Mwezi wa tatu baada ya kutoka wana wa Israeli katika nchi ya Misri; na leo unakwenda kutoka katika mikono ya wachawi, walioiba nyota yako, Wa Israeli walitoka katika nchi wa Misri ilikuwa ni mwezi wa tatu, na leo nataka nikutoe unayenitazama kwenye youtube na kunisoma kwenye blogu na facebook nataka nikutoe katika mikono ya Wamisri. Leo ni siku ya kutoka kwako kwa jina la Yesu, wamefunga ndoa yako, kizazi chako, unakuwa ukifanya biashara zinafeli hao ni Wamisri, na leo unakwenda kutoka.

Biblia inasema: Wakapiga kambi huko huko wakiukabili ule mlima; leo tunapiga kambi tukiukabili mlima wa magonjwa, watu waliokufa lazima warejee, nyota yako lazima irejee, sitatulia wala sitanyamaza mpaka haki yako ipate kurejea.


Tembelea
www.nabiiflora.blogspot.com
JINSI YA KUFIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASLA KWA NABII FLORA PETER
Kama unatokea Mwenge, panda magari ya Tegeta, shuka Mbezi Mbuyuni, uliza kanisani kwa Nabii Flora peter

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...