Siku ya jana ilikuwa ni siku ya furaha na ndelemo katika ukumbi tulivu
wa Ubungo Plaza katika kukamilisha kusudi la Mungu juu ya mwimbaji
maarufu Tanzania Mess Jacob Chengula alipokuwa akizindua albamu yake ya
"Mungu Habadiliki" Tamasha hili lilisindikizwa na waimbaji zaidi ya 20
waliovamia jukwaa na kuwaacha watu kupagawa na uwepo wa Mungu
ulioachiliwa kwa njia ya uimbaji. Viti vilikuwa havikaliki na kuwaacha
ma-MC kuwa katika wakati mgumu sana wa kuwaomba watu wakae chini.
Kila mwimbaji aliimba kwa kiwango cha
juu sana mpaka mgeni rasmi Mh Januari Makamba kuwaita baadhi ya
waimbaji ili ashikane nao mkono kama ishara ya ku-appreciate kazi yao,
mmojawapo alikuwa Edson Mwasabwite.
Baada ya uimbaji kufanyika, mgeni
rasmi akiongozana na wachungaji na wazee wa kanisa kutoka katika kanisa
la Mito ya Baraka kwa Askofu Mwakiborwa anakoabudu Mess Jacob Chengula walipanda jukwaani kwa
lengo zima la kuiombea albamu ile na kuifungua rasmi.
Mgeni rasmi Januari Makamba
alipomaliza kuizindua aliweza kuongea machache kuhusiana na waimbaji.
Aliwapongeza waimbaji kwa ushirikiano wao waliuonyesha katika kumuunga
mkono rafiki yao Mess Jacob Chengula. Alikipongeza Chama Cha Muziki
Tanzania na viongozi wao kwa kazi nzuri wanayofanya kwa waimbaji wa
nyimbo za Injili. Mh Januari Makamba aliwaalika viongozi wa Chama cha
Muziki Tanzania na baadhi ya waimbaji kufika katika Bunge la Jamhuri ya
Muungano ili waweze kutoa matatizo yao na changamoto wanazopata katika
huduma yao ya uimbaji.
Mh. Januari Makamba aliweza kuwaonya
waimbaji wa nyimbo za injili juu ya style za uchezaji ambazo hazina
baraka kwa mwenyezi Mungu kuziacha na kucheza kama vile Mungu anavyotaka
watu wake wamchezee. Pia aliwaonya wale waimbaji ambao wamebarikiwa na
kuwa maarufu sana, waachane na tabia ya kujivuna na kujiona wao ni wao.
Mbali na kuwaalika katika Bunge, pia aliwaomba waimbaji na viongozi
kutosita kufika ofisini kwake muda wowote na hakuna mtu atakayeweza
kuwazuia kumuona hata kama atakuwa na majukumu mengi, lakini katika
masuala ya Mungu kwa kupitia waimbaji na viongozi wa nyimbo za injili
yuko tayari kusimamisha kwa muda na kuwasikiliza.
Picha zimepigwa na RumAfrica
+255 715 851523
Tembelea
TUONE BAADHI YA MATUKIO SEHEMU YA KWANZA
Mkurugenzi wa RumAfrica Rulea Sanga (wa pili kutoka kulia) tembelea blogu yake www.rumaafrica.blogspot.com
Rulea Sanga
Rulea Sanga
Viti maalumu kwaajili ya Mgeni rasmi na crew yake.
Wauzaji wa tiketi
Tiketi zilizotumika katika uzinduzi huu. Kazi imefanywa na RumAfrica +255 715 851523
Masanduku yaliyobeba DVD za Mungu Habadiliki kabla ya kuzinduliwa
MC Chiwalo wa Wapo Radio na Boniface Magupa wa PPR
Miriamu Lukindo
Blogger Jimmy akiwa kazini
Ibarahimu Sanga
Betrice Mwaipaja
Bahati Bukuku
Atosha Kissava
Atosha Kissava
Mwinjilisti Sarah Mvungi
MC Boniface Magupa
Joshua Makondeko na madanza
Joshua Makondeko na madanza
Atosha Kissava (kulia)
USIKOSE KUANGALI SEHEMU YA PILI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni