Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Jumatatu, 3 Machi 2014

MZUNGU ABADILISHA MWILI WAKE NA KUWA MWAFRIKA BAADA YA KUONA WADADA WANATAMANI WATU WEUSI HUKO ULAYA

MZUNGU AJIAAFRIKA WAKATI MWAAFRIKA AJICHUBUA..HILI NI BALAA LA 2014

Aaaaaaahhhh jamani..!!! Dunia inaenda wapi sasa....???? Watu waanamua kumkufulu Mungu sasa........!!! Tumeona Waafrika wakijichubua na kutaka kuwa kama wazungu, lakini leo hii wazungu wanataka kuwa kama Waafrika, sasa hii ni kujichubua au kujiafrika....??? mimi sielewiiiiii...!!!  Mungu wetu anaonekana alifanya makosa kukupa rangi aliyokuumba na ndio maana unaamua kujibadilisha kwa kujichubua na kujiaafrika. Jamani tunakosea kabisa na ndio maana Mungu wetu anaachilia magonjwa kama kansa, kuharibika kwa ngozi yako na kuuwa cell za ngozi yako kutoka na ujinga unaofanya.

Shetani ameweka upovu katika macho yako na kuvuruga fahamu zako ili usitambue madhara ya kupandilisha mwili wako. Kama unaakili kweli na unajitambua, huwezi kufanya jambo ambalo unaona kabisa waliofanya wameadhirika na kuharibika. Inasikitisha sana jamani. Ninasema haya kwa kuumia sana na ninatamani Mungu angenipa uwezo wa kutamka jambo juu ya watu wenye mawazo haya kila wanapowaza washindwe kufanya yale wanayowaza juu ya kumshusha Mungu wetu na kudharau kazi ya uumbaji wake.

Shetani anafurahi sana anapoona mtu mwenye akili zako timamu unafanya ujinga na upumbavu. Shetani akishaona umefanya ujinga huo hukuacha udhalilike na kukutupa katika Recycle Bin ukafie huko na anaku-empty kabisa katika Recycle Bin yake.

Mimi nikuachie kidogo uendelee na ujinga wako huo, ila ninamuomba Mungu akufungue macho ya kuona na kutambua thamani ya mwili wako na uzuri wa mwili wako. Kila mtu ameumbwa kwa uzuri wake.

Poa, tutaona baadae katika mitikikasi mengine, ngoja nisepe nitafute riziki yangu mitaani. Mungu akubariki sana na abariki kazi ya mikono yako siku ya leo. Tuombeane ili tuwe na mafanikio na kufurahi utamu wa hapa duniani kabla hatujaona utamu wa milele huko mbinguni. Byeeeeeee

Wenu katika BWANA

Rulea Sanga wa RumaAfrica. Mkinga kutoka Makete Ugabwa. "Together We can"


"Mzungu mmoja huko majuu aliamua kujibandika ngozi nyeusi ili aonekane kama mtu weusi..kwa kuwa wadada wengii wanazimika na wanaume weusi kuliko weupe"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...