Dada kutoka Kenya ambaye ni muathirika wa UKIMWI alifika kwa Nabii Flora kwaajili ya maombezi ya uponyaji. Dada huyu alisema alivutiwa sana na ushuhuda wa Miss Kanda Mashariki Tanzania, Martha Julius ambaye alikuwa na virusi vya UKIMWI na baada ya kuhangaika sana aliweza kufika kwa Nabii Flora na akaombewa na mwisho wa siku akapona.
Dada kutoka Kenya akiwa na Nabii Flora
Kulia ni mshindi wa Miss Kanda Mashariki Tanzania Martha aliyepona UKIMWI akimfariji dada kutoka Kenya ambaye alimuona kwa kupitia facebook na akafunga safari kutoka Kenya akiwa na imani kuwa akifika kwa Nabii Flora atapata Uponyaji. Jumapili hii Nabii Flora aliweza kumuombea
Dada kutoka Kenya haamini kumuona rafiki yake aliyepona UKIMWI na yeye anatamani kupona UKIMWI na anaamini Nabii Flora kwa nguvu za Mungu atamponya
Hawa wote unawaona wameathirika wakifarijiana kwa kumkumbatia dada aliyepona virusi vya UKIMWI Martha Julius
Dada kutoka Kenya haamini kumuona rafiki yake aliyepona UKIMWI na yeye anatamani kupona UKIMWI na anaamini Nabii Flora kwa nguvu za Mungu atamponya
Hawa wote unawaona wameathirika wakifarijiana kwa kumkumbatia dada aliyepona virusi vya UKIMWI Martha Julius
EVANS KUTOKA MOSHI APONA FIGO
Bwana Yesu asifiwe, Kwa jina ninaitwa Evans nimetokea Moshi, nilikuja
kwa Nabii Flora siku ya Alhamisi nikiwa na hali mbali sana. Lakini sasa
hivi ninaona Mungu amenisaidia ninaendelea vizuri. Kipindi nakuja hapa
nilikuwa sitembei nimebebwa katika kiti. Tatizo hili nilikuwa nalo
tangia mwaka jana (2012) kutokana na figo zangu kuoza na moyo wangu
ulilika sana.
Mke wake alikuwa na haya ya kusema: Jamani mimi ninamshukuru sana nabii
Flora alivyomtendea mume wangu (baba Evans).Mnamo mwezi huu wa sita
kulekea wa saba, mdogo wake aliongozana na mume wangu kuja Dar es Salaam
kwaajili ya vipimo. Shemeji yangu akanambia ninaamini kaka yangu
atapona akifanyiwa maombi, nikamuuliza ni kanisa hgani? Akanambia wewe
twende nitakuonyesha kanisa. Nikamwambia kwasababu baba Evans anaumwa
sana ngoja tupunguze maji. Kweli mdogo wake na baba Evans akaja hapa na
mume wangu na alipofika hapa akawa ni mtu wa 19 kwa wale wanaotakiwa
kumuona nabii Flora.
Tulipofika hapa kanisani, baba Evans alisumbua sana, alikuwa haoni, hana
nguvu ni mtu wa kushikiria. Tilipofika Nabii akasema wenye matatizo
wapiti mbele ili waombewe hasa wafanyakazi (na sisi tukajichanganya humo
humo). Tukamkarisha baba Evans katika kiti. Nabii Flora aliposogea
tukamnyanyua. Nabii Flora akamshika mkono na akamuombea. Baada ya
kumaliza kumuombea akamwambia, “Nimekwambia tembea’’ Mara tukaona baba
Evans anatembea taratibu taratibu na jinsi anavyoendelea kutembea,
mabadiliko yanatokea na kuwa mazuri.
Ulipofika wakatii wa kumuona nabii Flora, watu walitupisha na tukaonana
naye. Nabii alipomuona akasema huyu mtu ameoza ini, ameoza figo na moyo,
kwahiyo anatakiwa abomolewe. Nabii akamuombea kwa danu ya Yesu. Jana
tulienda kupima hospitalini, kwa kweli mambo ni mazuri sana. Nabii Flora
ametusaidia bila ya malipo yoyote. Sina kitu cha kukurudishia Nabii
Flora ila Mungu ataendelea kukulinda
MAJI YA UPAKO YAVUTA KILIO CHA GETRUDE BAADA YA WANAE KUTESWA NA WAPANGAJI.
Bwana Yesu apewe sifa, mimi ninaitwa Getrude Gelvasi Magingo, ninakaa
Mbagala Dar es Salaam Tanzania. Mwezi wa 9 mwaka 2013 nilihamia kwenye
nyumba ambapo nilipata matatizo makubwa sana. Baba mwenye nyumba ambaye
anakaa mkoa wa Mtwara alikuwa akilalamika na kodi ya wapangaji amabao
walikuwa hawalipi nay eye anategemea hiyo kodi kuendesha maisha yake..
Kipindi anazungumza hayo mimi nilikuwa nimesafiri. Wapangaji wenzangu
wakawa wanawambia wale wanangu kuhusu kodi, wakawa wanawapiga na
kuwamwagia chakula.
Nilipopigiwa simu jinsi wanangu wanavyoteseka ilibidi nirudi na
nilipofika Ubungo, Dar es Salaam nikaja moja kwa moja kanisani kwa nabii
Flora, nikalala na asubuhi ilipofika Nabii Flora aliombea maji yangu.
Nilienda nyumbani na nilipofika wanangu wakanieleza matatizo
yaliyotokea. Mungu akasikia kilio change, wale wapangaji wawili
waliokuwa wakisumbua familia yangu juzi wamehama.
Muda si mrefu nikapata simu kutoka kwa mwenye nyumba kuwa anahitaji
nimpeleke kwa nabii Flora ili amuombee kwani ana matatizo yanayomsumbua.
Ninamshukuru sana Nabii Flora.
KIJANA KUTOKA MWANZA APONA KANSA NA BABA YAKE MKUBWA, PROFESA MOROGORO APONA UPOFU
Bwana Yesu asifiwe, mimi ninatokea Mwanza Bugando na jina langu ni
Edstamus Thomas na ni mwanafunzi kidato cga sita. Nilikuwa na tatizo la
jicho la kansa tokea nimezaliwa. Nilienda kupima Bugando wakanambia ni
kansa. Nikaambiwa matibabu ya kansa yanapatikana katika hospitali Ocean
Road Dar es Salaam kwa njia ya mionzi. Tuliandikiwa referal letter
Mwanza kuwa twende Dar es Salaam.
Tulipofika Dar es Salaam, ilibidi tuanzie Muhimbili katika hospitali ya
Rufaa. Madaktari Muhimbili waliangalia jicho langu na kuniambia niende
baada ya wiki mbili. Mama akanambia twende kwenye maombi kwa Nabii
Flora, kwa muda wa wiki mbili hizi Mungu atatenda.
Nilipofika hapa kanisani nilionana na Nabii Flora na akanambia nitapona.
Na ukumbuke hospitalini walinambia ninatakiwa kufanyiwa operation ya
kuondoa jicho. Basi tukawa tunakuja hapa kanisani na baba mkubwa ambaye
ni profesa Morogoro ambaye alikuwa na tatizo la kutoona (kipofu).
Alipokuwa akihudhuriwa maombi aliweza kupona na sasa anaona. Na mimi
nimeweza kupokea uponyaji nimeambiwa sina kansa kabisa.
Mama wa huyu kijana alikuwa na haya ya kusema: Baada ya wiki mbili
kuishi tukaenda tena hospitalini na wakatuambia maendeleo ni mazuri na
tuendelea kutumia dawa ndani ya wiki moja. Wiki moja ikiwa bado
haijaisha tukawa tumepigiwa simu kwamba, aende wakaamwangalie tena
hospitalini ili wapate ufumbuzi ili arudi shuleni. Ndipo tukaamua kuja
kwa nabii Flora na kuweza kumuombea, na baada ya kumuombea na kufuta
jicho la mwanangu kwa kitambaa na kurudisha jicho ndani. Tulipoenda siku
ya Ijumaa, madakatari wakamwamngalia wakasema, hii sio kansa ila ni
tatizo linguine, kwahiyo inabidi tuendelee kwa miezi mitatu, baada ya
hiyo miezi mitatu kuisha turudi hospitalini na kuangalia maendeleo yake
na ndipo tutakapowaruhusu.
ALISHA MUSA ALIYEPONA UKIMWI YEYE NA MWANAE NA MUME WAKE AMSHUKURU NABII FLORA KWA MAENDELEO MAZURI YA MAMA YAKE ANAYEUMWA.
Bwana asifiwe. Kwa jina ninaitwa Alisha Musa, Mungu amenitendea mengi
sana. Nilikuwa na HIV nilipona kwa kupitia Nabii Flora. Kuna jambo
ambalo sitasahau ambalo Nabii Flora alilisema ya kwamba, “Tuchukue
kitambaa cheupe” nilichukua kile kitambaa na sikujua kuwa mama yangu
ataumwa. Niliondoka na vile vitambaa viwili, kimoja nikampa mwanangu na
kimoja nikawa nacho. Baada ya wiki moja nikapigiwa simu na kuniambia
mama yako anaumwa sana na amelazwa hospitali. Nikamwambia mama yangu
utapona na mimi niko njia ninakuja huko Moshi. Nilipofika nikakuta mama
yangu anakula kwa kutumia mpira na kukojoa kwa kutumia mpira. Nikachukua
maji niliyoondoka nayo hapa kanisani na nikampapasa nayo usoni.
Nilimpigia Nabii Flora na akaniombea. Mama yangu alikuwa anakoroma tu,
ana ameteseka kwa muda wa wiki mbili. Nikasema “Eh Mungu wa nabii Flora,
ninaamini, kama mimi nilipona UKIMWI na mtoto wangu na mume wangu,
basin a mama yangu hatakoroma tena”. Mama yangu ikabidi wampeleke
hospitali nyingine na alipofika kule wakasema mama huyu hana ugonjwa
wowote. Tukaondoka na kumpeleka KCMC, na pale hakuweza kupokea uponyaji
wake. Mama yangu ikabidi arudishwe nyumbani. Nikampigia simu Nabii Flora
na nikamwambia mama yangu anaongea lakini anaongea kwa shida sana. Na
mpaka sasa ninaongea mandeleo yake ni mazuri lakini mkono wake mmoja
haufanyi kazi.
BIBI SILVIA MBUYA AMSHUKURU MUNGU KWA MWANAE KUJIFUNGU SALAMA
Bwana Yesu asifiwe. Ninaitwa silvia Mbuya. Ninashukuru sana madhabahu
hii ya Nabii Flora. Nilimpigia simu mwanangu alikuwa na mimba ambayo
imepitiliza siku zake na kufikia miezi 10. Ilibidi afanyiwe oparesheni
na bahati nzuri Mungu akaona hilo na hawajaweza kumfanyia operation na
amejifungua salama.
Mwanangu tangia amejifungua amelazwa hospitali Muhimbili kwa muda wa wiki moja sasa. Ninamshukuru Mungu anaendelea vizuri sana.
Pia eneo ninalokaa nimezungukwa na wachawi na watoto wangu wanalia sana usiku, na mimi ninaota ndoto mbaya sana.
Ninakushuru sana Nabii Flora
DADA AMBAYE ALIFNGWA KIMASOMO AKITAMANI KWENDA KUSOMA ULAYA, NDOTO YAKE YATIMIA
Bwana Yesu asifiwe, kwa jina ninaitwa Samason, nilikuja hapa kanisani,
nikaonana na Nabii Flora Peter nikamwambia ninataka kwenda Ulaya na chuo
maendeleo yangu sio mazuri. Akanambia Ulaya utaenda na ninakuona
umefungwa. Baada ya kununifanyia deliverance, nilipofika chuo nikawa
ninaendelea vizuri, nimemaliza masomo yangu salama, na nimepata chuo
ninaenda Hungary. Ninamshukuru sana Nabii Flora.
MWANAFUNZI APONA ALEJI ILIYOMSABABISHIA KUSHINDWA KUFIKA SHULE, SASA ASHIKA NAMBA MOJA DARASANI
Bwana Yesu asifiwe, kwa jina ninaitwa Maolela. Ninamshukuru Mungu wa
nabii Flora ameniponya. Nilikuwa nasumbuliwa na aleji upele kwa muda wa
miaka mitatu hata shule nilikuwa ninashindwa kwenda. Wanafunzi wenzangu
wakawa wananicheka wakisema labda nina UKIMWI. Wazazi wangu wote
walifariki. Lakini nilipofika mahali hapa Mungu ameniponya, na sasa
ninaendelea vizuri na masomo, ninafaulu vizuri sana, ninamshukuru sana
Mungu wa Nabii Flora kwani hata namba moja ninashika darasani.
VUMI APONA UVIMBE WA TITI, AOKOTA FEDHA MPAKA KUFIKIA TSH. 50,000
Kwa jina ninaitwa Vumi Lamson Kahama. Mimi ninapenda kumshukuru Mungu wa
Nabii Flora. Jumapili iliyopita nilikuwa nasumbuliwa na ziwa langu,
nilivimba sana kupita maelezo (jipu), nilishindwa hata kushika mtoto na
waumini walikuwa wakinisaidia kushika mtoto. Baada ya ibada nikaonana na
Nabii Flora akaweza kulishika ziwa langu na kuliombea, akasema ikifika
saa 12 jioni ninaamuru uvimbe huu na uishe. Ilipofika saa 12 niliweza
kumshika mtoto na zuwa likapungua uvimbe, likabaki na uvimbe kidogo.
Siku ya Jumatano nikaja na kumueleza tena nabii Flora, akashika titi
langu na akasema ninaamuru hili buya lote liishe na uishi kwa amani.
Ninamshukuru sana Mungu wa Nabii Flora amenitendea miuujiza.
Muujiza wa pili: Jamani tangia nije katika kanisa hili ni mwezi wa 6.
Jumapili ya kwanza nikasali mahali hapa, Jumapili ya pili nilipokuja
hapa nabii Flora alikuwa akifundisha jinsi ya kupokea mwezi wa Eludi
(6). Nabii Flora akaombea maji yangu, nilipotoka hapa nikasema sifiki
nyumbani lazima nifike katika Showbiz yangu nimwagie maji. Baada ya
kumwagia maji. Baada ya hapoa niakapanga vitnavyotakiwa kupangwa na
nikaacha kijana wangu akiendelea na kazi. Nilipotoka hapoa nikaanza
kuokota fedha, nikaokota 500, 1000, 5000, 10000 mpaka zikafika 50,000/=
Kwa kweli nilitetemeka sana nilishindwa kuelewa, nilijua ni Mungu wa
Nabii Flora ndiye anayeonyesha miujiza hii. Hakika Mungu wa nabii Flora
anaweza.
MAMA MZAZI WA MARY SHEMILA AWEZA KUTEMBEA MUHIMBILI ALIKOLAZWA
Bwana Yesu asifiwe, kwa jina jninaitwa Mary shemila, nimesimama hapa kwa
niaba ya mama yangu Mary shemila ambaye amelazwa katika hospitali ya
Muhimbili Dar es Salaam toka tarehe 8. Jumapili iliyopita nilikuja hapa
nikamuona mtumishi wa Mungu Nabii Flora. Mama yangu alikuwa hawezi
kutembea kabisa. Lakini baada ya mtumishi Nabii Flora kumuombea, mama
yangu aliweza kutembea.
Nabii Flora alituomba katikati ya wiki tumlete mama yetu, lakini
masharti ya pale Muhimbili ni magumu sana, hatukuweza kupata nafasi ya
kumleta. Sasa leo tumeweza kupata nafasi na tumemleta tena mama yetu ili
Nabii Flora akaweze kumuona tena. Asante Mungu.
ROBERT AFUNGULIWA MAJINI ALIYOTUPIWA. YEYE NA UKOO MZIMA
Mimi ninaitwa Robert Mwaipoa, ni mwenyeji wa Mbeya ila kwa sasa ninaishi
Bunju. Mimi nilitupiwa nguvu za kishirikina katika ukoo. Tulikuwa na
majini na vifaa vya aina mbalimbali. Nimezunguka mapaka nikaenda kwa
waganga.
Nilipokutana na mpendwa mmoja akanambia unahangaika nini, yupo mganga wa
waganga katika kanisa la Yesu Kristo kwa nabii Flora. Nikamwambia
unicholee ramani na mimi nitafika mwenyewe. Nilipoelekezwa nikawa
nimekosea kidogo na kuingia kanisani moja jirani na hili. Baada ya
kupotea nikachukua pikipiki na kufika hapa kwa nabii Flora nikajua hapa
upo uponyaji.
Ulipofika wakati wa kuombewa, niliombewa na baada ya hapo nikajisikia
nimefunguliwa. Ulipofika wakati wa kumuona Nabii Flora kesho yake jioni,
akasema hilo tatizo lako ni dogo, lete maji yaombewe. Nilipokunywa yale
maji nilitapika sana. Baada ya kuona hayo ndio maana leo nimekuja kwa
ushindi mkubwa wa uponyaji.
DADA ALIYEVUNJIKA MKONO BAADA YA MAOMBEZI MKONO UMEPONA
Bwana Yesu asifiwe, mimi nilikuja juzi mkono wangu ilikuwa umevunjika,
baada ya kufika hapa mkono wangu umepona. Mkono wangu ulikuwa umefungwa
bandeji
R.WILSON KALEBELWA ALIYEKUWA AKIFELI MITIHANI APATA MUUJIZA WA KWENDA CHUONI KUSOMA
Bwana asifiwe, kwa jina ninaitwa R. Wilson Kalebelwa, ninamshukuru Mungu
wa madhabahu hii amenifungua. Nilikuwa mwanafunzi niliyekata tamaa
kutokana na kufeli sana kimasomo. Lakini kwa kupitia madhabahu hii ya
Nabii Fllora, Mungu amenifungua nimemaliza shule, na majibu yangu
nimepata na ilibidi niondoke leo kuelekea chuoni. Mtumishi Nabii Flora
alisema nisiondoke leo bali ondoka kesho Jumatatu. Ninamshukuru sana
Mungu.
DADA APONA UKIMWI BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA PETER
MAMA NA MWANAE WAPONA UKIMWI BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA PETER
DADA APONA UKIMWI BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA PETER
DADA APATA MUUJIZA WA KUJENGA NYUMBA BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA PETER
BABA APONA KISUKARI BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA PETER