Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Ijumaa, 12 Julai 2013

WANAWAKE WATUMISHI WA KIKRISTO (WWW) MBALIZI WATOA PIKIPIKI KWA WAANGALIZI


Wanawake Watumishi wa Kristo (WWK), Sehemu ya Mbalizi, wiki iliyopita ilitoa zawadi ya usafiri wa pikipiki kwa viongozi waangalizi wa sehemu hiyo, ili kuiwezesha kazi ya Mungu kusonga mbele zaidi pasipo kukwama kwa namna yoyote ile.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, katika kongamano la siku mbili la WWK Sehemu ya Mbalizi, Mkurugenzi wa wanawake hao, Sevelina Mwasile alisema kuwa, wao kama wanawake wa kanisa la TAG wameona watoe vyombo hivyo vya usafuri ili kuondoa usumbufu kufika wasikoweza kirahisi.

Aidha Bi. Sevelina alisema, viongozi hao wamekuwa wakitumia baiskeli kwa muda mrefu na wakati mwingine walikuwa wakitembea kwa mguu kwenda kuifanya kazi ya Mungu mbali, jammbo ambalo limekwamisha kazi ya Mungu kwa kiwango kikubwa.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa, miongoni mwa zawadi walizojadili, walifikia muafaka wa kununua Pikipiki tatu ili kila kiongozi apate usafiri wake kuliko kununua gari moja ambayo kila mmoja atakuwa akiitegemea.

Kiongozi huyo wa wanawake, aliwataja viongozi waliopewa zawadi hizo kuwa ni pamoja na ; Watson Mwanjoka, ambaye ni Mwangalizi wa Sehemu ya Mbalizi, Eliya Mukuku, Makamu Mwangalizi na Furahisha Ngofyela, katibu Mbalizi.

Akishukuru kwa tukio lililofanywa na wanawake hao, Mwangalizi Mwanjoka alisema ameshangazwa na kitendo kilichofanywa na wanawake hao kwani hakutengemea kupata usafiri.

Mwangalizi huyo alisema kuwa, wanawake hao wamekatisha kilio chake cha muda mrefu, huku akiweka wazi kuwa, kazi ya Mungu inahitaji uharaka ili kuiendeleza.

Naye Makamu Mwangalizi wa Sehemu hiyo, Mchungaji Eliya Bukuku, alisema wametembea kwa baiskel kwa muda mrefu hata kufika hatua ya kuchoka, lakini Mungu amejifunua kwa kuwahurumia kupitia wanawake hao.

Alitoa wito kwa Wakristo kuwaombea kwa bidii wanawake ili Mungu ayatumia maono waliyo nayo katika kazi yake.

Mbali na kutoa zawadi kwa Viongozi wao, WWK Sehemu ya Mbalizi walichangisha zaidi ya milioni nne kujenga vibanda vya kufanyia biashara, ili kutunisha mfuko ndani ya mji huo mdogo wa Mbalizi.

Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi wa WWK Mbalizi, Bi. Mwasile alisema, kujengwa kwa vibanda hivyo, vya biashara vitasaidia kuongeza pesa na michango ya akina mama itapungua kwani mara baada ya vibanda hivyo kukamilika vitapangishwa na kodi zitakazo lipwa zitaingizwa moja kwa moja kwenye mfuko wa akina mama.

Alisema maono yao ni kupata milioni 50 kwaajili ya ujenzi na vibanda hivyo, ili kukamilisha ujenzi katikati mji huo wa Mbalizi unaosifika kibiashara mkoani Mbeya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...