Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Jumanne, 23 Julai 2013

SHUHUDA ZA JUMAPILI YA 21.07.2013 KATIKA KANISA LA YESU KRISTO LA HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI

Dada kutoka Kenya ambaye ni muathirika wa UKIMWI alifika kwa Nabii Flora kwaajili ya maombezi ya uponyaji. Dada huyu alisema alivutiwa sana na ushuhuda wa Miss Kanda Mashariki Tanzania, Martha Julius ambaye alikuwa na virusi vya UKIMWI na baada ya kuhangaika sana aliweza kufika kwa Nabii Flora na akaombewa na mwisho wa siku akapona.


Dada kutoka Kenya akiwa na Nabii Flora
 Kulia ni mshindi wa Miss Kanda Mashariki Tanzania Martha aliyepona UKIMWI akimfariji dada kutoka Kenya ambaye alimuona kwa kupitia facebook na akafunga safari kutoka Kenya akiwa na imani kuwa akifika kwa Nabii Flora atapata Uponyaji. Jumapili hii Nabii Flora aliweza kumuombea
 Dada kutoka Kenya haamini kumuona rafiki yake aliyepona UKIMWI na yeye anatamani kupona UKIMWI na anaamini Nabii Flora kwa nguvu za Mungu atamponya
Hawa wote unawaona wameathirika wakifarijiana kwa kumkumbatia dada aliyepona virusi vya UKIMWI Martha Julius
EVANS KUTOKA MOSHI APONA FIGO
Bwana Yesu asifiwe, Kwa jina ninaitwa Evans nimetokea Moshi, nilikuja kwa Nabii Flora siku ya Alhamisi nikiwa na hali mbali sana. Lakini sasa hivi ninaona Mungu amenisaidia ninaendelea vizuri. Kipindi nakuja hapa nilikuwa sitembei nimebebwa katika kiti. Tatizo hili nilikuwa nalo tangia mwaka jana (2012) kutokana na figo zangu kuoza na moyo wangu ulilika sana.
Mke wake alikuwa na haya ya kusema: Jamani mimi ninamshukuru sana nabii Flora alivyomtendea mume wangu (baba Evans).Mnamo mwezi huu wa sita kulekea wa saba, mdogo wake aliongozana na mume wangu kuja Dar es Salaam kwaajili ya vipimo. Shemeji yangu akanambia ninaamini kaka yangu atapona akifanyiwa maombi, nikamuuliza ni kanisa hgani? Akanambia wewe twende nitakuonyesha kanisa. Nikamwambia kwasababu baba Evans anaumwa sana ngoja tupunguze maji. Kweli mdogo wake na baba Evans akaja hapa na mume wangu na alipofika hapa akawa ni mtu wa 19 kwa wale wanaotakiwa kumuona nabii Flora.
Tulipofika hapa kanisani, baba Evans alisumbua sana, alikuwa haoni, hana nguvu ni mtu wa kushikiria. Tilipofika Nabii akasema wenye matatizo wapiti mbele ili waombewe hasa wafanyakazi (na sisi tukajichanganya humo humo). Tukamkarisha baba Evans katika kiti. Nabii Flora aliposogea tukamnyanyua. Nabii Flora akamshika mkono na akamuombea. Baada ya kumaliza kumuombea akamwambia, “Nimekwambia tembea’’ Mara tukaona baba Evans anatembea taratibu taratibu na jinsi anavyoendelea kutembea, mabadiliko yanatokea na kuwa mazuri.
Ulipofika wakatii wa kumuona nabii Flora, watu walitupisha na tukaonana naye. Nabii alipomuona akasema huyu mtu ameoza ini, ameoza figo na moyo, kwahiyo anatakiwa abomolewe. Nabii akamuombea kwa danu ya Yesu. Jana tulienda kupima hospitalini, kwa kweli mambo ni mazuri sana. Nabii Flora ametusaidia bila ya malipo yoyote. Sina kitu cha kukurudishia Nabii Flora ila Mungu ataendelea kukulinda
MAJI YA UPAKO YAVUTA KILIO CHA GETRUDE BAADA YA WANAE KUTESWA NA WAPANGAJI.
Bwana Yesu apewe sifa, mimi ninaitwa Getrude Gelvasi Magingo, ninakaa Mbagala Dar es Salaam Tanzania. Mwezi wa 9 mwaka 2013 nilihamia kwenye nyumba ambapo nilipata matatizo makubwa sana. Baba mwenye nyumba ambaye anakaa mkoa wa Mtwara alikuwa akilalamika na kodi ya wapangaji amabao walikuwa hawalipi nay eye anategemea hiyo kodi kuendesha maisha yake.. Kipindi anazungumza hayo mimi nilikuwa nimesafiri. Wapangaji wenzangu wakawa wanawambia wale wanangu kuhusu kodi, wakawa wanawapiga na kuwamwagia chakula.
Nilipopigiwa simu jinsi wanangu wanavyoteseka ilibidi nirudi na nilipofika Ubungo, Dar es Salaam nikaja moja kwa moja kanisani kwa nabii Flora, nikalala na asubuhi ilipofika Nabii Flora aliombea maji yangu. Nilienda nyumbani na nilipofika wanangu wakanieleza matatizo yaliyotokea. Mungu akasikia kilio change, wale wapangaji wawili waliokuwa wakisumbua familia yangu juzi wamehama.
Muda si mrefu nikapata simu kutoka kwa mwenye nyumba kuwa anahitaji nimpeleke kwa nabii Flora ili amuombee kwani ana matatizo yanayomsumbua.
Ninamshukuru sana Nabii Flora.
KIJANA KUTOKA MWANZA APONA KANSA NA BABA YAKE MKUBWA, PROFESA MOROGORO APONA UPOFU
Bwana Yesu asifiwe, mimi ninatokea Mwanza Bugando na jina langu ni Edstamus Thomas na ni mwanafunzi kidato cga sita. Nilikuwa na tatizo la jicho la kansa tokea nimezaliwa. Nilienda kupima Bugando wakanambia ni kansa. Nikaambiwa matibabu ya kansa yanapatikana katika hospitali Ocean Road Dar es Salaam kwa njia ya mionzi. Tuliandikiwa referal letter Mwanza kuwa twende Dar es Salaam.
Tulipofika Dar es Salaam, ilibidi tuanzie Muhimbili katika hospitali ya Rufaa. Madaktari Muhimbili waliangalia jicho langu na kuniambia niende baada ya wiki mbili. Mama akanambia twende kwenye maombi kwa Nabii Flora, kwa muda wa wiki mbili hizi Mungu atatenda.
Nilipofika hapa kanisani nilionana na Nabii Flora na akanambia nitapona. Na ukumbuke hospitalini walinambia ninatakiwa kufanyiwa operation ya kuondoa jicho. Basi tukawa tunakuja hapa kanisani na baba mkubwa ambaye ni profesa Morogoro ambaye alikuwa na tatizo la kutoona (kipofu). Alipokuwa akihudhuriwa maombi aliweza kupona na sasa anaona. Na mimi nimeweza kupokea uponyaji nimeambiwa sina kansa kabisa.
Mama wa huyu kijana alikuwa na haya ya kusema: Baada ya wiki mbili kuishi tukaenda tena hospitalini na wakatuambia maendeleo ni mazuri na tuendelea kutumia dawa ndani ya wiki moja. Wiki moja ikiwa bado haijaisha tukawa tumepigiwa simu kwamba, aende wakaamwangalie tena hospitalini ili wapate ufumbuzi ili arudi shuleni. Ndipo tukaamua kuja kwa nabii Flora na kuweza kumuombea, na baada ya kumuombea na kufuta jicho la mwanangu kwa kitambaa na kurudisha jicho ndani. Tulipoenda siku ya Ijumaa, madakatari wakamwamngalia wakasema, hii sio kansa ila ni tatizo linguine, kwahiyo inabidi tuendelee kwa miezi mitatu, baada ya hiyo miezi mitatu kuisha turudi hospitalini na kuangalia maendeleo yake na ndipo tutakapowaruhusu.
ALISHA MUSA ALIYEPONA UKIMWI YEYE NA MWANAE NA MUME WAKE AMSHUKURU NABII FLORA KWA MAENDELEO MAZURI YA MAMA YAKE ANAYEUMWA.
Bwana asifiwe. Kwa jina ninaitwa Alisha Musa, Mungu amenitendea mengi sana. Nilikuwa na HIV nilipona kwa kupitia Nabii Flora. Kuna jambo ambalo sitasahau ambalo Nabii Flora alilisema ya kwamba, “Tuchukue kitambaa cheupe” nilichukua kile kitambaa na sikujua kuwa mama yangu ataumwa. Niliondoka na vile vitambaa viwili, kimoja nikampa mwanangu na kimoja nikawa nacho. Baada ya wiki moja nikapigiwa simu na kuniambia mama yako anaumwa sana na amelazwa hospitali. Nikamwambia mama yangu utapona na mimi niko njia ninakuja huko Moshi. Nilipofika nikakuta mama yangu anakula kwa kutumia mpira na kukojoa kwa kutumia mpira. Nikachukua maji niliyoondoka nayo hapa kanisani na nikampapasa nayo usoni. Nilimpigia Nabii Flora na akaniombea. Mama yangu alikuwa anakoroma tu, ana ameteseka kwa muda wa wiki mbili. Nikasema “Eh Mungu wa nabii Flora, ninaamini, kama mimi nilipona UKIMWI na mtoto wangu na mume wangu, basin a mama yangu hatakoroma tena”. Mama yangu ikabidi wampeleke hospitali nyingine na alipofika kule wakasema mama huyu hana ugonjwa wowote. Tukaondoka na kumpeleka KCMC, na pale hakuweza kupokea uponyaji wake. Mama yangu ikabidi arudishwe nyumbani. Nikampigia simu Nabii Flora na nikamwambia mama yangu anaongea lakini anaongea kwa shida sana. Na mpaka sasa ninaongea mandeleo yake ni mazuri lakini mkono wake mmoja haufanyi kazi.
BIBI SILVIA MBUYA AMSHUKURU MUNGU KWA MWANAE KUJIFUNGU SALAMA
Bwana Yesu asifiwe. Ninaitwa silvia Mbuya. Ninashukuru sana madhabahu hii ya Nabii Flora. Nilimpigia simu mwanangu alikuwa na mimba ambayo imepitiliza siku zake na kufikia miezi 10. Ilibidi afanyiwe oparesheni na bahati nzuri Mungu akaona hilo na hawajaweza kumfanyia operation na amejifungua salama.
Mwanangu tangia amejifungua amelazwa hospitali Muhimbili kwa muda wa wiki moja sasa. Ninamshukuru Mungu anaendelea vizuri sana.
Pia eneo ninalokaa nimezungukwa na wachawi na watoto wangu wanalia sana usiku, na mimi ninaota ndoto mbaya sana.
Ninakushuru sana Nabii Flora
DADA AMBAYE ALIFNGWA KIMASOMO AKITAMANI KWENDA KUSOMA ULAYA, NDOTO YAKE YATIMIA
Bwana Yesu asifiwe, kwa jina ninaitwa Samason, nilikuja hapa kanisani, nikaonana na Nabii Flora Peter nikamwambia ninataka kwenda Ulaya na chuo maendeleo yangu sio mazuri. Akanambia Ulaya utaenda na ninakuona umefungwa. Baada ya kununifanyia deliverance, nilipofika chuo nikawa ninaendelea vizuri, nimemaliza masomo yangu salama, na nimepata chuo ninaenda Hungary. Ninamshukuru sana Nabii Flora.
MWANAFUNZI APONA ALEJI ILIYOMSABABISHIA KUSHINDWA KUFIKA SHULE, SASA ASHIKA NAMBA MOJA DARASANI
Bwana Yesu asifiwe, kwa jina ninaitwa Maolela. Ninamshukuru Mungu wa nabii Flora ameniponya. Nilikuwa nasumbuliwa na aleji upele kwa muda wa miaka mitatu hata shule nilikuwa ninashindwa kwenda. Wanafunzi wenzangu wakawa wananicheka wakisema labda nina UKIMWI. Wazazi wangu wote walifariki. Lakini nilipofika mahali hapa Mungu ameniponya, na sasa ninaendelea vizuri na masomo, ninafaulu vizuri sana, ninamshukuru sana Mungu wa Nabii Flora kwani hata namba moja ninashika darasani.
VUMI APONA UVIMBE WA TITI, AOKOTA FEDHA MPAKA KUFIKIA TSH. 50,000
Kwa jina ninaitwa Vumi Lamson Kahama. Mimi ninapenda kumshukuru Mungu wa Nabii Flora. Jumapili iliyopita nilikuwa nasumbuliwa na ziwa langu, nilivimba sana kupita maelezo (jipu), nilishindwa hata kushika mtoto na waumini walikuwa wakinisaidia kushika mtoto. Baada ya ibada nikaonana na Nabii Flora akaweza kulishika ziwa langu na kuliombea, akasema ikifika saa 12 jioni ninaamuru uvimbe huu na uishe. Ilipofika saa 12 niliweza kumshika mtoto na zuwa likapungua uvimbe, likabaki na uvimbe kidogo. Siku ya Jumatano nikaja na kumueleza tena nabii Flora, akashika titi langu na akasema ninaamuru hili buya lote liishe na uishi kwa amani.
Ninamshukuru sana Mungu wa Nabii Flora amenitendea miuujiza.
Muujiza wa pili: Jamani tangia nije katika kanisa hili ni mwezi wa 6. Jumapili ya kwanza nikasali mahali hapa, Jumapili ya pili nilipokuja hapa nabii Flora alikuwa akifundisha jinsi ya kupokea mwezi wa Eludi (6). Nabii Flora akaombea maji yangu, nilipotoka hapa nikasema sifiki nyumbani lazima nifike katika Showbiz yangu nimwagie maji. Baada ya kumwagia maji. Baada ya hapoa niakapanga vitnavyotakiwa kupangwa na nikaacha kijana wangu akiendelea na kazi. Nilipotoka hapoa nikaanza kuokota fedha, nikaokota 500, 1000, 5000, 10000 mpaka zikafika 50,000/= Kwa kweli nilitetemeka sana nilishindwa kuelewa, nilijua ni Mungu wa Nabii Flora ndiye anayeonyesha miujiza hii. Hakika Mungu wa nabii Flora anaweza.
MAMA MZAZI WA MARY SHEMILA AWEZA KUTEMBEA MUHIMBILI ALIKOLAZWA
Bwana Yesu asifiwe, kwa jina jninaitwa Mary shemila, nimesimama hapa kwa niaba ya mama yangu Mary shemila ambaye amelazwa katika hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam toka tarehe 8. Jumapili iliyopita nilikuja hapa nikamuona mtumishi wa Mungu Nabii Flora. Mama yangu alikuwa hawezi kutembea kabisa. Lakini baada ya mtumishi Nabii Flora kumuombea, mama yangu aliweza kutembea.
Nabii Flora alituomba katikati ya wiki tumlete mama yetu, lakini masharti ya pale Muhimbili ni magumu sana, hatukuweza kupata nafasi ya kumleta. Sasa leo tumeweza kupata nafasi na tumemleta tena mama yetu ili Nabii Flora akaweze kumuona tena. Asante Mungu.
ROBERT AFUNGULIWA MAJINI ALIYOTUPIWA. YEYE NA UKOO MZIMA
Mimi ninaitwa Robert Mwaipoa, ni mwenyeji wa Mbeya ila kwa sasa ninaishi Bunju. Mimi nilitupiwa nguvu za kishirikina katika ukoo. Tulikuwa na majini na vifaa vya aina mbalimbali. Nimezunguka mapaka nikaenda kwa waganga.
Nilipokutana na mpendwa mmoja akanambia unahangaika nini, yupo mganga wa waganga katika kanisa la Yesu Kristo kwa nabii Flora. Nikamwambia unicholee ramani na mimi nitafika mwenyewe. Nilipoelekezwa nikawa nimekosea kidogo na kuingia kanisani moja jirani na hili. Baada ya kupotea nikachukua pikipiki na kufika hapa kwa nabii Flora nikajua hapa upo uponyaji.
Ulipofika wakati wa kuombewa, niliombewa na baada ya hapo nikajisikia nimefunguliwa. Ulipofika wakati wa kumuona Nabii Flora kesho yake jioni, akasema hilo tatizo lako ni dogo, lete maji yaombewe. Nilipokunywa yale maji nilitapika sana. Baada ya kuona hayo ndio maana leo nimekuja kwa ushindi mkubwa wa uponyaji.
DADA ALIYEVUNJIKA MKONO BAADA YA MAOMBEZI MKONO UMEPONA
Bwana Yesu asifiwe, mimi nilikuja juzi mkono wangu ilikuwa umevunjika, baada ya kufika hapa mkono wangu umepona. Mkono wangu ulikuwa umefungwa bandeji
R.WILSON KALEBELWA ALIYEKUWA AKIFELI MITIHANI APATA MUUJIZA WA KWENDA CHUONI KUSOMA
Bwana asifiwe, kwa jina ninaitwa R. Wilson Kalebelwa, ninamshukuru Mungu wa madhabahu hii amenifungua. Nilikuwa mwanafunzi niliyekata tamaa kutokana na kufeli sana kimasomo. Lakini kwa kupitia madhabahu hii ya Nabii Fllora, Mungu amenifungua nimemaliza shule, na majibu yangu nimepata na ilibidi niondoke leo kuelekea chuoni. Mtumishi Nabii Flora alisema nisiondoke leo bali ondoka kesho Jumatatu. Ninamshukuru sana Mungu.
DADA  APONA UKIMWI BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA PETER


MAMA NA MWANAE WAPONA UKIMWI BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA PETER


DADA APONA UKIMWI BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA PETER

DADA APATA MUUJIZA WA KUJENGA NYUMBA BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA PETER

BABA APONA KISUKARI BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA PETER

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...