Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Jumatatu, 15 Julai 2013

UPENDO BENSON: NINI KINATOKEA UKIMPOKEA YESU KRISTO NDANI YAKO?



Ukishampokea Yesu ndani yako, manaake siri zote za moyoni mwako shetani anakua hazijui, na anakua hajui akutege vipi maana hajui umejidhatitije.. ila anakaa kusubiri maneno yanayotoka kinywani mwako ndo ayafanyie kazi.. manaake ukiongea maneno ya kukata tamaa na kushindwa anayachukua na kuyafanyia kazi ipasavyo ili uzidi kukata tamaa na kushindwa.. lakini unapotamka maneno ya ushindi na kujipa moyo, unapotamka maneno ya kumtukuza aliye ndani mwako(Yesu), unazidi kuwa tishio kwa shetani.. CHUNGA SANA KINYWA CHAKO, ILI KISIMPE ADUI MUONGOZO WA KUKUMALIZA. Kumbuka, kinywa chako ndicho kinachofunga au kufungua lolote(Matthew 18:18) ukisema unamikosi, utaletewa mikosi, ukisema wewe ni wa kushindwa tu.. utaletewa kushindwa, ukisema umebarikiwa baraka zitakufuata nk.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...