Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Jumatatu, 15 Julai 2013

PADRI ALIYESHAMBULIWA IRINGA KURUDI KWAO, KUAGWA ALHAMISI DSM


Padri Angelo Burgeo wa kanisa Katoliki Parokia ya Isimani, Iringa.
Hatimaye baada ya kupota kutokana na majeraha ya kushambuliwa usiku wa kuamkia tarehe 16 Novemba 2012 akiwa kwenye eneo lake la kazi, Padri Angelo Burgeo anatarajia kuagwa rasmi kwa utumishi wake nchini, na kurejea kwao, Italia (Italy).
Padri Angelo alikuwa nchini Italia kwa matibabu zaidi, kutokana na kushambuliwa kwa silaha na kuporwa pesa kiasi cha zaidi ya milioni 2.5 kwenye kanisa Katoliki Parokia ya Isimani mkoani Iringa, habari ya kushwambuliwa huko iliripotiwa na Gospel Kitaa kwa mara ya kwanza na kisha habari mwendelezo zikafuata kwenye vyombo vingine vya habari siku iliyofuatia.
Wana Isimani leo hii walipata nafasi ya kumuaga padri huyo anayesemakan kuwepo nchini kutokea kwao kwa matibabu kwa takribani wiki 2 sasa, ambaye baada ya kuhudumu kwa takriban miaka 30, hatimaye anarejea kwao Italia, ambako ataendelea na huduma. Kwa mujibu wa taarifa ambayo Gospel Kitaa imeipata, kutakuwa na hafla fupi ya kumuaga siku ya alhamisi tarehe 18 Julai kwenye hoteli ya Marrioti iliyopo Mabibo External, kwa wana Isimani na wanamaendeleo ikiwemo pia waandishi wa habari ambapo wanaohitaji kuhudhuria, wanaweza kuwasiliana na mratibu wa tukio hilo, Mchungaji Watende kwa simu namba 0655331000.


Katika huduma yake kwenye parokia hiyo, Padri Angelo amekuwa kichocheo kikubwa cha maendelo ambapo pia amejenga kituo cha kusaidia watoto yatima, ambapo kimekuwa msaada mkubwa kwa jamii, ikiwemo kuepusha watoto kujiingiza katika makundi ya kihuni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...