Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Jumapili, 4 Agosti 2013

LEO NI LEO NDANI YA BCIC MBEZI BEACH JIJINI DAR ES SALAAM


Viongozi wa kidini na jamii kwa ujumla, wametakiwa kuwaruhusu na kuwawezesha vijana kuhudhuria kwa wingi semina kuhusu utandawazi itakayofanyika leo kuanzia majira ya saa tatu asubuhi katika Ukumbi wa BCIC Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam.

Wito huo umetolewa na Mwangalizi Mkuu wa Wapo Mission International, Askofu Sylivester Gamanywa wakati akifundisha katika mwendelezo wa kampeni maalum ya Operesheni Takasika Jijini Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa, katika semina hiyo ambayo itahitimishwa Jumapili hii Agosti 4 mwaka huu, amepanga kufundisha kuhusu athari za ulevi na utandawazi jinsi vinavyoathiri vijana kitabia na kimaadili na jinsi ya kukabiliana nazo na kuzishinda.

Ibada za Operesheni Takasika ambazo zilianza rasmi Juni 2 mwaka huu, hufanyika kila Ijumaa kuanzia saa kumi jioni ambapo kwa siku za Jumapili, Ibada hizo huendeshwa kuanzia saa nane mchana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...