Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Alhamisi, 15 Agosti 2013

WATU WAKO "VERY BUSY" KUMTAFUITA MUNGU KWA KUSOMA NENO LAKE KATIKA KANISA LA YESU KRISTO LA HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASALA KWA NABII FLORA PETER. HII ILIKUWA TAREHE 28.07.2013



UJUMBE WA LEO UNATOKA KATIKA KITABU CHA KUTOKA 9:8..
Nakukaribisha sana katika mwezi huu, kabla hatuja ingia mwezi Buni tulikuwepo katika mwezi Ethanimu. Niliweza kuzungumza nikasema ndipo Bwana akasikia arufu njema, baada ya kutua ile Safina katika Mlima Hararati.

Ilipokuwa imetua ile Safina Nuhu alichukua mke wake na watoto wake, na kila mnyama aliyekuwa na uhai akamtolea Mungu, ndipo Bwana akasikia arufu njema na ya kuridhisha.
Aliposikia arufu nzuri na ya kuridhisha akasema sinta ipiga hii nchi tena, lakini ndipo tukakumbuka kipindi cha Nabii Musa,walipo kuwa wamejiinua waganga na wapiga ramli katika lile taifa. Kama wanavyojiinua hapa Tanzania, wamekuwa wakipoteza watoto kila siku, zimekuwa ni kesi za watu kufa kufa, ajali zisizoeleweka.
Sasa Mungu akaniambia jitwalie konzi ya Tanuuni, uende kuitupa juu, majivu yatatembea nchi yote, alafu ufanyavyo hivyo patatokea majipu makubwa, yenye kufura na yenye kutumbuka na kutoa usaha. Ili waiachie nchi yetu tupate maendeleo, tufanye kazi, watu wafanikiwe, watu wamuone mungu, fanya kazi kwa bidii utafanikiwa.
Ninakwenda kumkamata na kumwaribu adui yako, watupishe tupite, lazima watupishe tupenye, lazima ukuta uanguke tuvuke. Yeyote aliyekuzuilia mambo yako nakwambia leo lazima atapisha utapita, haijalishi leo nakwenda kuteketeza mahitaji yetu. Ndipo litatokea vumbi kwa maadui zako, wataota majipu yenye kufura na kutumbuka, mengine yatakuja mpaka usoni.
Sikubali kuona watu wanateseka, ninakataa lazima iwe. Aliyekuchukulia mume litatokea jipu lenye kufura na kutumbuka tena lenye usaa yatatokea. Nakwambia hata akienda kwa waganga watashindwa kupiga ramli, leo ni siku yako ya kukukomboa juu ya adui yako, aliye zuia muujiza wako nakwambia leo ni siku yake ya kupigwa.
Ndio maana wanasema Yesu alimpiga Yeriko kuta zikaanguka, na mimi napiga kuta zianguke, lazima kuta zianguke ndani yako, hata kama ameweka jiwe la gubegube leo nalivunja lazima iwe. Lazima leo niangushe ngome, kunatatizo linalokusumbua leo lazima liangushwe, kama Daudi alivyompiga Goliati jiwe moja akaanguka.
Aliyechukua mume wako leo ataachia, aliyezuia cheo chako namtwanga leo, Nabii ni kichwa cha Mungu ameyasikia Mungu mateso yenu. Ameniambia shuka nami niatapiga maadui zenu, tumechoka kuonewa, lazima Yesu aonekane.
Bwana akawaambia Musa na Haruni, jitwalieni konzi za majivu ya tanuuni kisha Musa na ayarushe juu kuelekea mbinguni, mbele ya Farao. Nayo yatakuwa ni mavumbi membamba juu ya nchi yote ya Misri; Farao ni adui anayekutesa, yaani Nabii Flora ayarushe juu yale majivu ya tanuuni, Misri ni watu wasiomjua Mungu.
Nayo yatakuwa ni majipu yenye kufura na kutumbuka, juu ya wanadamu na juu ya wanyama katika nchi ya Misri. Basi wakatwaa majivu ya tanuuni na kusimama mbele ya Farao; wanaokusema juu yako, wanaokuloga usiku kucha, utakuwa na majipu makubwa yenye kufura nakufungua. Farao ni ugonjwa ulionao, pamoja na mateso uliyonayo, wamezuia usiolewe wamefunga funga uchumba wako lakini leo nimesimama.
Lazima umuone Yesu alzima ufanikiwe, aliyezuia atapata majibu, anayezuia usiolewe majipu yatakuja kwake, anayezuia usizae, nakutamkia atapata majipu yenye kufura. Anayezuia mambo yako kwamba usifanikiwe.
Basi wakayatoa majivu ya tanuuni, kasha Musa akayarusha juu mbinguni; umepima ukakuta bado tarajia uzima, lakini uzima upo mahali hapa. Aliyeokoka hawi na Virusi, ukija hapa lazima Virusi viondoke, Mungu wetu ni mwaminifu, tumesikia kijana aliyekuwa amefungungwa kifungo cha maisha ameweza kutoka. Na pia tumesikia ushuhuda watu wamepona magonjwa yote UKIMWI, Kansa wamekuja na vyeti vyao.
Picha zimepigwa na Rumafrica +255 715 851523
You might also like:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...