Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Jumatatu, 12 Agosti 2013

RUMAFRICA YAFUNGULIWA MACHO JUU YA UZINDIZI WA ALBAMU YA SHUJAA SIKU YA TAREHE 01.09.2013 UBUNGO PLAZA JIJINI DAR


Ki ukweli mimi kama Rumafrica sijui zimebaki siku ngapi ila ninachojua ni kwamba tarehe 01.09.2013 ndio siku ya uzinduzi wa albamu ya SHUJAA ya Neema Gaspa.

Kilichonishangaza na kunifanya nijiwekee pesa kwaajili ya kiingilio ni ule  ujumbe alioubeba mwana wa Mungu Neema Gaspa katika albamu yake. waimbaji watakaoimba ni wale ambao kiukweli nyimbo zao zinaupako mkubwa na hili si la kuficha kwani unajua....

Nilikuwa najiuliza ni kiasi gani kinahitajika ili watu wote waingie katika kujimwaga kwa Yesu. Neema aliweza kuniambia ya kwamba, watoto ni Shilingi 2,00/= viti vya kawaida in sh. 5000/= na VIP ni sh. 10,000/= na issue nzima inaanza saa 7 na kuendelea mpaka hapo baadae.

Nikajiuliza tena, hivi Neema anaupako gani mpaka akamshauri Mh. Samweli Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania  kuwa mgeni rasmi, Roho wa Bwana akasema, "Kwa Mungu kila jambo linawezekana"

Mimi kama Rumafrica ninaomba sana Mungu anipe uhai na afya njema siku hiyo nishuhudia kazi ya Mungu inavyofanyika na watu wake wanaompenda Mungu na kufanya kazi yake bila kujali gharama.

Unaweza pia ukajiuliza kuwa tiketi utapata wapi?  Ninaamini unajua sana kituo cha Radio cha Wapo (Kurasini) na Praise Power (Mikocheni) huko ndiko unaweza kupata na kama unaona mbali au umebanwa na huwezi kwenda huko basi njoo siku hiyo ya tamasha na utapata mlangoni. Halijaharibika jambo.

Ninamshukuru sana Mungu kwa kuweza kumuwezesha Neema Gaspa kufanya kazi ya matangazo na RUMAFRICA.
Kazi imefanywa na Rumafrica Tanzania. Wasiliana naye kwa simu +255 715851523 au kwa B/Pepe: rumatz2012@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...