Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Jumatatu, 12 Agosti 2013

PASCAL CASIAN AFUNGUKA JUU YA MAFREEMASON ALIOKUWA NAO ENZI HIZO


Mwanamuziki wa Injili ambaye aliwahi shiriki Bongo Star Search Pascal Casian amefunguka kupitia gazeti la Nyakati wiki hii kudai kuwa anawajua watumishi wa Mungu waliopo hapa nchini ambao ni Ma-Freemasons. Mwanamuziki huyo ambaye amedai kutokana na changamoto za Maisha alijikuta akidondokea katika kundi hilo la "Wajenzi Huru" ambao inasadikika walianzia kazi zao rasmi wakati wa Ujenzi wa Mnara wa Babeli.


Mwanamuziki hiyo kupitia gazeti la Nyakati la tarehe 04 August, 2013 alidai wengi wa watumishi wa Mungu maarufu hapa nchini na wenye ushawishi katika Jamii ni Ma-Freemasons na anawafahamu wachungaji hao kwakuwa walikuwa wote enzi hizo kabla neema ya kutoka Katika Kundi hilo haijamzukia. Mwanamuziki huyo amezidi kufunguka na kutangaza kuwa ameandaa albam ya nyimbo pamoja na Filamu yenye kuonesha uhalisia wa mambo hayo ili kuzidi kufungua macho ya Wakristo ambao anaamini wengi wao hawayafahamu mambo hayo.

Blog hii na Kipindi mwenza Cha Chomoza Kitakuletea full story ya Mwanamuziki Huyu wa Injili na Madai yake dhidi ya watumishi wa Mungu ambao kwa maelezo yake wameshaanza kumtishia maisha.

Inatoka kwa Samsasali ze blogger

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...