Kardinali Dolan kwenye mojawapo ya mahojianoNBC. Picha kwa kwa hisani ya CP kama ilivyona-
kiliwa kutoka kituo cha TV cha NBC kwenye kipindi cha Today.
Siku chache baada ya kauli ya Papa Francis kuibua mijadala maeneno mbalimbali ulimwenguni kuhusiana na kauli ya kanisa na mashoga/wasagaji. Rais wa baraza la maaskofu wa katoliki nchini Marekani amejitokeza na kufafanua kauli ya Papa, na kusema kuwa imetafsiriwa tofauti miongoni mwa watu.
Kardinali Timothy Dolan, ambaye pia anatoka dayosisi ya New York amesema wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha CBS kwenye kipindi cha CBS This Morning kuwa kauli ya papa ilihusu kuwakubali mashoga, ila si tabia za kishoga.
"Papa angekuwa wa kwanza kusema, kazi yangu si kubatilisha mafundisho ya kanisa. Kazi yangu ni kuyawasilisha kwa uwazi ipasavyo" Ananukuliwa Dolan akisema hivyo siku ya Jumanne wakati wa mahojiano.
Kardinali Dolan pia ameeleza kuwa si Papa wala Kanisa Katoliki ambalo liko tayari kuruhusu jambo hilo.
Christian Post imeandika
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni