Na
hii yote ni kutokana na upendo wa Mungu kwa watu wake. Juhudi zako za
kumtafuta Mungu na kuwa mwaminifu zitakufanya ujibiwe swali lako. Zidi
kumtumikia Mungu na kuachana na dhamibi, kuwa mtoaji ili kazi ya Mungu
izidi kukua, fanya yaliyo ya Mungu na Mungu atakubariki na kukutatulia
matatizo yako. Soma shuhuda hizi
JINSI YA KUFIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASLA KWA NABII FLORA PETER
Kama unatokea Mwenge, panda magari ya Tegeta, shuka Mbezi Mbuyuni, uliza kanisani kwa Nabii Flora peter
SHUHUDA MBALIMBALI
BABA ANAMSHUKURU MUNGU KUMPONYA MWANAYE

Bwana
Yesu asifiwe; madhabahu hii ya Nabii Flora, siku moja nilikuwa kazini,
ilikuwa muda wa saa kumi nikapigiwa simu mtoto wanaumwa, nikachuwa
usafiri kweli nikafika mpaka Tegeta, nikakuta mtoto wangu anataka
kukimbia, nikamkamata tukalala tumemshikilia mpaka asubuhi. Asubuhi ile
tukachukuwa usafiri tukaja hadi Hospitali moja ipo Kibaoni, basi
wakamwangalia mtoto wakamwandikia dawa, alikuwa amelala bila kula kitu
chochote akatundikiwa drip. Baada ya hapo mtoto hali iliendelea kuwa
nzuri kidogo tukarudi nyumbani, tukalala ilipofika saa kumi na moja
mtoto akawa anasema Baba kuna watu wanataka kuniua hata baba na wewe
ukiwemo. Tukamrudisha Hospitali Daktari akasema tumpeleke Muhimbili,
lakini mama mmoja akasema tumlete kwa Nabii Flora. Basi tukaja hapa
tukaangaika naye mpaka tukafika kwenye meza ya Nabii Flora, Nabii
akasema huyu mtoto atapona wala msiwe na wasiwasi. Nilijisikia kuwa na
imani kwa sababu niliangaika sana, na sasa hivi namuamini Mungu wa
madhabahu hii ya Nabii Flora, naimani mwanangu amepona kabisa kwa uwezo
wa mwenyezi Mungu wa Nabii Flora
DADA ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA MDHAMINI KWAAJILI YA KAZI YAKE YA MUZIKI WA INJILI
Bwana
Yesu asifiwe; namshukuru Mwenyezi Mungu wa mahali hapa anatenda
makubwa, Jumapili iliyopita nilikutana na mtumishi wa Mungu Nabii Flora,
nikamweleza kuhusu matatizo yangu, nikamwambia nimechoka kuitukuza
dunia.
Sasa
kwa nini hii sauti nzuri iendelee kutukuza walimwengu wakati yeye
aliyenipatia hii sauti nishindwe kumuinua, nahitaji sasa hivi kumtukuza
ila sina uwezi, nimetengeneza sasa hivi nyimbo moja. Nabii akaniambia
hii wiki haitapita utapata mfadhili, alipokuja huyo mfadhili siku ya
kwanza alikuwa ananishangilia tu hakuniambia chochote, siku ya pili
akaniambia dada unasauti nzuri kuanzia leo mimi nitakuwa mfadhilia wako.
Nikasema
Mungu wangu ambaye anamuinua Nabii Flora mahali alipo pale Salasala
wakati huu akipiga goti lake yeye kwaajili yangu mimi basi akubariki
wewe kazi yako ya mikono unayofanya, huku unakokwenda urudi basi
akubariki na wewe uweze kunibariki. Akaniambia naenda Iringa kununua
uwanja mkubwa sana kwa sababu ya kazi zangu, nikirudi uniambie mahitaji
ya studio ni shilingi ngapi ili niweze kukudhamini.
DEO DAUDI ANAMSHUKU MUNGU BAADA YA KUTUMIA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA AMERUDISHWA KAZINI
Bwana
Yesu asifiwe, naitwa Deo Daudi; nilikuja hapa nilikuwa nasumbuliwa sana
na viupele katika mwili wangu, pia nilikuwa sina kazi, kwa hiyo
nilipofika hapa Nabii Flora akanipa sabuni. Baada ya kuondoka hapa
nilipofika nyumbani nikaogea sabuni hii, nilimsalimia mama mwenye nyumba
akakataa kuitika, kumbe ni sabuni hii imeshaleta madhara katika ile
nyumba. Asubuhi nilipoamka nikamsalimia tena akakataa kuitika, nikasema
ngoja niendelee kuitumia hii sabuni nione nini kitatokea, ilipofika siku
ya tatu, kuna sehemu nilikuwa nafanya kazi lakini nilisimamishwa, bosi
akanipia simu akaniambia njoo uendelee na kazi. Namshukuru sana Mungu wa
Nabii Flora kwa aliyonitendea kwa sababu sikutegemea kama nitapata
miujiza kama hii, na mama mwenye nyumba sasa nikimsalimia anaitika,
shetani maeshindwa kwa jina la Yesu.
FLORA JUSTINE ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA MAOMBI YA NABII FLORA MDOGO WAKE ALIYEKUWA AMEKAMATWA NA MAPILOSI AMEACHILIWA
Bwana
Yesu asifiwe, naitwa Flora Justine; nilikuja hapa mdogo wangu alishikwa
akawekwa rumande, alizuiliwa hata zamana asiwekewe, mama alizunguka
huku na huku lakini ilishindikana. Nikamwambia mama subiri naenda kwa
Nabii Flora utasikia mdogo wangu ametoka, nilipokuja hapa akaombewa,
ilipofika saa tatu mama akanipigia simu, akasema mapolisi wamempigia
simu kwamba mdogo wangu ameruhusiwa kutoka. Namshukuru Mungu wa Nabii
Flora mdogo wangu ametoka, alikuwa mkoa wa Musoma.
EDNA MPANZI ANAMSHUKURU MUNGU KUPATA KAZI
Bwana
Yesu asifiwe, naitwa Edina Mpanzi; namshukuru Mungu, mimi nilipofika
kwenye madhabahu hii nilikuwa sina kazi, hata nauli ya kuja hapa
nilikuwa Napata kwa shida, naombaomba tu. Lakini sasa hivi ninamshukuru
Mungu nimepata kazi kwenye madhabahu hii hii ya Nabii Flora.
GERALD MICHAEL ANAMSHUKURU MUNGU RAFIKI YAKE AMETOKA JELA PIA YEYE MWENYEWE AMEPATA KAZI ALIYOKUWA ANAITAKA
Bwana
Yesu asifiwe, naitwa Gerald Michael; namshukuru Mungu kwa mambo makuu
aliyoyatenda, kulikuwa na rafiki yangu alikuwa amewekwa ndani na
kulikuwa hakuna zamana wala kutoa rushwa. Lakini Mungu wa mahali hapa
anayetenda makuu, ilikuwa mwaka jana mwezi wa 12, nikamsii Mungu, Mungu
akatenda, akapata kuwa huru. Mwezi wa pili mwanzoni bado Mungu
aliendelea kututenda, tulikuwa tunajenga saiti moja kwa askari mmoja,
basi alitaka kufanya tena hila ili nisirudi tena kule kazini, Mungu
akaziba ndani yake, niliondoka saa kumi usiku na nilipanga kuondoka saa
kumi na moja. Basi namshukuru Mungu ameendelea kuonekana tena, nilienda
sehemu moja kuomba kazi, nilipofika pale nikanyimwa kazi, lakini
nikapata kazi moja ambayo sikuifuraia lakini nikafanya hivyo hivyo. Siku
ya pili nikaenda nikawaambia kazi hiyo siifanyi nataka kazi nyingine,
Mungu alitenda kitu cha ajabu sana, pale kazini walikuwa wanatoa pesa
ndogo sana, lakini baada ya kufika mimi zile siku mbili mshahara
ukaongezwa, na walikuwa hawajawai kununuliwa juice hata siku moja na
Engineer, lakini siku hiyo walinunuliwa. Wakasema ni nini kwani una nini
wewe, nikawaambia ninamwamini Mungu anayetenda, na ninatokea kwa Nabii
Flora. Siku ya jana tuliambiwa na bosi tufanye kazi lakini miili yetu
ilikuwa imechoka, tukasema hatufanyi kazi, kwa hiyo hatukufanya kazi, na
leo nikasema naondoka kwenda Kanisani Mungu utende kazini kwa sababu
nikiondoka anapewa mtu mwingine, namshukuru Mungu mvua inanyesha kazi
hakuna imesimamishwa.
GLADNESS JACKSON ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA STICKER, NYUMBA WALIYOKUWA WANATAKA KUZULUMIWA IMESHINDIKANA KUZULUMIWA
Bwana
Yesu asifiwe, naitwa Gladness Jackson; nauhakika kabisa watumishi wa
Mungu pale mbele nilishawahi kuongea nao kupitia picha ya nyumba yangu,
hii sticker ya Nabii Flora imefanya mambo makubwa sana kwangu ambayo
miaka 4 iliyopita sikutegemea kama itatokea. Hii sticker nilinunua muda
mrefu kulikuwa na kaka yangu anaumwa, na shangazi yangu alikuwa anaumwa,
na sisi tulikuwa na matatizo ya nyumba, sasa nikawa najishahuri sijui
niiweke kwenye picha ya nyumba yangu, sijui niiweke kwa shangazi au
nimpelekee kaka yanagu.
Nilipokuwa
nawaza niibandike kwenye picha ya nyumba yangu, nikawa nimeibandika
chumbani kwangu, nikamwambia mume wangu tuangalie hii picha tumuombe
Mungu hii nyumba itakuwa ya kwetu. Sasa Ijumaa nikawa nimeenda kazini,
niliporudi mume wangu akaniuliza Jumatatu unaenda kazini, nikamwambia
ndio kwani kuna sikukuu yoyote, akaniambia hapana hakuna sikukuu,
nikamwambia kwani kuna nini, akaniambia ngoja kwanza tule alafu
nitakwambia kuna kitu gani kimetokea. Kwenye hii nyumba madalali
wameshapelekwa nyumba inauzwa milioni 80, wakati sisi tulinunua kiwanja
milioni 1 na tukajenga hii nyumba mpaka hapa tulipofikia. Basi
tulipokuwa chumbani nikawa sina amani, nikamwambia mume wangu kwani kuna
nini, akaniambia tusalikwanza maana hatujasali. Ilikuwa juzi Ijumaa
nilikuwa fellowship mchungaji akanipigia simu akaniambia njoo officen
kwangu, alipoenda akamkuta Yule mchungaji ambaye lile eneo tulilinunua
kwake, tukawa tumeelewana tulipe milioni 25 ili kufidia kile kiwanja
ndugu yake kutoka Arusha amekuja yupo pale kwa mchungaji. Yule baba
akasema kwa kweli hii imeshakuwa ni laana katika ukoo wetu, hatutapenda
kitu kama hiki kitokee wala hatutaweza kujenga wala kuishi kwenye nyumba
hii, akasema kesho Jumatatu tutakuja hapa officen Mr. Kimaro utakuja na
mke wako na nyie wengine mtakuja tukutane hapa, tunataka hili tatizo
liishe kuna kiwanja kipo Tabata Segerea tutaenda kukiangalia, tutapatana
na Yule mtu mtanunua mumfidie Yule mchungaji kile kiwanja, ambacho Yule
mchungaji tulikabidhi milioni 15 na risiti tunazo. Kwa hiyo Mungu wa
Nabii Flora ameenda kutenda miaka 4 ambayo tuliishi kwa mateso.
HAPPINESS ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI
HAPPINESS ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI
Bwana
Yesu asifiwe, naitwa Happiness; namshukuru Mungu nilikuja hapa
ninawashwa, Nabii aliniambia nilete maji akayaombea. Yale maji
nikayaogea, na nikayanawia huku chini, yaani nilijiona kama naota mpaka
sasa hivi siwashwitena, sasa hivi nimepona kabisa namshukuru Mungu, pia
napenda kuwaambia watu wote tumwamini Mungu.
HENDREW ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA NA SASA AMEPATA KAZI