Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Alhamisi, 20 Februari 2014

KITUNDA KUGUSWA NA NGUVU ZA MUNGU HUMAPILI HII


Maono ya mtumishi wa Mungu mama mchungaji Happyness Madembwe juu ya ibada ya sifa na kuabudu bado yanaendelea kutenda kazi ndani ya uwepo wa Mungu na kwa wale waliopata nafasi ya kuhudhuria ibada hiyo wamekuwa mashuhuda jinsi Mungu anavyo wahudumia watu wake.

Ikiwa ni mwendelezo wa ibada hizo kwa kila jumapili ya mwisho wa mwezi ibada hiyo hufanyika katika kanisa la TAG KITUNDA KATI MIRACLE CENTRE lakini kwa jumapili hii ya tarehe 23 mwezi wa huu wa pili ibada hiyo itafanyika kanisa la TAG KIVULE NYANG'ANDU kuanzia saa 8 mchana hadi saa 12 jioni lengo likiwa ni lilelile Roho mtakatifu kuwahudumia watu ikiwemo kuponywa,kujazwa Roho mtakatifu,na Mungu akihudumia juu ya mahitaji mabalimbali.

Ibada hiyo itaongozwa na timu ya kusifu na kuabudu iitwayo Haleluya ilyopo chini ya mama mchungaji Happyness pamoja na kwaya na waimbaji binafsi alikwa hakuna kiingilio mama Happyness Madembwe anawakaribisha wote kufika katika ibada hiyo ili kukutana na uweza wa Mungu

Mama mchungaji Madembwe akiwa katika kumwabudu Mungu.





Hakika wenye nguvu ndio watauteka...




Watu wakiwa uweponi mwa BWANA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...