Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Jumatatu, 3 Februari 2014

MESS JACOB CHAENGULA SIKU YA JANA ATOA AHADI YA MIFUKO KUMI YA SIMENT KATIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASALA KWA NABII FLORA PETER


Kutoka kulia ni mtumishi wa Mungu, Mess Jacob Chengula

Mess Jacob Chengula kwa asiyemjua ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania. Siku ya Jumapili ya jana 02.02.2014 aliweza kutoa ahadi yake ya kuchangia kazi ya Bwana kusonga mbele kwa kutoa mifuko kumi (0) ya simenti. Akiongea madhabahuni alisema anamshukuru sana Mungu kwani amembariki sana na ameona hakuna sababu yeyote itakayomzuia kutoa shukrani zake kwa Mungu.

Mess Jacob Chengula amekuwa msaada mkubwa sana katika jamii, amekuwa akijitoa katika kazi ya Bwana bila ya kuangalia fedha kama watu wengine wanavyofanya, amekuwa akitoa misaada kwa yatima na wasiojiweza, amekuwa akichangia sana kazi ya Mungu kusonga mbele kwa mali zake na akili zake. Huu ni mfano wa kuigwa na watu wengi.

Dancers wa Mess Jacob Chengula

Siku ya jana baada ya kutoa ahadi yake, aliweza kumuimbia Mungu. Waumini walibarikiwa sana na uimbaji wake na kufanya kujaa madhabahuni kumshangilia na wengine wakiwa busy kumpiga picha kwa kupitia simu zao. Hii inaonyesha kwamba Mungu ameikubali huduma yake ya uimbaji.

Siku oya tarehe 02.Machi. 2014 saa 6 mchana atakuwa anazindua albamu yake ya Mungu wetu habadiliki katika ukumbi wa UBUNGO PLAZA ambapo mgeni rasmi atakuwa ni Naibu Waziri wa Mawasiliano Tanzania, Mh. Januari Makamba, na kutakuwa na waimbaji 20 watakaoimba siku hiyo kwa utukufu wa Mungu Baba. Unakaribishwa sana siku hiyo, kiingilio ni Tshs. 10,000 kwa VIP na Tshs. 5000 kwa viti vya kawaida.

KARIBU SANA UBUNGU PLAZA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...