Tangazo

Tangazo

NEEMA GASPA KUACHIA ALBAMU MPYA YA NI SHUJAA...

Jumanne, 18 Februari 2014

MUNGU MWAMINIFU!


Wakati Mwingine unapatwa na mambo ya kuumiza sana moyo wako, inawezekana uliamini sana mtu fulani na akafanya tofauti na tarajio lako au akakutendea jambo ambalo limekuumiza sana…. Inawezekana tukio fulani limetokea la huzuni na kusikitisha na limeacha majeraha moyoni kiasi kwamba unaona maisha hayana maana tena….

Kuna wakati ungependa hata kumuomba Mungu akuchukue uondoke duniani….. Hata wakati wa kuomba unakosa cha kusema…hali hii huitwa pia ni kukosa MATUMAINI… Neno hili limekuja kwa nguvu kwangu kukwambia kwamba MUNGU NI MWAMINIFU, “He is too faithful to fail”… wakati huu ni wakati wa kuangalia Uaminifu wa Mungu – naye ni mwaminifu kukupa TUMAINI kipindi cha maumivu…naye Atabadilisha hali mbaya kuwa Njema kwa utukufu wake… Ataondoa maumivu yako na kukupa furaha, Amani na kujaza moyo wako kwa Upendo wake ambao haulinganishwi na chochote….Kwamba atafanya kwa njia gani na lini sijui, ila kwamba atafanya NAJUA kwa HAKIKA – maana MUNGU NI MWAMINIFU.

Source: Strictly Gospel

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...